UKAWA ni wazembe wa kutupwa

UKAWA ni wazembe wa kutupwa

Hapa siwazungumzia wana UKAWA ambao ni watu wa kawaida mitaani wasio na nyadhifa kwenye vyama vinavyounda UKAWA. Hapa nawalenga viongozi wa vyama hivyo kuanzia wenyeviti wao hadi maofisa wa Makao Makuu kwenye vyama hivyo.

Kuna suala linaendelea la kuwa na Rais bila ya kuwa na Baraza la Mawaziri, hivi msimamo wa UKAWA ni nini hasa. Wao wanaona kuwa ni sawa au si sawa? Kwa maana nyingine kama wao ndiyo wangekuwa wamepewa serikali mpaka leo wangekuwa pia hawajatangaza baraza lao la mawaziri?

Hili jambo la Bandari UKAWA wana taarifa gani kuhusu sakata zima? Kwa maana watu wafahamu kuwa Bandari ya Dar es salaam ina uwezo wa kutunza kwa wakati mmoja Makontena zaid ya milioni 4. kwa maana nyingine hayo zaidi ya 2000 yanayotajwa na Waziri Mkuu Majaliwa ni tone tu katika makontena yanayopitia Dar es salaam. Maana yangu ni kwamba inawezekana kuna watu wameachwa kutokana na maslahi ya kisiasa waliyonayo Waziri Mkuu na wenzake ndani ya CCM.

Ada elekezi kwa shule binafsi UKAWA wao msimamo wao ni upi? Maana wenye shule zao wameahidi kutozifungua msimu wa kufungua ukifika. Je UKAWA wanandhani hatua za Serikali ni sahihi au si sahihi na wao msimamo wao ni upi? Wanaona hiyo njia wanayotumia Serikali ndiyo itakuwa inajenga uwezo wa shule za Umma na kuboresha elimu au ndiyo Elimu inashushwa kiwango chake?

Halafu kuna hili la CCM kufanyia vikao vyake kwenye ofisi kuu ya Umma Tanzania, Ikulu. Kama sheria inazuia siasa kwenye majengo ya umma kama mashule na kadhalika inakuwaje chama cha siasa kitumie Ikulu ambayo ni ofisi kuu ya Umma kufanyia vikao vyake? Je UKAWA na wao wangeshika madaraka wangetumia Ikulu kufanyia vikao vyao vya kisiasa.

UKAWA ni wazembe sana, kila inapotokea nafasi ya kujijenga kisiasa wao huwa wako Bize na harakati zisizo na mashiko!

Wewe mtoa mada unechanganyikiwa! Unajua kabisa kuna baadhi ya mambo yanayofanywa na Magufuli ambayo watanzania waliyapigia kelele siku nyingi, unataka tuendeshe nchi kwa visasi na chuki sio? Badala ya kusema watanzania tuungane kuliokoa taifa letu hili lakini wewe unaleta porojo tu humu. Kuna mambo ambayo UKAWA watayazungumzia kwa kutoridhishwa nayo lakini si kwa chuki na ghilba kama unavyotaka wewe.
 
MAHANJU chuki na ghiliba ndiyo nini? Panua kidogo ubongo wako. Kwa mfano wote tunataka Taifa Stars ishinde lakini je ni wote tunaamini ili Stars ishinde tuajiri makocha toka nje? Au wewe ukiambiwa uchague wachezaji wa timu hiyo utachagua wale wale wote waliochaguliwa na Kocha Charles Mkwasa? Ukitaka mawazo ya watu wa UKAWA katika kuendesha nchi yafanane kwa kila nukta na yale mawazo ya watu wa CCM basi hakuna haja ya kuwa na vyama vingi vya siasa.
 
Ibilisi wewe unaona ni sawa kwa muda wote huu nchi ina watu wawili tu wanaozunguka huku na huko. Huo ndiyo utawala bora? MTAZAMO mimi huwa nachukia kuona eti vitu au watu ambao wanatakiwa kuwajibika kwa umma wanakuwa hawagusiki (Untouchable) kwa hofu tu ya baadhi ya watu wanaodhani kwamba watu hao wakisemwa makosa yao taasisi wanayoingoza itasambaratika.

