UKAWA umebaki kuwa ukiwa! Kuntu Kikwete

UKAWA umebaki kuwa ukiwa! Kuntu Kikwete

Mwaka jana wakati wa kampeni, Mwenyekiti wa CCM Taifa pale Morogoro alitamka kuwa baada ya Uchaguzi ambao alikuwa na uhakika wa CCM kushinda, Kikundi kilichojiita UKAWA kitabadilikika kuwa UKIWA! Kuntu Mzee wangu JK. Kweli wamebaki UKIWA kwa sababu:

1. Kumbe hawakujipanga kuchukua dola na hata Mgombea hawakuwa naye!

2. Hawakuwa na Sera za kutekeleza pindi wangefanikiwa kuingia IKULU zaidi
ya kuwaimbisha vijana wimbo wa mabadiliko bila kueleza tunabadilikaje!

3. UKAWA yenyewe haikuwa na dhamira ya kutetea Katiba ya Wananchi bali ni udandiaji tu wa Treni kwa mbele ili kutafuta uungwaji mkono. Ndio maana hata Bungeni walikimbia badala ya kubaki na kupambana kwa hoja!

4. UKAWA yenyewe ilijaa maigizo kama vita vya Majimaji kwa kuaminisha watu wanashinda Uchaguzi na kuingia Ikulu bila kueleza wana shindaje bila Miundombinu thabiti ya Vyama vyao vya Mijini!

5. Vyama vyao karibu vyote havina Taasisi bali vinategemea watu binafsi kung'ara. Kwa jinsi hii kuingia IKULU itachukua miaka 50 tena labda CCM wamkate mtu wao na wao wadandie na kumtumia kama daraja.

KWELI UKAWA IMEBAKI KUWA UKIWA! BADO HAMJACHELEWA LAKINI, REJEENI CCM TUTAWAPOKEA TU!!
Mleta mada ulitaka iweje vyama vyote vishinde kwa pamoja?! Au ? Uungwana wa ukawa kukubali kuporwa ushindi kwako ni raha mustarehe. Zanzibar mlishinda nyie?! Unapojivunia chaguzi kama hizi za kwetu zisizo huru lazima utakuwa na kasoro si bure
 
Kwenye mechi ya mpira mchezaji wako akiumia huwezi kuazima mchezaji toka timu pinzani. Tabia ya upinzani kuazima mgombea kutoka ccm ndiyo imeua Ukawa
 
Enyi walevi mnapeleka wapi hii nchi.Mnaleta propaganda zisizo na mashiko.
 
Kwenye mechi ya mpira mchezaji wako akiumia huwezi kuazima mchezaji toka timu pinzani. Tabia ya upinzani kuazima mgombea kutoka ccm ndiyo imeua Ukawa
Msiwafunge wananchi kuchagua wagombee kupitia vyama vipi ?! Inaonekana anayetokea ukawa kwenda ugambani ni shujaa na anayetokea Lumumba ķwenda Ukawa ni msaliti ?!

Mchezaji wa upinzani kuhamia upande wa pili si kosa la kupigia kelele.
 
Kwenye mechi ya mpira mchezaji wako akiumia huwezi kuazima mchezaji toka timu pinzani. Tabia ya upinzani kuazima mgombea kutoka ccm ndiyo imeua Ukawa
UKAWA haijafa na haitakufa, hivi sukari vp? Msikwepe hoja ya msingi.
 
Back
Top Bottom