UKAWA na Operation "Hakuna tume huru hakuna uchaguzi".

UKAWA na Operation "Hakuna tume huru hakuna uchaguzi".

"Neno (Tume) yaani imetumwa, sasa kwanini useme iwe Huru"
Hebu tuacheni tusherehekee ushindi wetu acheni kutuzingua.
View attachment 870968
Mwita hebu testi huu mmea wa Kiabakari.
Ukiona hadi Nape, Bashe, Mwigulu na Makamba wamebana kutoa maoni juu ya matokeo ya uchaguzi, basi ujue kulikuwa hakuna uchaguzi.

Vv
 
Kuendelea kushiriki uchaguzi ambao unafahamu kabisa, hata ukishinda huwezi kutangazwa mshindi, ni kupoteza muda.

Vyama vya Upinzani vilifanya vizuri kushiriki ili kupata uthibitisho. Sasa hakuna haja tena na kuendelea kushiriki uchaguzi ambao unasimamiwa na kamati ya CCM.

Kwa sasa nguvu zielekezwe kwenye kupata Tume ya Uchaguzi. Kwa sasa kimsingi, hatuna Tume ya Chaguzi bali tuna kamati ya makada wa CCM ambao wanajiita ni Tume ya Uchaguzi. Ni kikundi cha kuwalaghai wananchi wa Tanzania na Jamii ya Kimataifa kuwa Tanzania huwa tunafanya uchaguzi.
Chadema wangejitoa kabla ya kuonekana hujuma zilizo wazi watu wangewalaumu sana, lkn sasa watu wanasema ni heri wajitoe kuliko kuendelea kuumiza wafuasi wao, ni timing nzuri.
 
Sidhani kama kususia uchaguzi ndio solution hapa kinachotakiwa Ni kuirewind ile mission ya mange kwa umoja uliotukuka kwa hapo tunaweza tukamshinda kichaa
 
Naunga mkono,
Ila siamini Hao tunao tegemea kuchukua hizo hatua kama wako teyali kama mtu anasahau wapiga kura wake na kuhama Chama kwa maslah binafsi hata shindwa kufanya anachojua ili hilo lisifanikiwe
 
Sidhani kama kususia uchaguzi ndio solution hapa kinachotakiwa Ni kuirewind ile mission ya mange kwa umoja uliotukuka kwa hapo tunaweza tukamshinda kichaa
Lakini ni hatua mojawapo kuelekea kwenye mikakati mingine.
 
Kujitoa tu haitoshi. Lazima hii vita tuielekeze kwa wanachama wa sisiem huko vijijini. Ianzishwe kampeni ya kuwatisha wasidhubutu kupiga kura kama polisi wanavyowatishia wanachama na wapenzi wa chadema.
Inabidi vianzishwe vikundi vya vijana vya kuwatia watu hofu ili tume na mawakala wajipigie kura peke yao. Wananchi tubaki wote nyumbani. Atakayeenda kupiga kura hata kama atalindwa na polisi, wakiondoka lazima akione cha mtema kuni.
 
Tuanze na tume huru katiba itafuata, wapinzani wakiendelea kuingia kwenye uchaguzi huu wa kiini macho wanainufaisha CCM kwa siasa za ndani na kimataifa.

Wabunge wa upinzani ni msaada mkubwa kwa maendeleo ni kama jicho la pili la serikali, hebu turudi kwenye Bunge la chama kimoja tuone kama CCM itasalimika.

Naunga mkono hoja. wapinzani waanze kuhuburi tume huru ya uchaguzi sasa na watoe mapendekezo. Pia wapige kauli mbiu kwamba bila tume huru wananchi wasusie kupiga kura ili kutoa uhalali wa kwamba wananchi hawaridhishwi na chaguzi zisizo huru. Kampeni hii ianzie mitandaoni, huko mitaani, kwenye viwanja vya michezo, masokoni nk. Kampeni hii nina hakika itapata uungwaji mkono mkubwa kwani watu wengi wamechoshwa na hali ya uongozi ilivyo.
 
Tume Huru ni Ngumu Sana, Labda wajilipe wenyewe
 
kwa sasa wahamasishe wafuasi wao wasiende kupiga kura chini ya tume hii. wasimamizi wote ni makada toka juu hadi chini.

Kujitoa tu haitoshi. Lazima hii vita tuielekeze kwa wanachama wa sisiem huko vijijini. Ianzishwe kampeni ya kuwatisha wasidhubutu kupiga kura kama polisi wanavyowatishia wanachama na wapenzi wa chadema.
Inabidi vianzishwe vikundi vya vijana vya kuwatia watu hofu ili tume na mawakala wajipigie kura peke yao. Wananchi tubaki wote nyumbani. Atakayeenda kupiga kura hata kama atalindwa na polisi, wakiondoka lazima akione cha mtema kuni.
 