Hata hoja yangu dhidi ya CCM ni kukataa kwangu kwamba bila ya CCM hakuna Tanzania. Hawa UKAWA wao kila siku kisingizio chao eti wanafanya "Utafiti" sasa kama kila kitu ni utafiti wao wanajua nini hasa kuhusu nchi hii? Yaani ni kama wanasubiri kila siku washambuliwe kazi yao ni kujibu.

Mambo haya ya kukaa kimya bila sababu ndiyo yamewafikisha hapo walipo wamebung'aa. Wakati wa Kampni walikuwa wanaulizwa kwa nini wameamua kupmoke Lowassa wakati walikuw wanasema ni Fisadi mpaka kampeni zinaisha hakuna jibu la maana walilolitoa. Mbowe kauza cha kwa mabilioni ya shilingi wao kimya. UKAWA ni muungano wa ukanda, wao Kimya.

Hata kule sehemu ambako UKAWA walisimamisha wagombea wawili wawili viongozi wakawa kimya, matokeo yake tumepoteza kata nyingi na majimbo ya kutosha kutokana na ukimya wa Viongozi wa UKAWA. labda leo Julius Mtatiro angekuwemo Bungeni akitoa mchango wake kwa ujenzi wa taifa. Mwanasiasa ni lazima uonekane kwenye kila jambo linaloihusu jamii yako wewe umesimamia wapi!!

Thanks brother, na wewe utaitwa msaliti very soon. Tutajenga upinzani wa kweli kwa kuwaambia ukweli viongozi wa vyama vyetu .....CCM imefika hapa kwasababu ya kuogopana ....sasa inawagharimu kweli kweli .....
 
Nalaani vikali magufuli kugeuza ikulu ni kijiwe cha kupigia majungu. Nyerere mwenyewe hajawahi fanya upuuzi kama huo. Hivi magufuli ni nani hasa, hadi afanye ikulu pango la kukutania wanyang'anyi?

Magufuli ni Rais wa Tanzania. Waliotumbuliwa majipu watajitetea wenyewe. Ikulu ni ofisi na kama kuna taarifa zozote zinafikishwa huko. Wakati wa Nyerere ulisikia wizi kama uliopo sasa? Acheni kuweweseka.
 
Kama hujui haya yote mazuri yanayofanywa na Magufuli yanatokana na kazi nzuri ya UKAWA,dosari zinazojitokeza UKAWA wanaziona,kwa kuwa si wa kukurupuka watatoa jibu sahihi nini ambacho Magufuli ana takiwa akifanye ili mambo yaendelee kwenda vizuri.

Muda upi muda ndio huu nchi inaenda na maamuzi yanafanywa na kutekelezwa 🙂 au wanatafuta watatokaje
 
Na yeye ni sawa na wenzie Ukawa, maswali meengi kumbe hamna kitu.
Soma kimakinifu utayaona majibu. kama nasema kula magimbi ni kosa basi jua kutokula ndiyo sahihi. Fikirisha kidogo ubongo wako!
 
chadema wanaumiza kichwa waje na ajenda gani ya kuushika umma baada ya ile ya ufisadi kudhihirika kuwa walikuwa wanafanya SIASA ZA UNAFIKI.
 
TEKNOLOJIA nashukuru kwa kunielewa! Unga mkono hoja kwa mantiki na pinga kwa mantiki!!
 
Last edited by a moderator:
Hapa siwazungumzia wana UKAWA ambao ni watu wa kawaida mitaani wasio na nyadhifa kwenye vyama vinavyounda UKAWA. Hapa nawalenga viongozi wa vyama hivyo kuanzia wenyeviti wao hadi maofisa wa Makao Makuu kwenye vyama hivyo.

Kuna suala linaendelea la kuwa na Rais bila ya kuwa na Baraza la Mawaziri, hivi msimamo wa UKAWA ni nini hasa. Wao wanaona kuwa ni sawa au si sawa? Kwa maana nyingine kama wao ndiyo wangekuwa wamepewa serikali mpaka leo wangekuwa pia hawajatangaza baraza lao la mawaziri?

