UKAWA wagawana majimbo 211

UKAWA wagawana majimbo 211

Wamekaa makao makuu na kugawana au wameshirikisha wa majimboni?
Bado wanaweka Urais kiporo manake hapo napo kuna kizungumkuti: Prof. Lipumba ameishasema hagombei ubunge popote kwa maana yake ni kwamba atagombea Urais.

Kimbunga

This is one step forward mlisema kugawana ubunge kitachimbika baada ya kufanikisha mmegeukia urais, mimi nafikiri kazi kubwa ilikuwa kugawana majimbo na sio urais.
 
Last edited by a moderator:
Mwisho wake wataanza kugawanyika yangu macho Sasa majimbo 28 Je kwenye URAIS? Huko ndiko kutakuwa na Vita kubwa na mwishowe watasema CCM
 
Hapa tuna-share information hatufanyi biashara.Haya ndio matumizi ya mitandao ya kijamii.Siku hizi hata picha za maiti utazikuta mitandaoni sasa sijui huko nako ni kumtangaza marehemu?

Kwa hiyo ndio hauweki details za hayo majimbo, at least by percentage?
 
Wamekaa makao makuu na kugawana au wameshirikisha wa majimboni?
Bado wanaweka Urais kiporo manake hapo napo kuna kizungumkuti: Prof. Lipumba ameishasema hagombei ubunge popote kwa maana yake ni kwamba atagombea Urais.

Shida iko wapi sasa?Mambo ya UKAWA wewe yanakuhusu nini?Acha kihererehe mtoto WA kiume,waachie kina dada.
 
Mmegawana majimbo CCM hatupo mkianza kugombana Na kutoelewana basi CCM hao.

Nyie mna chama chenu nasi tuna chetu, kila mmoja abebe mzigo wake mwenyewe
 
Shida iko wapi sasa?Mambo ya UKAWA wewe yanakuhusu nini?Acha kihererehe mtoto WA kiume,waachie kina dada.

Acha matusi Bavicha,

Kama mmeshanza kushindana kwenye majimbo 28 Je kwenye Urais na Ruzuku? Huko Si mtatoana roho kabisa?
 
Acha matusi Bavicha,

Kama mmeshanza kushindana kwenye majimbo 28 Je kwenye Urais na Ruzuku? Huko Si mtatoana roho kabisa?
Hawa watoto wamekosa malezi ya baba na mama. Wanadhani matusi ndio hoja, badala ya kujenga hoja wanakuja na matusi. Sijui ndio wanajifunza matusi huko waliko.
 
Tumaini Makene unaombwa hapa kwa uthibitisho tafadhari....

What a good news..???

Ingependeza hayo 28 Chadema ichukue hata 15 then mengine yagawanywe kwa washirika. Ila kikubwa tuyajue kwanza maana unaweza kukuta labda Chadema ina nguvu sana huko ama chama kingine kinanguvu kushinda kingine. Ingependeza tuyajue hayo majimbo waliyoshindwa kuelewana.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Kutokukubaliana ni sehemu ya siasa. Kizuri kuwe na mwafaka wa kutokukubaliana. mfano hayo majimbo 28 kila chama kipime uwezo wake...na ktk hilo ukawa inaweza kusimamisha wagombea wote (on exceptional basis). Hii itagawanya kura miongoni mwa wagombea lakini si faida kwa ccm.
 
Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA), wamegawana jumla ya majimbo 211 huku wakishindwa kuelewana katika kugawana majimbo mengine 28.

Pia,jimbo la Zitto limebaki kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Chanzo:Mtanzania

My take:
This is a significant breakthrough in achieving political changes in our country.

Habari kamili (Mtanzania)

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


KAMATI maalumu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), imekamilisha kazi ya ugawaji wa majimbo 211 ambayo ni sawa na asilimia 88 kati ya majimbo yote 239, imefahamika.

Wakati hayo yakiendelea, kamati hiyo imeshindwa kuafikiana katika majimbo 28 ambayo yanasubiri uamuzi wa wenyeviti wa vyama vinavyounda Ukawa, ambao watamaliza kiporo hicho mwezi huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa juu wa umoja huo, kutangaza mkakati wa kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo ya uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba.

Ukawa ni umoja ulioanzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, ukiundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kamati hiyo maalumu ya Ukawa, kiliiambia MTANZANIA jana kuwa kwa muda wa wiki moja sasa, kamati hiyo imekamilisha kazi hiyo kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeelezwa linaweza kutoa upinzani mkali kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu.

