UKAWA walivyogawana kura udiwani kata 22 hadi kupelekea ushindi wa CCM

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,683
Baada ya uchaguzi mdogo kumaIizika kata 22 na CCM kuibuka na ushindi imebainika kuwa moja kati ya kitu kilichowafanya CCM kushinda ni UKAWA kugawana kura baada ya kila chama kuweka mgombea wake.
na hii ndivyo ilivyotokea.

1. Kata ya Kijichi iliyopo jijini Dar

CCM 7647
CUF 4574
CDM 3433

Ukijumlisha za CUF na CDM, UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda.

2. Kata ya Mateves iliyopo Arumeru Magharibi
CCM 2045
CHADEMA 1966
NCCR 897

Kama UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda kata.

3. Kata ya Ngarenanyuki
CCM 1746
CHADEMA 1556
NCCR 87

Hapa UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda

4. Kata ya kiwanja cha Malta, Halmashauri ya Kwimba
CCM 1997
CUF 1725
CHADEMA 422

Hapa UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda

5. Kata ya Nkome, Halmashauri ya Geita
CCM 5443
CUF 3035
CDM 2333

6. Kata ya Misugusugu, Kibaha mjini
CCM 1545
CHADEMA 1525
CUF 55
ACT 66

7. Kata ya Kasansaaa, Halmashauri ya Katavi
CCM 1494
CHADEMA 1088
NCCR 97

8. Kata ya Mkalama, Halmashauli ya Singida
CCM 1944
CHADEMA 1133
NCCR 102

9. Kata ya Isagehee, Halmashauli ya Kahama.
CCM 1562
ACT 578
CHADEMA 439
CUF 30
NCCR 11
CHAUMA 11
Kura zilizoharibika 49 ila hapa upinzani wangejipanga vizuri na kuweka mgombea mmoja wangeshinda tu.

Hii ndo tathmini ya uchaguzi.
 
ila sio lazima wangeungana wapinzani kuwa wangeishinda CCM. hilo imekaa kinadharia tu!
Ila kiuhalisia unaweza ukanganisha vyama mfano CUF na CDM akasimamishwa mmoja toka CUF. Halafu watu wachache wa CDM wasipendezwe na hilo basi aidha wakasusa kupiga kura au wakaona bora waipe CCM halafu siku ya mwisho matokeo yakaenda kwa CCM.
 
Daaa. Haya ndio mambo ya Lipumba na wenzake kutumika na CCM. Wamefanya kazi waliyotumwa. Ila niisemee Kata ya Isaghehe huko kahama. Kiukweli kahama kuna shida kubwa ya Uongozi pale Wilayani kuanzia Mwenyekiti, katibu na timu yake. Wanajua udhalimu walioufanya kwa katibu Arnold Nshibo na mwenezi yule Mustapha aliyepo gerezani Hadi Leo. Mbowe chukua hatua kahama pameoza wamebaki wapiga deal uongozini.
 
Hiyo ilikuwa ni strategy ya makusudi ya CCM kwa kuwaonga baadhi ya ya viongozi wa UKAWA kusudi wavuruge umoja unadhani hata wewe ungepewa bilioni 'uende Rwanda kufanya utafiti' ungeacha au kuingiziwa bilions kwenye akaunti ya mke wako unayempenda kuliko kitu chochote hapa Dunian.Wanachotakiwa UKAWA kwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao kwa kuwaondoa mamluki woote bila kujali wanalindwa na nani awe msajili au geshi la polisi vinginevyo CCM haitakaa iondoke....
 
Uhalisia ni kuwa maccm inaungwa mkono kwa chini ya 47%

Hapo ukiondoa figisufigisu unapata wanaoiunga mkono ni 25%.
 
Hiyo ilikuwa ni strategy ya makusudi ya CCM kwa kuwaonga baadhi ya ya viongozi wa UKAWA kusudi wavuruge umoja unadhani hata wewe ungepewa bilioni 'uende Rwanda kufanya utafiti' ungeacha au kuingiziwa bilions kwenye akaunti ya mke wako unayempenda kuliko kitu chochote hapa Dunian.Wanachotakiwa UKAWA kwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya uchaguzi ujao kwa kuwaondoa mamluki woote bila kujali wanalindwa na nani awe msajili au geshi la polisi vinginevyo CCM haitakaa iondoke....
KWANI MGAWANYO WA KATA KABLA YA UCHAGUZI WA MADIWANI UKAWA KATI YA CHADEMA,NCCR,NLD ,CUF WALIKUBALIANA VIPI KATA IPI ITAENDA CHADEMA, KATA IPI ITAENDA NCCR, KATA IPI ITAENDA NLD
 
Baada ya uchaguzi mdogo kumaIizika kata 22 na CCM kuibuka na ushindi imebainika kuwa moja kati ya kitu kilichowafanya CCM kushinda ni UKAWA kugawana kura baada ya kila chama kuweka mgombea wake.
na hii ndivyo ilivyotokea.

