UKAWA na Operation "Hakuna tume huru hakuna uchaguzi".

UKAWA na Operation "Hakuna tume huru hakuna uchaguzi".

Muwe mnafuatilia taarifa sahihi ,usisubiri kuletewa taarifa na wanasiasa wanaojitetea.

Mgombea wa chadema monduli amesema yeye mwenyewe kuwa aliapisha mawakala wake 100, lakini kesho yake hawakuonekana kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kuambiwa chama hakina hela za kuwalipa..

Mawakala kukosa hela ni kosa la nani?

Polisi walikuwa wanashangilia uchaguzi kuisha kwa amani bila damu kumwagika ,lakini viongozi wanageuza taarifa kuwa walikuwa wanashangilia ushindi wa ccm ili kuwapotosha wafuasi wao waendelee kuwaamini!!

Viongozi waseme ukweli kama hawana hela za kulipa mawakala wa majimbo mawili ,je watakuja kutoa wapi hela za kulipa mawakala nchi nzima??
 
Nafikiri nimeshakujibu, CHADEMA imeshajitoa rasmi hizo sababu hazina maana tena hata ukiambiwa hazitakusaidia.
 
Mkuu umeongea point sana, huo ndio ukweli pamoja na kuwa hata hiyo kampeni ikianzishwa haitasaidia sana kwa sababu sa hivi ni marufuku kufanya mkutano wa kisiasa nje ya jimbo lako, na kama wewe sio mbunge/diwani huruhusiwi kufanya mkutano sehemu yoyote ile ndani ya Jamuhuri, ukianza kuhamasisha kupitia mitandao utashitakiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mtandao, kiufupi sa hivi hakuna njia yoyote ya busara inayoweza kutumika zaidi ya ubabe ubabe.
Viongozi wetu wa dini baada ya waraka zao za kuikosoa serikali sa hivi sijui wamefanywa nini, hatuwasikii tena wakikosoa au kusifia, ni kama wamesusa kushauri chochote kile.
Kampeni ikianza kadri unavyoizuia ndivyo unavyoifanya isambae, uliona operation UKUTA ilivyosambaa.
 
Mawazo ya busara yaungwe mkono
Hapo zamani nilikuwa na mawazo ya kuwa chama kikisusia uchaguzi kinawanyima wanachama haki ya msingi ya kuchagua na kuchaguliwa, unafanya mpinzani wako kupita bila kupingwa, na yeye anafurahi kuwa peke yake, wengine wakawa wanasema "ukisusa wenzako wala" au "hakuna kususia shamba nguruwe".

Lakini baada ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali awamu hii mawazo yamegeuka kabisa nimebadili msimamo, sioni haki wanayopata wapiga kura kama maoni yao kwenye sanduku la kura hayaheshimiwi. Leo naungana na wale wenye mawazo ya kususia sijui kama nitakuwa sahihi ama la, nitaeleza.

Ni ukweli usiopingika kuwa chaguzi za awamu hii ni kiini macho tu, tofauti na chaguzi za awamu zilizopita, ingawa kulikuwa na wizi lkn angalau walijua kula na kipofu. Wizi wa kura wa awamu hii ni wa wazi kabisa wa nguvu, si rais, jeshi la polisi, NEC, viongozi mbalimbali wanaoona aibu kuiba, kwa matamshi na vitendo.

Pamoja na hayo yote CCM wanachukulia advantage kuona vyama vya upinzani kama CHADEMA na CUF bado vinaendelea kushiriki kwa lengo la kuwasindikiza na kuuhadaa ulimwengu kuwa Tanzania kuna demokrasia ya vyama vingi, kumbe chama ni kimoja tu na vingine ni wasindikizaji.

Hebu tujiulize, niwaulize wabunge niwaulize madiwani unashiriki uchaguzi ili iweje wakati unajua kabisa hautatangazwa mshindi, na rais ameshawaelekeza wakurugenzi hataki kuona mpinzani akitangazwa mshindi.

Hapo zamani (Jecha effect) nilijua kuwa tunashiriki uchaguzi na NEC hii hii mbovu ili baadaye tuionyeshe dunia kuwa Tanzania hatuna demokrasia ya kweli lkn sioni matokeo chanya au labda dunia haijali kinachoendelea nchini, sasa kama mbinu hiyo haisaidii kwanini tuendelee kuitegemea.

