UKAWA turushe hoja tuache matukio

maganjwa

JF-Expert Member
Sep 11, 2012
2,800
2,337
Nawaomba wote wenye nia njema na nchi yetu na baadae yetu tuungane kudai tume huru ya uchaguzi.

Ukawa tuache matukio badala yake tusimamie hoja hiyo ili kuleta mabadiliko ya kweli. Kiukweli matukio yanatupotezea dira upinzani.

Kupambana na rais ni kutwanga maji kwenye kinu kwa kuwa vyombo vyote vya dola anamiliki yeye. kwa hiyo bila hoja tunapotezwa kirahisi sana
 
kweli mkuu unakaribia kufa watu hawapendi hoja wanavutiwa na matukio
 
  • Thanks
Reactions: nao
Wakati nchi inalia viwanda viwanda viwanda...

wapinzani wanalia Rambirambi rambirambi rambirambi

Hapo ndio utajua nani mwenye malengo ya muda mrefu
wameawaambukiza hadi wananchiwengine wasio na hatia ugonjwa wa malalamiko na matukio
 
Ukisikiliza bunge kidogo utajua nani mwenye hoja kati ya wapinzani na CCM.
Ukiweka ulingo sawa wa kisiasa utajia nani mwenye hoja kati ya CCM na wapinzani.

Hujo hupingwa kwa hoja. Kama matukio ndio gia ya wapinzani basi wamefaulu kwa % kubwa sana kwani CCM kupitia viongozi wake wanalazimishwa kuvitangaza vyama vya upinzania kupitia matukio hayo hayo.
Kwa mfano tukio la Arusha au kule Kagera palikua na shida gani kama viongozi wa serikali wangewashirikisha viongozi wa miji na majiji hao yaani mameya.?

Kwa sasa Huu sio ule uungwaji mkono wa CCM wa kuanzia Novemba mpaka July 2016.

Watu wana mambo Mengi ya kusema lakini hawana pa kusemea ,watu wanalalamika na kupoteza matumaini .
CCM hii ni ya maneno matupu huku ikizuia wengine kusema. Imekosa mvuto kwa jamii.
Kuna mtu mmoja aliifananisha CCM na mwindaji mwenye risasi ya mwisho kwenye Gobore.Akiitumia vibaya anakua amejimaliza.
 
Tatizo ni kuwa inaporudiwa rudiwa jambo baya watu wataona sio baya ndo la msingi hakika nchi iko hoi
 
UKAWA wamefurah sana vifo vya wale watoto ....mana ndo kiki ya msimu...kweli UKAWA imelaaniwa
 
Hoja hutokana na matukio...je hoja hutokea hewani?Kupambana na utawala mbaya sio kupambana na raisi
Makosa ni kumkumbatia Mange kimambi kama mpambanaji wao,hakika wanapoteza dira.
 
Hoja hutokana na matukio...je hoja hutokea hewani?Kupambana na utawala mbaya sio kupambana na raisi
Makosa ni kumkumbatia Mange kimambi kama mpambanaji wao,hakika wanapoteza dira.
vita ni vita mange kimambi anapigana kivyake lakini kama vita vyake ni vya maana anaungwa mkono maadam ni mzalendo
 
UKAWA wamefurah sana vifo vya wale watoto ....mana ndo kiki ya msimu...kweli UKAWA imelaaniwa


ccm ndo waliofurahi soma hapa chini

Bollen Ngeti kada mtiifu wa ccm anaandika kuhusu Rambirambi Arusha

WANA CCM wenzangu, hiki tunachokifanya hakina baraka za Allah/Mungu/Yehova/ Nyasaye kabisa. Hebu tulitafakari maana sidhani kama ni ubinadamu. Huu ni utapeli ndugu zangu tusiunge mkono hata kama nia ni njema kiasi gani.

Nazungumzia huu utamaduni mpya wa kukusanya pesa za rambi-rambi na kuyapangia matumizi mengine. Hii ni dhahiri Serikali yetu inafurahia majanga na mabalaa kutokea ili kupata pesa. Kwamba majanga ni dili (biashara). Hii ni aibu kubwa. Tunaona wivu wa mini na hela za rambi-rambi? Huu si utu!

Nimekutana na mzazi aliyepoteza mwanaye Arusha anaumia sana kusikia eti kifo cha mwanaye imekuwa ni chanzo cha mapato ya Serikali kukarabati Hospitali ya Mount Meru. Amelia sana mbele yangu kwenye simu.

Nashauri ingependeza basi baada ya kukusanya rambi-rambi yote hata kama ni Mabilioni Ndg Mrisho Gambo angewaita wafiwa wote pamoja na kuuza wazo hilo kwao then kuwasikiliza maoni yao. Pengine wangesema kiasi Fulani mtupe na salio ikaboreshe hospitali au kununua vitabu kwa shule zote za Arusha. Wafiwa si wajinga wangetoa mawazo mazuri. Huo ndio uongozi shirikishi na si kuwapangia matumizi pesa zao. Ndio maana nimetoa wito kwa wanasheria kuwasaidia wafiwa hawa kudai pesa hizi ni zao. Mkoa haukufiwa, Gambo hakufiwa. Wapo wazazi in person waliofiwa ndio wanaochangiwa. Daini hela hizi ili iwe fundisho kwa majanga yajayo (hatuombei).

Tukiruhusu utamaduni huu mpya wa kutumia rambi-rambi siku atatokea Mkurugenzi mwendawazimu akishatafuna hela za umma na hana namna ya kulipa ni kuhujumu njia ya reli iache njia watu wafee kadhaa au achome shule maana rambi-rambi itakusanywa naye kuzipangia matumizi alikoiba. Tusishabikie hili la rafiki yangu Gambo. Si Jema!

NASISITIZA: Wanasheria wasaidieni wafiwa kudai hela hizi maana ni zao. Ni kwa ajili ya watoto wao. Watatumia kupalilia makaburi ya wanao. Niko tayari kulipia gharama za mawakili ili tabia hii ikome Tanzania. Misiba ya watu isiwe harusi ya Serikali.
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]. Bollen Ngeti. UVCCM Taifa
 
Wakati nchi inalia viwanda viwanda viwanda...

wapinzani wanalia Rambirambi rambirambi rambirambi

Hapo ndio utajua nani mwenye malengo ya muda mrefu
wameawaambukiza hadi wananchiwengine wasio na hatia ugonjwa wa malalamiko na matukio
Bora tulilie ata rambirambi maaan hoja ya viwanda ni viwonder tu... Kwanza serikali yenyew nayo inaenda kwa matukio na mizuka tu....kwaio usidhani una akili kuliko wapinzani kama akina mbowe na wengine ambao ni wapinzni miaka nenda rudi they use brain
 
Haha huwezi kusema watu hawana hoja wakati ulingo haupo sawa... Kama unataka hoja weka ulingo sawa sio kuziba wengine pakusemea ww ndio useme .
 
Upinzani wa kweli ulishajifia siku nyingi toka 2015 hukooo zimebakia porojo tu.

Mungu atuweke hai tu labda wajukuu zetu watajabadilisha huuu upinzani uliopo uwe na maana wa sasa ni upinzani matusi na matukio basi akili ya kujiongeza hakuna ukiwaambiaa eti mikutano imepigwa marufuku ndo jibu.
 
Back
Top Bottom