UKAWA walivyogawana kura udiwani kata 22 hadi kupelekea ushindi wa CCM

bado kuna mazuzu huku yanataja neno ukawa , kama vile wamemezeshwa ngisi
NDIO MAANA NIKAULIZA HIVI KABLA YA UCHAGUZI MGAWANYO WA KATA UKAWA WALIKUBALIANA NINI,

KAMA CUF WALISEMA HAWATASIMAMISHA VIPI KUHUSU NAFASI YA NCCR YA MAGEUZI NA NLD NDANI YA UKAWA HAPO WALIKUBALIANA KATA IPI NA IPI ITAENDA NLD NA NCCR
 
Ubinafsi unawaponza watanzania sana. Hakuna dhamira ya kuishinda CCM bali kila mmoja anataka awe yeye kiongozi
 
Ubinafsi unawaponza watanzania sana. Hakuna dhamira ya kuishinda CCM bali kila mmoja anataka awe yeye kiongozi
NDIO MAANA NIKASEMA KAMA ACT,NCCR,CHADEMA,CUF WANGEKUBALIANA KUWEKA MGOMBEA MMOJA KILA KATA NI DHAHIRI UPINZANI UNGEONGOZAAAA TUU.

ILA SHIDA NI KWAMBA CHADEMA WANATAKA, CUF WANATAKA, NCCR WANATAKA , NLD WANATAKA HAPO KURA BABU ZA UPINZANI NI LAZIMA ZITAGAWANYIKA TUU
 
Baada ya uchaguzi mdogo kumaIizika kata 22 na CCM kuibuka na ushindi imebainika kuwa moja kati ya kitu kilichowafanya CCM kushinda ni UKAWA kugawana kura baada ya kila chama kuweka mgombea wake.
na hii ndivyo ilivyotokea.

1. Kata ya Kijichi iliyopo jijini Dar

CCM 7647
CUF 4574
CDM 3433

Ukijumlisha za CUF na CDM, UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda.

2. Kata ya Mateves iliyopo Arumeru Magharibi
CCM 2045
CHADEMA 1966
NCCR 897

Kama UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda kata.

3. Kata ya Ngarenanyuki
CCM 1746
CHADEMA 1556
NCCR 87

Hapa UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda

4. Kata ya kiwanja cha Malta, Halmashauri ya Kwimba
CCM 1997
CUF 1725
CHADEMA 422

Hapa UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda

5. Kata ya Nkome, Halmashauri ya Geita
CCM 5443
CUF 3035
CDM 2333

6. Kata ya Misugusugu, Kibaha mjini
CCM 1545
CHADEMA 1525
CUF 55
ACT 66

7. Kata ya Kasansaaa, Halmashauri ya Katavi
CCM 1494
CHADEMA 1088
NCCR 97

8. Kata ya Mkalama, Halmashauli ya Singida
CCM 1944
CHADEMA 1133
NCCR 102

9. Kata ya Isagehee, Halmashauli ya Kahama.
CCM 1562
ACT 578
CHADEMA 439
CUF 30
NCCR 11
CHAUMA 11
Kura zilizoharibika 49 ila hapa upinzani wangejipanga vizuri na kuweka mgombea mmoja wangeshinda tu.

Hii ndo tathmini ya uchaguzi.
tatizo la ukawa ni ubinafsi wa chadema kutaka kuwafunika vyama vingine. Kila chama kisimame kivyake na kuhamasisha wananchi, huu umoja wa ukawa kiini macho na ubinafsi ndo vimetawala. Chadema ikubali hata siku moja kuiachia CUF jimbo la Arusha mjini basi.
 
Kwani kijichi ni kijijini.
kijichi ni mjini ila kama chadema asingesimamisha mgombea akabakia mgombea wa cuf ni dhahiri cuf ingeshinda tuu ukiangalia mgawanyo wa kura 4889 na 3784 za chadema ukiziweka pamoja tungechukua kataa
 
Kumbe CUF bado wana nguvu km ilivyoonekana kwenye kura. CHADEMA inapaswa waheshimu CUF kama chama. Wasione ni Sawa na NCCR.
CUF INA NGUVU SANA LAKINI PIA CUF INA WENYEWE NA HAO WENYEWE HUWEZI KUWAKUTA JF, HUWEZI KUWAKUTA MITANDAONI WALA KWENYE VYOMBO VYA HABARI ILA UTAWAJUA KATIKA SANDUKU LA KURA TUU.

