UKAWA ni wazembe wa kutupwa

UKAWA ni wazembe wa kutupwa

Teh teh teh..UKAWA ni CHADEMA na CHADEMA ni Mbowe...lazima asome upepo asije nae akashikwa pabaya!
...Mbowe kichwa!
 
Mtoa mada , nakupa pole na kukushangaa sana, niliposoma uzi wako nikawaza mengi sana, kwanza nilifikili ni miongoni mwa waliotumbuliwa jibu na maumivu ni makali ,sasa unaomba angalau mawaziri wawepo ili waendelee na uzembe wao wa siku zote na majipu ya situmbuliwe. Pili nikaona unayohoja ya msingi isipo kuwa umekosea kwa kuielekeza, kuwatupia lawama UKAWA juu ya hili sio shihi kabisa. UKAWA haipo kumsaidia magufuli kufanya kazi yake vizuri, bali ipo kwaajili ya kukosoa utendaji wake na kueleza kwa wananchi namna sahihi ya utendaji. Uwezi jua katika hilo wameona nini na watakuja na jambo gani.

Unapo amua kukosoa utendaji wa mtu lazima ufanye utafiti kwanza
 
Mleta mada anasema eti bandari ya Dar es salaam ina uwezo wa kuhifadhi makontena million 4 na huo upotevu wa makontena elfu 2 ni tone tu.

Swali: je uwezo huo wa bandari katika uhifadhi wa makontena mil. 4 ni wa muda gani? Maana sidhani kama ni wa wakati mmoja ( at once), je na hayo makontena yaliyopotea yamepotea kwa kipindi gani?

Jibu maswali hapo juu kwanza kabla hatujathibisha kwamba umekurupuka kwenye suala la makontena.

Ishu ya cabinet:
Katiba yetu ya mwaka '77 tunayotumia sasa iko kimya kuhusu muda sahihi hasa wa Rais anatakiwa awe ameunda baraza lake la mawaziri ila inazungumza kuhusu kuteuliwa kwa PM tangu Rais aapishwe.
Kwahiyo Magufuli yupo sahihi na ukawa wakipiga kelele kuhusu hili basi wazi watajidhihirisha wazi walivyo mbumbumbu kuhusiana na katiba.

Hayo mengine ya:-
1: ada elekezi
2: kufanyia vikao vya chama kwenye public building na mengineyo mengi....!!!!!!
"Yanajibika"
 
Mkuu hili unalijua leo? unatakiwa ukapimwe akili kama alivyowahi kushauri mchungaji Msigwa! UKAWA hawajali maslahi mapana ya wananchi....LENGO la UKAWA ni Kutwaa MADARAKA hata kama Kiongozi wao ni JIWE ....

Wewe umerukia kama wale watoto wa kike JK aliosema wanapata mimba kwa viherehere vyao. Kwanza napenda nimjulishe mtoa mada kwamba, hilo la upinzani kupigia kelele vikao vya chama kufanyikia ikulu sio geni. Na kwa hali ilivyo kwa Tanzania na nchi nyingi za kiafrika unapokuwa madarakani unaamua sheria gani utii na zipi usitiii. Kwa maneno marahisi chama chako kinapokuwa madarakani unakuwa juu ya sheria. Hilo la makontena kwa mazingira yalivyo hata wapinzani wakienda kutaka taarifa za kina sio rahisi kupewa maana wataambiwa wanataka kuleta siasa waache serekali ifanye kazi. Kumbuka hicho kinachoendelea hapo bandarini ni uozo wa muda mrefu na wapinzani wameshapigia kelele sana na mapendekezo wakatoa bungeni, ila utashi wa kutekeleza ndio ulikosekana. Hilo la ada elekezi ni yaleyale itaonekana wakipigia kelele au kutoa pendekezo siku hizi kuna kichaka cha kujifichia kwamba wanapenda siasa za matukio. Kuhusu baraza la mawaziri, katiba iko kimya kuhusu eneo hili. Hivyo utashi wa kiongozi husika ndio utaamua.

CC: Allen Kilewella
 
born again pagan na tindo mimi sijasema kwamba wapinzani wapige kelele!! Wao wanafanya nini kama kazi yao siyo kuchambua jinsi serikali iliyoko madarakani inavyofanya kazi? Kuhusu uwezo wa Bandari kuhifadhi makontena mangapi kwa wakati mmoja hilo si u-google tu!
 