Hili jambo la Bandari UKAWA wana taarifa gani kuhusu sakata zima? Kwa maana watu wafahamu kuwa Bandari ya Dar es salaam ina uwezo wa kutunza kwa wakati mmoja Makontena zaid ya milioni 4. kwa maana nyingine hayo zaidi ya 2000 yanayotajwa na Waziri Mkuu Majaliwa ni tone tu katika makontena yanayopitia Dar es salaam. Maana yangu ni kwamba inawezekana kuna watu wameachwa kutokana na maslahi ya kisiasa waliyonayo Waziri Mkuu na wenzake ndani ya CCM.

Ada elekezi kwa shule binafsi UKAWA wao msimamo wao ni upi? Maana wenye shule zao wameahidi kutozifungua msimu wa kufungua ukifika. Je UKAWA wanandhani hatua za Serikali ni sahihi au si sahihi na wao msimamo wao ni upi? Wanaona hiyo njia wanayotumia Serikali ndiyo itakuwa inajenga uwezo wa shule za Umma na kuboresha elimu au ndiyo Elimu inashushwa kiwango chake?

Halafu kuna hili la CCM kufanyia vikao vyake kwenye ofisi kuu ya Umma Tanzania, Ikulu. Kama sheria inazuia siasa kwenye majengo ya umma kama mashule na kadhalika inakuwaje chama cha siasa kitumie Ikulu ambayo ni ofisi kuu ya Umma kufanyia vikao vyake? Je UKAWA na wao wangeshika madaraka wangetumia Ikulu kufanyia vikao vyao vya kisiasa.

UKAWA ni wazembe sana, kila inapotokea nafasi ya kujijenga kisiasa wao huwa wako Bize na harakati zisizo na mashiko!

Unawaonea bure UKAWA, daflau walilopigwa ni kubwa mno gia za angani nouma sana. Waache kwanza wakizinduka na akili kukaa sawa watakumbuka wajibu wao. CCM wataendelea kushtua kijoti na kucheza viduku mpaka miaka yao iishe lakini kumbuka pia JK alijenga ukumbi wa mikutano ombeni na mkiwa na adabu JPM ananouma atawaruhusu na UKAWA tatizo hakuna juice wala chai.
 
Kama hujui haya yote mazuri yanayofanywa na Magufuli yanatokana na kazi nzuri ya UKAWA,dosari zinazojitokeza UKAWA wanaziona,kwa kuwa si wa kukurupuka watatoa jibu sahihi nini ambacho Magufuli ana takiwa akifanye ili mambo yaendelee kwenda vizuri.

Kwakupenda mteremko nyie, JPM alikuwa mpaka anaapia akiamungu na kapiga push up ili apate hii kazi, nyie wote mlikuwa upande wa mabwana zenu anatimiza ahadi zake mnasema kazi nzuri ya Ukawa? anaenda kuutubia bunge mnazomea nyie watu kweli! Mlikuwa mnashika funguo ktk kampeni nyie na kuzungusha mikono. Aliwaambia Magufuli 4 change mlitaka kwenda mahakamani au mmesahau sasa mwacheni apige kazi kwanza na anavyoonekana shobo apendi atawazingua.
 
Upinzani hasa UKAWA tz unakosa "think tankers" kiasi flani Slaa alikuwa anafikiri kidogo.
 
Unataka ukawa wafanye nini ?

Kwa hiyo UKAWA waende waseme au wawatetee uozo uliofanyika ? Wakifanya hivyo basi , wao ni ndio wapinzani.

Mtu hajaingia katika ndoa unapinga ndoa yake , unataka wapinge kutokea wapi. Waanze kufanya maandamo?

Maandamano yalishakatazwa na polisi.

Ungetoa your side of story na ukaonyesha uzembe wao ni upi?

Of course kuna maeneo mengi ambayo, ikibidi yatapingwa na upinzani kwa hoja za msingi.

Mfano je katika eneo la bandari , je majipu yametumbuliwa kwa haki au kuna mengine yameachwa .

Kuwalaumu upinzani, ni sawa sawa fire department , wanaenda kuzima moto au unauliza wapinzani wako wapi.

Kuzima moto ni kazi ya fire men. Kwa sasa JPM kuzima moto ni kazi yake anuai.
 