"Tumekutana mara kadhaa na kukubaliana kuachiana majimbo. Tulijadili katika hatua za awali, na sasa kazi imekamilika kwa asilimia 88 na kubaki asilimia 12 ambayo itaamuliwa na wenyeviti.
"Majimbo 28 ambayo tumeshindwa kupata mwafaka tunaamini kamati ya kitaifa ya Ukawa inayoundwa na wenyeviti ndiyo itatoa dira ya nini kifanyike, ingawa sisi kama kamati maalumu tumekamilisha kazi yetu.

"Kamati ilitafiti namna gani bora ya kuachiana madiwani, wabunge na rais ili tusimamishe mgombea mmoja katika kila eneo, lakini tulivutana kwani kila upande uliangalia masilahi yake, ingawa katika suala linaloitwa la ushirikiano ni lazima ukubali kupoteza sehemu na ninaamini Ukawa sasa itakuwa imara zaidi," kilisema chanzo chetu.

MAJIMBO YA DAR ES SALAAM
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya kamati hiyo maalumu, mgawanyo wa majimbo kwa Mkoa wa Dar es Salaam umeangalia vigezo vya kukubalika kwa mtu pamoja na yalipo makao makuu ya chama.
Kutokana na hali hiyo, Chadema imekubaliwa itasimamisha wagombea katika majimbo ya Ubungo, Kawe, Kinondoni na Ukonga huku CUF ikiachiwa majimbo ya Segerea, Temeke na Kigamboni na NCCR-Mageuzi ikipewa Ilala.


KILIMANJARO
Chanzo hicho kiliyataja baadhi ya majimbo ambayo yamepitishwa uamuzi kuachiwa Chadema kuwa ni Moshi Mjini, Moshi Vijijini, Rombo, Same Mashariki, Same Magharibi, Hai na Siha, huku NCCR-Mageuzi ikiachiwa Vunjo na Mwanga.


KIGOMA
Mgawanyo huo umeifanya NCCR-Mageuzi kuachiwa kusimamisha wagombea katika majimbo sita ya Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini, Buhigwe, Muhambwe, Buyungu na Kigoma Kusini na Chadema ikibaki na Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini.


MAJIMBO TATA
Katika majimbo 28 ambayo ni tata, kamati hiyo maalumu imeitaka kamati ya kitaifa ya Ukawa kuwezesha kukubaliana kwa baadhi ya vyama ambapo katika Jimbo la Mtwara Mjini NCCR-Mageuzi na CUF vinatakiwa kukaa na kukubaliana kuachiana.
Mbali na hilo pia katika Jimbo la Babati Vijijini, Chadema na NCCR-Mageuzi wanatakiwa kukaa na kukubaliana namna ya kuachiana.


MAJIMBO YA WAPINZANI
Kamati hiyo maalumu ya wataalamu wa Ukawa imeshauri kuwa kwa majimbo yanayoongozwa na wabunge kutoka upinzani kwa sasa yatabaki kwa vyama husika bila vyama vinavyounda Ukawa kuteua wagombea wengine.


WENYEVITI KUAMUA
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa ndani ya kamati hiyo maalumu, wajumbe walikubaliana kusitisha mazungumzo hayo na kuiachia kamati ya wenyeviti wa vyama kitaifa itakayokutana mapema mwezi huu.
"Kamati imefanya kazi yake na sasa tupo kwenye maandalizi ya kikao cha viongozi wa kitaifa ambao ndio watatoa dira ya namna ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao hasa kwa majimbo ambayo tumekubaliana kupitia vikao vyetu.
"Kama wakifikia mwafaka na kila chama kuridhia, ni wazi siku za Serikali ya CCM kuendelea kuwa madarakani zinahesabika," kilisema chanzo chetu.


VIONGOZI WA VYAMA WAJICHIMBIA
MTANZANIA ilipotaka kupata ufafanuzi kutoka kwa viongozi wakuu wa vyama hivyo jana, mara zote walikuwa wakisema wako kwenye vikao.
Ingawa hawakueleza ni vikao gani walivyokuwa wakihudhuria, inasemekana walikuwa kwenye vikao vya vyama vyao kujadili namna kupanga mikakati kwa majimbo 28 yaliyosalia ambayo yanahitaji kuamuliwa na viongozi wa juu wa Ukawa.
 
Kwani kutofautiana cinijambo la kawaidaa Ila mwisho wa siku nguvu ya hoja itazingatiwa
 
Mwisho wake wataanza kugawanyika yangu macho Sasa majimbo 28 Je kwenye URAIS? Huko ndiko kutakuwa na Vita kubwa na mwishowe watasema CCM

Mkuu una habari zozote za Jairo, mara ya mwisho kumsikia alikuwa katibu mkuu wizara, alikuwa muumini wa kugawa mlungula.
Samahani kwa kukutoa nje ya mada
 
Back
Top Bottom