Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,368
Kila mji una namna yake ya kupambana changamoto..,ninachokuambia kwa sasa hata wananchi hawana tabia ya usafi..inahitajika washirikishwe na viongozi ili kujenga tabia hata nyenzo zinapokuwepo inakuwa rahisi kufanikisha.
Sio kweli kuwa wananchi hawana tabia ya usafi, bali Halmashauri ya jiji haina mikakati ya kulifanya jiji safi, ile nguvu iliyokuwa inatumika kipindi cha Nyerere iliishia wapi?, jiji lilikuwa safi mno, sasa jiji linakuwa na halmashauri ya jiji haina plan yoyote ya kuendana na kasi ya maendeleo
Kwa taarifa yako tu,
Hakuna nyumba isiyofagiliwa hapa Dar hata Tandale au Mazense,
Hakuna nyumba yenye choo isiyokuwa na ufagio wa chooni na bafuni
Hakuna nyumba isiyokuwa na kiroba cha uchafu hapa Dar
Shida ni kuwa huo uchafu wa kutoka kwenye hayo majumba unaenda wapi? Siku za mvua ndio siku za kuvubua vyoo na kutiririsha mitoni, ndio siku ya kurushia viroba vya uchafu mitaroni
Kila kona kuna gereji na hakuna utaratibu unaoeleweka wa wapi pa kuweka uchafu
Halmashauri ya jiji imefail kwenye hili na hilo sio jukumu lako wala UKAWA, Jukumu lako ni kupiga kelele na kuwaamsha Halamashauri ya jiji wafanye kazi zao ipasavyo