Naunga mkono hoja. wapinzani waanze kuhuburi tume huru ya uchaguzi sasa na watoe mapendekezo. Pia wapige kauli mbiu kwamba bila tume huru wananchi wasusie kupiga kura ili kutoa uhalali wa kwamba wananchi hawaridhishwi na chaguzi zisizo huru. Kampeni hii ianzie mitandaoni, huko mitaani, kwenye viwanja vya michezo, masokoni nk. Kampeni hii nina hakika itapata uungwaji mkono mkubwa kwani watu wengi wamechoshwa na hali ya uongozi ilivyo.

Kujitoa tu haitoshi. Lazima hii vita tuielekeze kwa wanachama wa sisiem huko vijijini. Ianzishwe kampeni ya kuwatisha wasidhubutu kupiga kura kama polisi wanavyowatishia wanachama na wapenzi wa chadema.
Inabidi vianzishwe vikundi vya vijana vya kuwatia watu hofu ili tume na mawakala wajipigie kura peke yao. Wananchi tubaki wote nyumbani. Atakayeenda kupiga kura hata kama atalindwa na polisi, wakiondoka lazima akione cha mtema kuni.
 
Sasa jiwe si ndio atarawala hadi akufwe!!
Tunahitajika kufanya jambo la kihistoria.
 
Hapo zamani nilikuwa na mawazo ya kuwa chama kikisusia uchaguzi kinawanyima wanachama haki ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa, unafanya mpinzani wako kupita bila kupingwa, na yeye anafurahi kuwa peke yake, wengine wakawa wanasema "ukisusa wenzako wala" au "hakuna kususia shamba nguruwe".

Lakini baada ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali awamu hii mawazo yamegeuka kabisa nimebadili msimamo, sioni haki wanayopata wapiga kura kama maoni yao kwenye sanduku la kura hayaheshimiwi. Leo naungana na wale wenye mawazo ya kususia sijui kama nitakuwa sahihi ama la, nitaeleza.

Ni ukweli usiopingika kuwa chaguzi za awamu hii ni kiini macho tu, tofauti na chaguzi za awamu zilizopita, ingawa kulikuwa na wizi lkn angalau walijua kula na kipofu. Wizi wa kura wa awamu hii ni wa wazi kabisa wa nguvu, si rais, jeshi la polisi, NEC, viongozi mbalimbali wanaoona aibu kuiba, kwa matamshi na vitendo.

Pamoja na hayo yote CCM wanachukulia advantage kuona vyama vya upinzani kama CHADEMA na CUF bado vinaendelea kushiriki kwa lengo la kuwasindikiza na kuuhadaa ulimwengu kuwa Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi, kumbe chama ni kimoja tu na vingine ni wasindikizaji.

Hebu tujiulize, niwaulize wabunge niwaulize madiwani unashiriki uchaguzi ili iweje wakati unajua kabisa hautatangazwa mshindi, na rais ameshawaelekeza wakurugenzi hataki kuona mpinzani akitangazwa mshindi.

Hapo zamani (Jecha effect) nilijua kuwa tunashiriki uchaguzi na NEC hii hii mbovu ili baadaye tuionyeshe dunia kuwa Tanzania hatuna demokrasia ya kweli lkn sioni matokeo chanya au labda dunia haijali kinachoendelea nchini, sasa kama mbinu hiyo haisaidii kwanini tuendelee kuitegemea.

Hoja yangu ni kuwa, kama hakutakuwa na tume huru, wanachama wa upinzani hasa vyama vikubwa vya CHADEMA na CUF wasusie chaguzi zote zinazofuata ukiwemo ule wa 2020. No pain no gain.

Ianzishwe kampeni kubwa mapema kuwaelimisha wananchi kwa slogan ya "HAKUNA TUME HURU HAKUNA UCHAGUZI", "NO FREE ELECTORAL COMMISSION NO ELECTION".

Kuingia kwenye uchaguzi na tume hii, ni kuwapotezea wananchi muda wao bure, chama kupoteza resources bure kwa vile hakuna Mbunge wala Diwani yeyote atakayetangazwa kashinda hata kama atapata kura zote 100%.

Nina hakika once mkiamua kususia serikali haitapuuza, tumeona NEC walivyolalamika turnout ndogo kwenye uchaguzi uliopita, najua mwanzo CCM watakuja na kejeli lkn mkibaki firm impact yake kijamii siyo ndogo, (rejea NASA ya Odinga).