NA SIO CUF HATA NCCR INA WENYEWE NA HAO WENYEWE UKITAKA KUWATAMBUA SUBILI KWENYE SANDUKU LA KURA.

NDIO HUU UCHAGUZI UMETOA FUNDISHO KWA UPINZANI MAANA KUNA WALISHAJIAMINISHA UPINZANI PEKEE NI CHADEMA
 
Mimi naamini baada ya kushiriki chaguzi nyingi, vyama vya upinzani, vilitakiwa viwe vimejifunza mengi. Na sasa ulikuwa ni wakati sahihi wa kusimama na fikra, mitazamo na mbinu mpya. Kuendelea kufanya vile vile, kwa namna ile ile, kwa mbinu zile zile, lazima kutaleta matokeo yale yale.

Kwenye nchi kama ya kwetu ambako demokrasia ni ya kinadharia, huwezi kushinda bila ya kwanza kufanya jitihada za kupambana na mifumo gandamizi ya demokrasia. Kwanza wanatakiwa kuondoa mifumo gandamizi ya demokrasia. Na hicho ndicho kilichofanywa na vyama vya upinzani katika nchi zote za kiafrika zilizoweza kuleta mabadiliko ya kiuongozi.

Vyama vya upinzani vya Tanzania, vimekuwa kama matawi ya CCM kwani vinaishi na kufanya siasa zao kwa hisani au kufuata maelekezo ya CCM, serikali ya CCM au vyombo vinavyofanya kazi kwa maelekezo ya CCM. Utashinda vipi kama unatenda kazi kwa kufuata maelekezo ya mpinzani wako? Jukumu la msingi la vyama vya upinzani kwa sasa ilikuwa ni kupata Katiba, baada ya kupata Katiba, watende wajibu wao kwa kufuata katiba na siyo maelekezo ya CCM au wakala wao maana CCM ni mshindani wao, utashinda vipi kwa kufuata maelekezo ya mshindani wako?

Kama vyama vya upinzani haviwezi kupigania kupata katiba nzuri, na haviwezi kufanya kazi kwa kufuata katiba bali wanataka watende kazi kwa maelekezo ya CCM, ni aheri kuacha kufikiria kuishinda CCM hata siku moja. Wao wakajua hivyo na wananchi wakajua hivyo.
Asanteeee Nimepata kitu hapa Ubarikiwe
Nadhani upo sahihi
 
Hii dhana ya kumtumia Lipumba km kichochoro haikubaliki. Vyama vijiakisi vyenyewe na kuangalia uwezo wao kusimama peke yao kabla ya kuhitaji usaidizi wa vyama vingine
 
ufipa wanachojua ni kwamba chadema isimamishe wagombea huku bara vyama vingine vikawapigie kampeni la sivyo utakuwa msalti kwikwikwi team mbowe bhana
HILI NDIO TATIZO LA SIASA NA WANASIASA KIUKWELI KATIKA HUU UCHAGUZI KILA CHAMA KILIKUWA NA NAFASI YAKE YA KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI HUU.

NCCR,CUF,NLD KUTOKUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI WA MARUDIO YA KATA KISA CHADEMA WAMEWEKA WAGOMBEA UNGEKUWA NI UENDAWAZIMU ILA UKAWA WANGEKUWA INGEKUWA KABLA YA UCHAGUZI WANGEKUBALIANA KUGAWANA KATA KAMA ILIVYOKUWA UCHAGUZI MKUU 2015 BASI NADHANI WANGEFANYA VIZULI

TATIZO LINALOWASUMBUA NI UROHO WA MADARAKA NA KWA MANTIKI HII KUELEKE 2020 HADI 2025 CCM ITAENDELEA KUSHINDA DAIMA.

