Hapo zamani nilikuwa na mawazo ya kuwa chama kikisusia uchaguzi kinawanyima wanachama haki ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa, unafanya mpinzani wako kupita bila kupingwa, na yeye anafurahi kuwa peke yake, wengine wakawa wanasema "ukisusa wenzako wala" au "hakuna kususia shamba nguruwe".
Lakini baada ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali awamu hii mawazo yamegeuka kabisa nimebadili msimamo, sioni haki wanayopata wapiga kura kama maoni yao kwenye sanduku la kura hayaheshimiwi. Leo naungana na wale wenye mawazo ya kususia sijui kama nitakuwa sahihi ama la, nitaeleza.
Ni ukweli usiopingika kuwa chaguzi za awamu hii ni kiini macho tu, tofauti na chaguzi za awamu zilizopita, ingawa kulikuwa na wizi lkn angalau walijua kula na kipofu. Wizi wa kura wa awamu hii ni wa wazi kabisa wa nguvu, si rais, jeshi la polisi, NEC, viongozi mbalimbali wanaoona aibu kuiba, kwa matamshi na vitendo.
Pamoja na hayo yote CCM wanachukulia advantage kuona vyama vya upinzani kama CHADEMA na CUF bado vinaendelea kushiriki kwa lengo la kuwasindikiza na kuuhadaa ulimwengu kuwa Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi, kumbe chama ni kimoja tu na vingine ni wasindikizaji.
Hebu tujiulize, niwaulize wabunge niwaulize madiwani unashiriki uchaguzi ili iweje wakati unajua kabisa hautatangazwa mshindi, na rais ameshawaelekeza wakurugenzi hataki kuona mpinzani akitangazwa mshindi.
Hapo zamani (Jecha effect) nilijua kuwa tunashiriki uchaguzi na NEC hii hii mbovu ili baadaye tuionyeshe dunia kuwa Tanzania hatuna demokrasia ya kweli lkn sioni matokeo chanya au labda dunia haijali kinachoendelea nchini, sasa kama mbinu hiyo haisaidii kwanini tuendelee kuitegemea.
Hoja yangu ni kuwa, kama hakutakuwa na tume huru, wanachama wa upinzani hasa vyama vikubwa vya CHADEMA na CUF wasusie chaguzi zote zinazofuata ukiwemo ule wa 2020. No pain no gain.
Ianzishwe kampeni kubwa mapema kuwaelimisha wananchi kwa slogan ya "HAKUNA TUME HURU HAKUNA UCHAGUZI", "NO FREE ELECTORAL COMMISSION NO ELECTION".
Kuingia kwenye uchaguzi na tume hii, ni kuwapotezea wananchi muda wao bure, chama kupoteza resources bure kwa vile hakuna Mbunge wala Diwani yeyote atakayetangazwa kashinda hata kama atapata kura zote 100%.
Nina hakika once mkiamua kususia serikali haitapuuza, tumeona NEC walivyolalamika turnout ndogo kwenye uchaguzi uliopita, najua mwanzo CCM watakuja na kejeli lkn mkibaki firm impact yake kijamii siyo ndogo, (rejea NASA ya Odinga).
Kwa tume hii ninawahakikishia kuwa uchaguzi wa 2020 si CHADEMA wala CUF watakaokuwa na Mbunge hata mmoja bungeni.
Kwenye utawala huu wa Magufuli na NEC hii na polisi hii na wakuu wa mikoa hawa wanaoshangilia ushindi hadharani bila woga na aibu, mshiriki uchaguzi hamtaingia bungeni msishiriki uchaguzi hamtaingia bungeni, ni kunyoa au kusuka.
Waacheni CCM waandae uchaguzi wao wateue wagombea wao wajitangaze washindi wao waingie bungeni wao peke yao, liwe bunge la CCM perse, waingie mikataba wao, watunge sheria wao, najua kwa muda mfupi hawatabaki salama.
Tuanze na uchaguzi mdogo wa jimbo la Liwale - Lindi UKAWA wajitoe wasiweke mgombea pesa zake zikajenge ofisi ya chama hapo hapo Liwale, wakiweka watueleze ni kwa sababu zipi.
cc: #mashinji
cc: #maalimuseif
cc: #prof abdallahsafari
cc: #edwardlowassa

==========
Mawazo huru ya mwanaJF Quinine==========
cc: #freemanmbowecc: #mashinji
cc: #maalimuseif
cc: #prof abdallahsafari
cc: #edwardlowassa