1. Kata ya Kijichi iliyopo jijini Dar

CCM 7647
CUF 4574
CDM 3433

Ukijumlisha za CUF na CDM, UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda.

2. Kata ya Mateves iliyopo Arumeru Magharibi
CCM 2045
CHADEMA 1966
NCCR 897

Kama UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda kata.

3. Kata ya Ngarenanyuki
CCM 1746
CHADEMA 1556
NCCR 87

Hapa UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda

4. Kata ya kiwanja cha Malta, Halmashauri ya Kwimba
CCM 1997
CUF 1725
CHADEMA 422

Hapa UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda

5. Kata ya Nkome, Halmashauri ya Geita
CCM 5443
CUF 3035
CDM 2333

6. Kata ya Misugusugu, Kibaha mjini
CCM 1545
CHADEMA 1525
CUF 55
ACT 66

7. Kata ya Kasansaaa, Halmashauri ya Katavi
CCM 1494
CHADEMA 1088
NCCR 97

8. Kata ya Mkalama, Halmashauli ya Singida
CCM 1944
CHADEMA 1133
NCCR 102

9. Kata ya Isagehee, Halmashauli ya Kahama.
CCM 1562
ACT 578
CHADEMA 439
CUF 30
NCCR 11
CHAUMA 11
Kura zilizoharibika 49 ila hapa upinzani wangejipanga vizuri na kuweka mgombea mmoja wangeshinda tu.

Hii ndo tathmini ya uchaguzi.

bado kuna mazuzu huku yanataja neno ukawa , kama vile wamemezeshwa ngisi
 
Daaa. Haya ndio mambo ya Lipumba na wenzake kutumika na CCM. Wamefanya kazi waliyotumwa. Ila niisemee Kata ya Isaghehe huko kahama. Kiukweli kahama kuna shida kubwa ya Uongozi pale Wilayani kuanzia Mwenyekiti, katibu na timu yake. Wanajua udhalimu walioufanya kwa katibu Arnold Nshibo na mwenezi yule Mustapha aliyepo gerezani Hadi Leo. Mbowe chukua hatua kahama pameoza wamebaki wapiga deal uongozini.
VIPI KUHUSU NCCR MAGEUZI NDANI YA UKAWA ILIKUWA NA NAFASI GANI
 
Hii ndio maana aliletwa mtu anaeitwa Lipumba.
Kuja kwa Lipumba si Bahati mbaya bali ni mkakati maalum wa ccm kuakikisha kuwa wanabaki madarakani na hii lazima upinzani waifanyie kazi haraka.
Ccm wanatumia mbinu ya divide and rule. Huwa nashangaa sana watu wasio na hilo na kuendelea kumshabikia Lipumba.
Lipumba ni kirusi kikali sana ndani ya ushindi wa wapinzani
 
Vijijini ccm inakubalika sana na wameinvest zaidi vijijini ambapo ndio kuna wapigakura wengi zaidi ya 70% ipo vijijini
 
KWANI MGAWANYO WA KATA KABLA YA UCHAGUZI WA MADIWANI UKAWA KATI YA CHADEMA,NCCR,NLD ,CUF WALIKUBALIANA VIPI KATA IPI ITAENDA CHADEMA, KATA IPI ITAENDA NCCR, KATA IPI ITAENDA NLD
Kaka wasingeweza kukubaliana kwa vile CUF walishavurugwa bara. Kupitia Mwenyekiti wao anayetambulika kwa msajili ili kuwa lazima waweke mgobea kwa maagizo ya kutoka Thithiem..So hata wangefanyaje ilikuwa ni lazima CUF waweke wagombea sehemu zoote.Na walifanya hivyo makusudi kwa maelekezo maalum.
 
Back
Top Bottom