Hapa siwazungumzia wana UKAWA ambao ni watu wa kawaida mitaani wasio na nyadhifa kwenye vyama vinavyounda UKAWA. Hapa nawalenga viongozi wa vyama hivyo kuanzia wenyeviti wao hadi maofisa wa Makao Makuu kwenye vyama hivyo.

Kuna suala linaendelea la kuwa na Rais bila ya kuwa na Baraza la Mawaziri, hivi msimamo wa UKAWA ni nini hasa. Wao wanaona kuwa ni sawa au si sawa? Kwa maana nyingine kama wao ndiyo wangekuwa wamepewa serikali mpaka leo wangekuwa pia hawajatangaza baraza lao la mawaziri?

Hili jambo la Bandari UKAWA wana taarifa gani kuhusu sakata zima? Kwa maana watu wafahamu kuwa Bandari ya Dar es salaam ina uwezo wa kutunza kwa wakati mmoja Makontena zaid ya milioni 4. kwa maana nyingine hayo zaidi ya 2000 yanayotajwa na Waziri Mkuu Majaliwa ni tone tu katika makontena yanayopitia Dar es salaam. Maana yangu ni kwamba inawezekana kuna watu wameachwa kutokana na maslahi ya kisiasa waliyonayo Waziri Mkuu na wenzake ndani ya CCM.

Ada elekezi kwa shule binafsi UKAWA wao msimamo wao ni upi? Maana wenye shule zao wameahidi kutozifungua msimu wa kufungua ukifika. Je UKAWA wanandhani hatua za Serikali ni sahihi au si sahihi na wao msimamo wao ni upi? Wanaona hiyo njia wanayotumia Serikali ndiyo itakuwa inajenga uwezo wa shule za Umma na kuboresha elimu au ndiyo Elimu inashushwa kiwango chake?

Halafu kuna hili la CCM kufanyia vikao vyake kwenye ofisi kuu ya Umma Tanzania, Ikulu. Kama sheria inazuia siasa kwenye majengo ya umma kama mashule na kadhalika inakuwaje chama cha siasa kitumie Ikulu ambayo ni ofisi kuu ya Umma kufanyia vikao vyake? Je UKAWA na wao wangeshika madaraka wangetumia Ikulu kufanyia vikao vyao vya kisiasa.

UKAWA ni wazembe sana, kila inapotokea nafasi ya kujijenga kisiasa wao huwa wako Bize na harakati zisizo na mashiko!

Swala la baraza la mawaziri ni uamuzi wa Rais. katiba yetu haimlazimishi kuteua baraza la mawaziri; inamlazimisha kuteua waziri mkuu tu. Ndiyo maana ukiwa na rais janga basi anaweza kuunda baraza la mawaziri 60 na ukiwa na rais makini anaweza kuwa na mawaziri watatu tu na nchi ikaendelea. Kinachotakiwa ni kuwepo mawaziri kadhaa wakati wa vikao vya bunge, kwa hiyo wakati huu ambapo hamna vikao vya bunge, rais anaweza kuendesha nchi bila waziri hata mmoja bali waziri mkuu na wakuu wa mikoa tu.
 
Nalaani vikali magufuli kugeuza ikulu ni kijiwe cha kupigia majungu. Nyerere mwenyewe hajawahi fanya upuuzi kama huo. Hivi magufuli ni nani hasa, hadi afanye ikulu pango la kukutania wanyang'anyi?
Hahahaah,Tupoze mizuka yetu tusikurupuke!Nadhani hapo Rais wa JMT amekutana na chama kimojawapo ya vyama vilivyopo TZ,hakatazwi kufanya hivyo.Ndio kusema hata CDM wakitaka kumfata Ikulu ni rukhsa!!..
 
Kwa hiyo ccm wameenda ikulu kunywa juice?
 
Kama kweli leo UKAWA wameshindwa kwenye uchaguzi wa Meya Tanga na wao wako Madiwani 20 dhidi ya 17 wa CCM bado narudia watu wa UKAWA ni wazembe sana. Kwani wao walidhani CCM hawatawashawishi hao madiwani wawili walioongeza kura kwao. Yaani hawa jamaa ni wazembe sana kazi yao ni kusubiri kulalamika!!
 
Mkuu naunga mkono hoja,kweli UKAWA ni Wazembe kweli,
 
Back
Top Bottom