Kwa tume hii ninawahakikishia kuwa uchaguzi wa 2020 si CHADEMA wala CUF watakaokuwa na Mbunge hata mmoja bungeni.

Kwenye utawala huu wa Magufuli na NEC hii na polisi hii na wakuu wa mikoa hawa wanaoshangilia ushindi hadharani bila woga na aibu, mshiriki uchaguzi hamtaingia bungeni msishiriki uchaguzi hamtaingia bungeni, ni kunyoa au kusuka.

Waacheni CCM waandae uchaguzi wao wateue wagombea wao wajitangaze washindi wao waingie bungeni wao peke yao, liwe bunge la CCM perse, waingie mikataba wao, watunge sheria wao, najua kwa muda mfupi hawatabaki salama.

Tuanze na uchaguzi mdogo wa jimbo la Liwale - Lindi UKAWA wajitoe wasiweke mgombea pesa zake zikajenge ofisi ya chama hapo hapo Liwale, wakiweka watueleze ni kwa sababu zipi.

==========​
Mawazo huru ya mwanaJF Quinine
==========​
cc: #freemanmbowe
cc: #mashinji
cc: #maalimuseif
cc: #prof abdallahsafari
cc: #edwardlowassa
Mbona Le Professeri Lipumb* hujamtaja?
 
Jaman sisi police tunapewa order tu so msituchukie
Wewe si mbwa ambaye akiambiwa kamata, anakamata tu bila kujiuliza ni kwanini anakamata. Garang mbona hakutii order baada ya kuona kinachofanyika ni uonezi dhidi ya jamii yake?
 
niliona mahali watu wanasema upinzani hawasomi ushauri wa mtandaoni,so sadly hii topic yako itaishia kwenye makabati ya JF!
 
Ndugu zangu Tanzania ni yetu si ya Magufuli wala hilo kundi ndogo la ccm.Tukiamua hakuna wa kutuzuia.
Tumeshachezewa sana ndugu zangu enough is enough tusimameni kutetea utu wetu taifa letu na heshima yetu.
Ccm hawatatuheshimu mpaka waone utayari wetu wa kufa kwa ajili ya kutetea utu wetu.
Tujitoe kwa ajili ya KATIBA yenye usawa kwa raia wote mengine yatakuja.
 
Maalim Seif aliyaona mbali haya lakini wengi wetu tulishindwa kumuelewa. Nina hakika mkakati huu umekuja baada ya mazungumzo ya majuzi kati ya Maalim na uongozi wa Chadema. Kwa wakati ule Maalim alikuwa akijibu hoja kuwa si suala la.kushinda au kuwa serikalini (SUK) ni suala la principles na sheria kufatwa..

As things go, 2020 election, tume itaamua wabunge gani wa upinzani wapite na wale wote wenye msimamo na nguvu bungeni, to wit; Mbowe, Lissu, Heche, Mnyika, Kubenea, Sugu, Mdee, Mchungaji, Easter to name the few, hawataingia bungeni hata kampeni wafanye kwa Dreamliner!

Mind you, hii ilikuwa ni intro tu, ngoma yote imekuwa reserved for 2020 na iwe practised mpaka Zanzibar.

Tusidanganyane, uchaguzi Tanzania bila ya CDM na CUF (halali ya Maalim), hauwezi kutambulika kimataifa. Huwezi kumng'ang'ani mwanamke anayepigwa nje kwa sababu eti mkaka anayempiga atafaidi. Muwache na uone kama watadumu! CCM watachijana wenyewe kwenye kura zao za maoni na michujo. Walioshiriki katika wizi huu na wao watatendwa tu katika chaguzi zao za ndani. Hawawezi wote wakafaidika na uovu huu. We are to wait and see!
 
Naunga mkono hoja. wapinzani waanze kuhuburi tume huru ya uchaguzi sasa na watoe mapendekezo. Pia wapige kauli mbiu kwamba bila tume huru wananchi wasusie kupiga kura ili kutoa uhalali wa kwamba wananchi hawaridhishwi na chaguzi zisizo huru. Kampeni hii ianzie mitandaoni, huko mitaani, kwenye viwanja vya michezo, masokoni nk. Kampeni hii nina hakika itapata uungwaji mkono mkubwa kwani watu wengi wamechoshwa na hali ya uongozi ilivyo.
Ndio tumeanza mwambie ndugu yako kijijini bila tume huru kura yake haina thamani siku ya kupiga kura bora abaki nyumbani au aende shambani akalime.
 
Back
Top Bottom