UKAWA walivyogawana kura udiwani kata 22 hadi kupelekea ushindi wa CCM

KWANI MGAWANYO WA KATA KABLA YA UCHAGUZI WA MADIWANI UKAWA KATI YA CHADEMA,NCCR,NLD ,CUF WALIKUBALIANA VIPI KATA IPI ITAENDA CHADEMA, KATA IPI ITAENDA NCCR, KATA IPI ITAENDA NLD
ufipa wanachojua ni kwamba chadema isimamishe wagombea huku bara vyama vingine vikawapigie kampeni la sivyo utakuwa msalti kwikwikwi team mbowe bhana
 
Kaka wasingeweza kukubaliana kwa vile CUF walishavurugwa bara. Kupitia Mwenyekiti wao anayetambulika kwa msajili ili kuwa lazima waweke mgobea kwa maagizo ya kutoka Thithiem..So hata wangefanyaje ilikuwa ni lazima CUF waweke wagombea sehemu zoote.Na walifanya hivyo makusudi kwa maelekezo maalum.
Na hiyo ndio "FAIR COMPETITION" vyama vyote vishiriki uchaguzi
 
Nilichojifunza: CUF ya Lipumba bado ina nguvu....

ACT wazalendo wana nguvu kahama kuliko CDM.

In general Watanzania tunahitaji elimu kubwa ya kujitambua.
 
Kumbe CUF bado wana nguvu km ilivyoonekana kwenye kura. CHADEMA inapaswa waheshimu CUF kama chama. Wasione ni Sawa na NCCR.
 
Mimi naamini baada ya kushiriki chaguzi nyingi, vyama vya upinzani, vilitakiwa viwe vimejifunza mengi. Na sasa ulikuwa ni wakati sahihi wa kusimama na fikra, mitazamo na mbinu mpya. Kuendelea kufanya vile vile, kwa namna ile ile, kwa mbinu zile zile, lazima kutaleta matokeo yale yale.

Kwenye nchi kama ya kwetu ambako demokrasia ni ya kinadharia, huwezi kushinda bila ya kwanza kufanya jitihada za kupambana na mifumo gandamizi ya demokrasia. Kwanza wanatakiwa kuondoa mifumo gandamizi ya demokrasia. Na hicho ndicho kilichofanywa na vyama vya upinzani katika nchi zote za kiafrika zilizoweza kuleta mabadiliko ya kiuongozi.

Vyama vya upinzani vya Tanzania, vimekuwa kama matawi ya CCM kwani vinaishi na kufanya siasa zao kwa hisani au kufuata maelekezo ya CCM, serikali ya CCM au vyombo vinavyofanya kazi kwa maelekezo ya CCM. Utashinda vipi kama unatenda kazi kwa kufuata maelekezo ya mpinzani wako? Jukumu la msingi la vyama vya upinzani kwa sasa ilikuwa ni kupata Katiba, baada ya kupata Katiba, watende wajibu wao kwa kufuata katiba na siyo maelekezo ya CCM au wakala wao maana CCM ni mshindani wao, utashinda vipi kwa kufuata maelekezo ya mshindani wako?

Kama vyama vya upinzani haviwezi kupigania kupata katiba nzuri, na haviwezi kufanya kazi kwa kufuata katiba bali wanataka watende kazi kwa maelekezo ya CCM, ni aheri kuacha kufikiria kuishinda CCM hata siku moja. Wao wakajua hivyo na wananchi wakajua hivyo.
 
tatizo mimi nadhani labda ni aina ya upinzani tuliokuwa naoo
Nadhani tathimini aliyoitoa Tundu Lissu ina mantiki. Upinzani uliopo hauna tatizo kwa aina ya watu tulionao hapa nchini! Ukiangalia kura zilizopatikana kwa upande wa upinzani ukalinganisha na nguvu kubwa inayogandamiza upinzani, jibu liko wazi kwamba wananchi wameichoka CCM!
 
Back
Top Bottom