MUNGU IBARIKI CCM IENDELEE KUTAWALA MILELE HADI PALE UPINZANI WATAKAPOJITAMBUA NDIO UWAKABITHI NCHI
 
Hii ndio maana aliletwa mtu anaeitwa Lipumba.
Kuja kwa Lipumba si Bahati mbaya bali ni mkakati maalum wa ccm kuakikisha kuwa wanabaki madarakani na hii lazima upinzani waifanyie kazi haraka.
Ccm wanatumia mbinu ya divide and rule. Huwa nashangaa sana watu wasio na hilo na kuendelea kumshabikia Lipumba.
Lipumba ni kirusi kikali sana ndani ya ushindi wa wapinzani
mbona mnamsema tu lipumba na wakati hata nccr wapo,chadema wote wameshiriki uchaguzi wote katika baadhi ya maeneo badala ya kuachiana....tukae tuelewe tuu chadema wants everything,chadema wana ubinafsi,chadema wanahisi wao ndo kila kitu, hawaangalii wapinzani wenzao ,na ndomaana wanataka wao tu wasimaamishe watu wengine hawataki wasisimamishe, wanatumia mgongo wa ukawa kujinasibu kuwepo na umoja lakini ni wanafiki hamna kitu....
 
Pamoja na tume ya Uchaguzi kuwa haitoi "Fair play" na matumizi mabaya ya vyombo vya dola kuibeba CCM bado wapinzani wanajimaliza wenyewe kwa kutokuwa na ushirikiano dhabiti.
inakuwaje wasishirikiane pamoja kusimamisha mgombea moja moja jama kwelu wao ni wapinzani wa kweli?
Wapinzani wasipoungana na kuwa wamoja ktk sanduku la kura kuishinda CCM ni ndoto za Alinacha.
Acheni ubinafsi wa vyama vyenu jamani...
Ktk uchaguzi huu wa marudio mgeungana na kuwa kitu kimoja, mgegawana kata kadhaa na macccm. Hii mbina haihitaji hata akili za kisomi?
MSIPOFANYA HIVYO MTAKUWA MNAPOTEZA MUDA NA RASIMALI ZENU BURE...
 
Baada ya uchaguzi mdogo kumaIizika kata 22 na CCM kuibuka na ushindi imebainika kuwa moja kati ya kitu kilichowafanya CCM kushinda ni UKAWA kugawana kura baada ya kila chama kuweka mgombea wake.
na hii ndivyo ilivyotokea.

1. Kata ya Kijichi iliyopo jijini Dar

CCM 7647
CUF 4574
CDM 3433

Ukijumlisha za CUF na CDM, UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda.

2. Kata ya Mateves iliyopo Arumeru Magharibi
CCM 2045
CHADEMA 1966
NCCR 897

Kama UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda kata.

3. Kata ya Ngarenanyuki
CCM 1746
CHADEMA 1556
NCCR 87

Hapa UKAWA wangekuwa na mgombea mmoja wangeshinda

4. Kata ya kiwanja cha Malta, Halmashauri ya Kwimba
CCM 1997
CUF 1725
CHADEMA 422

Hapa UKAWA wangeweka mgombea mmoja wangeshinda

5. Kata ya Nkome, Halmashauri ya Geita
CCM 5443
CUF 3035
CDM 2333

6. Kata ya Misugusugu, Kibaha mjini
CCM 1545
CHADEMA 1525
CUF 55
ACT 66

7. Kata ya Kasansaaa, Halmashauri ya Katavi
CCM 1494
CHADEMA 1088
NCCR 97

8. Kata ya Mkalama, Halmashauli ya Singida
CCM 1944
CHADEMA 1133
NCCR 102

9. Kata ya Isagehee, Halmashauli ya Kahama.
CCM 1562
ACT 578
CHADEMA 439
CUF 30
NCCR 11
CHAUMA 11
Kura zilizoharibika 49 ila hapa upinzani wangejipanga vizuri na kuweka mgombea mmoja wangeshinda tu.

Hii ndo tathmini ya uchaguzi.

Wapinzani ni wanafiki sana. Wengi wapo kwa ajili ya tumbo na umaarufu tu. Alafu wengi viongozi wapo kwa ajili ya sifa na kujiona kwamba wanaweza. Ndio maana wengi wanahama hama chama kimoja kwenda kingine. Shame!
 
Back
Top Bottom