Last edited by a moderator:
Wewe umerukia kama wale watoto wa kike JK aliosema wanapata mimba kwa viherehere vyao. Kwanza napenda nimjulishe mtoa mada kwamba, hilo la upinzani kupigia kelele vikao vya chama kufanyikia ikulu sio geni. Na kwa hali ilivyo kwa Tanzania na nchi nyingi za kiafrika unapokuwa madarakani unaamua sheria gani utii na zipi usitiii. Kwa maneno marahisi chama chako kinapokuwa madarakani unakuwa juu ya sheria. Hilo la makontena kwa mazingira yalivyo hata wapinzani wakienda kutaka taarifa za kina sio rahisi kupewa maana wataambiwa wanataka kuleta siasa waache serekali ifanye kazi. Kumbuka hicho kinachoendelea hapo bandarini ni uozo wa muda mrefu na wapinzani wameshapigia kelele sana na mapendekezo wakatoa bungeni, ila utashi wa kutekeleza ndio ulikosekana. Hilo la ada elekezi ni yaleyale itaonekana wakipigia kelele au kutoa pendekezo siku hizi kuna kichaka cha kujifichia kwamba wanapenda siasa za matukio. Kuhusu baraza la mawaziri, katiba iko kimya kuhusu eneo hili. Hivyo utashi wa kiongozi husika ndio utaamua.

CC: Allen Kilewella

Umelijibu vizuri hili nyumbu, Muda wote nyumbu yeye siasa tuu waache ukawa wapumue
 
Allen Kilewella nilikwambia hatuna wapinzani na viongozi wa upinzani hawasimamii misingi wanayohubiri ukabisha ....nikakwambia utakuja kuanza kulalamika pale utapoanza kuona hata viongozi wanaishia kutoa hoja nyepesi badala ya Sera mbadala ....sasa umeanza kidogo kuona ....alafu hakuna tena UKAWA ...CUF na Chadema ndio waliobakia na kama unajua itikadi za vyama hivi utaelewa kilichobakia kuwaweka pamoja ni uchaguzi wa Zanzibar then utashuhudia rangi halisi za wapinzani hawa wa kizazi chetu ...
 
Last edited by a moderator:
mleta mada kubali kuwa umekurupuka ,tena umetumia maneno makali sana kwenye heading yako, hapo hoja hamna, na ntawashangaa sana UKAWA wakikurupuka kulaumu kuundwa kwa baraza la mawaziri, hayo ni mawazo yako, wengi wanasemaje juu ya ukimya wa magufuli kuunda baraza ?
 
Mada imejaa chembe za ubaguzi wa kipinzani kwa nini isiwe upinzani na wala si UKAWA kuwashauri wafanye uliyowashauri. Kumbuka kuna ACT-Wazalendo, TLP, UDP na wengine hawako kwenye ukawa. Kama UKAWA wataendelea na mtindo wao wa kuangalia zaidi mapungufu kama mtaji wao wa kisiasa watashindwa kujijenga kama mleta mada anavyofikiri. Tunataka kuona upinzani wa dhati unaojikita katika hoja na kujitolea. Mfano, walitakiwa kuwahamasisha wanachama wake kushiriki kikamilifu katika zoezi la usafi ikiwa pamoja na kutumia vipato vya vyama vyao kusaidia jamii katika mataizo yake.
 
Mimi naona hakuna haja wafanye mini wakati Sera na ilani ya uchaguzi inatekekelezwa na rais na mgombea toka ccm nyie vipi mnataka Ukawa wapige kelele IPI tena?
 
kasome katiba ndugu, baraza la mawaziri atalitengeneza kwa muda anaotakaa.

Mbona JK alichelewesha kulivunjaa hukusemaa hayaa
 
Ibilisi wewe unaona ni sawa kwa muda wote huu nchi ina watu wawili tu wanaozunguka huku na huko. Huo ndiyo utawala bora? MTAZAMO mimi huwa nachukia kuona eti vitu au watu ambao wanatakiwa kuwajibika kwa umma wanakuwa hawagusiki (Untouchable) kwa hofu tu ya baadhi ya watu wanaodhani kwamba watu hao wakisemwa makosa yao taasisi wanayoingoza itasambaratika.

Hata hoja yangu dhidi ya CCM ni kukataa kwangu kwamba bila ya CCM hakuna Tanzania. Hawa UKAWA wao kila siku kisingizio chao eti wanafanya "Utafiti" sasa kama kila kitu ni utafiti wao wanajua nini hasa kuhusu nchi hii? Yaani ni kama wanasubiri kila siku washambuliwe kazi yao ni kujibu.

Mambo haya ya kukaa kimya bila sababu ndiyo yamewafikisha hapo walipo wamebung'aa. Wakati wa Kampni walikuwa wanaulizwa kwa nini wameamua kupmoke Lowassa wakati walikuw wanasema ni Fisadi mpaka kampeni zinaisha hakuna jibu la maana walilolitoa. Mbowe kauza cha kwa mabilioni ya shilingi wao kimya. UKAWA ni muungano wa ukanda, wao Kimya.

Hata kule sehemu ambako UKAWA walisimamisha wagombea wawili wawili viongozi wakawa kimya, matokeo yake tumepoteza kata nyingi na majimbo ya kutosha kutokana na ukimya wa Viongozi wa UKAWA. labda leo Julius Mtatiro angekuwemo Bungeni akitoa mchango wake kwa ujenzi wa taifa. Mwanasiasa ni lazima uonekane kwenye kila jambo linaloihusu jamii yako wewe umesimamia wapi!!
 
Mkuu UKAWA wamevurugwa kusema ukweli

Matokeo na kasi ya Magufuli imekua ni kama shambulio la ghafla kwao
Tuwape muda wajipange, so far hata wao wanapenda kuona nchi inakwenda vizuri pia
 
Huo ndio udhaifu mkubwa wa Mbowe, hazijui kabisa fursa za kisiasa za kukiwezesha chama kujiimarisha kisiasa.Walizipoteza fursa muhimu mbili wakati wa sakata la ESCROW na vibali vya sukari huku Mbowe akiridhika tu akiwa kama kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.Kuondoka kwa Dr Slaa kumeacha pengo kubwa sana ila Wana CHADEMA hawajui tu.Lakini pia kumtwaa Lowassa kumewafanya CHADEMA wawe bubu kuhusu masakata ya ufisadi.
 
Subira Ya Jambo Ndio Hekima, Wanasubiri Kuona Kama Mafisadi Wakubwa Watakamatwa Ndipo Watoke Taarifa Yao Ila Wasubiri Bungeni
 
Mtoa mada , nakupa pole na kukushangaa sana, niliposoma uzi wako nikawaza mengi sana, kwanza nilifikili ni miongoni mwa waliotumbuliwa jibu na maumivu ni makali ,sasa unaomba angalau mawaziri wawepo ili waendelee na uzembe wao wa siku zote na majipu ya situmbuliwe. Pili nikaona unayohoja ya msingi isipo kuwa umekosea kwa kuielekeza, kuwatupia lawama UKAWA juu ya hili sio shihi kabisa. UKAWA haipo kumsaidia magufuli kufanya kazi yake vizuri, bali ipo kwaajili ya kukosoa utendaji wake na kueleza kwa wananchi namna sahihi ya utendaji. Uwezi jua katika hilo wameona nini na watakuja na jambo gani.

Unapo amua kukosoa utendaji wa mtu lazima ufanye utafiti kwanza

Hujamwelewa mleta mada,hazungumzii kuhusu UKAWA kumsaidia Magufuli,anazungumzia iwapo CHADEMA wameridhishwa na viwango vya hatua anazochukua ktk kushughulikia ufisadi?Kwa mfano kule bandarini,CHADEMA wameridhika na namna Magufuli anavyoshughulikia ufisadi wa bandarini?kwa mfano tuhuma kwamba kuna makontena zaidi ya 2000 hayajulikani yalipo,UKAWA walipaswa kufukua zaidi na kuwasilisha majina ya watuhumiwa kwa Magufuli au kuwatangaza hadharani.Opposition patties supposed to go extra mile.
 
Back
Top Bottom