Hoja yangu ni kuwa, kama hakutakuwa na tume huru, wanachama wa upinzani hasa vyama vikubwa vya CHADEMA na CUF wasusie chaguzi zote zinazofuata ukiwemo ule wa 2020. No pain no gain.

Ianzishwe kampeni kubwa mapema kuwaelimisha wananchi kwa slogan ya "HAKUNA TUME HURU HAKUNA UCHAGUZI", "NO FREE ELECTORAL COMMISSION NO ELECTION".

Kuingia kwenye uchaguzi na tume hii, ni kuwapotezea wananchi muda wao bure, chama kupoteza resources bure kwa vile hakuna Mbunge wala Diwani yeyote atakayetangazwa kashinda hata kama atapata kura zote 100%.

Nina hakika once mkiamua kususia serikali haitapuuza, tumeona NEC walivyolalamika turnout ndogo kwenye uchaguzi uliopita, najua mwanzo CCM watakuja na kejeli lkn mkibaki firm impact yake kijamii siyo ndogo, (rejea NASA ya Odinga).

Kwa tume hii ninawahakikishia kuwa uchaguzi wa 2020 si CHADEMA wala CUF watakaokuwa na Mbunge hata mmoja bungeni.

Kwenye utawala huu wa Magufuli na NEC hii na polisi hii na wakuu wa mikoa hawa wanaoshangilia ushindi hadharani bila woga na aibu, mshiriki uchaguzi hamtaingia bungeni msishiriki uchaguzi hamtaingia bungeni, ni kunyoa au kusuka.

Waacheni CCM waandae uchaguzi wao wateue wagombea wao wajitangaze washindi wao waingie bungeni wao peke yao, liwe bunge la CCM perse, waingie mikataba wao, watunge sheria wao, najua kwa muda mfupi hawatabaki salama.

Tuanze na uchaguzi mdogo wa jimbo la Liwale - Lindi UKAWA wajitoe wasiweke mgombea pesa zake zikajenge ofisi ya chama hapo hapo Liwale, wakiweka watueleze ni kwa sababu zipi.

==========​
Mawazo huru ya mwanaJF Quinine
==========​
cc: #freemanmbowe
cc: #mashinji
cc: #maalimuseif
cc: #prof abdallahsafari
cc: #edwardlowassa
 
kwa sasa wahamasishe wafuasi wao wasiende kupiga kura chini ya tume hii. wasimamizi wote ni makada toka juu hadi chini.
Kitendo cha mkiti kutangaza kususia chaguzi ni kampeni tosha nina imani hadi sasa imesambaa sana hadi vijijini kesho inahitimishwa na magazeti.
 
Kitendo cha mkiti kutangaza kususia chaguzi ni kampeni tosha nina imani hadi sasa imesambaa sana hadi vijijini kesho inahitimishwa na magazeti.
Kweli tume huru ndiyo suluhisho, ila nataka niweke angalizo ni kuwa tayari kuna nunuanunua (wabunge,madiwani) je hii haitaweza mpaka hao wa tume huru? naona hatuaminiani kabisa kuwa maskini ni dhambi kubwa ndo maana Lowasa alisema hapendi umaskini na anauchukia sana. Naomba kuwakilisha.
 
Muwe mnafuatilia taarifa sahihi ,usisubiri kuletewa taarifa na wanasiasa wanaojitetea.

Mgombea wa chadema monduli amesema yeye mwenyewe kuwa aliapisha mawakala wake 100, lakini kesho yake hawakuonekana kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kuambiwa chama hakina hela za kuwalipa..

Mawakala kukosa hela ni kosa la nani?

Polisi walikuwa wanashangilia uchaguzi kuisha kwa amani bila damu kumwagika ,lakini viongozi wanageuza taarifa kuwa walikuwa wanashangilia ushindi wa ccm ili kuwapotosha wafuasi wao waendelee kuwaamini!!

Viongozi waseme ukweli kama hawana hela za kulipa mawakala wa majimbo mawili ,je watakuja kutoa wapi hela za kulipa mawakala nchi nzima??
Acha kulialia wewe
 
Ni uamuzi sahihi na wakati sahihi. Ni kupoteza pesa za walipa kodi. Hawa wote waliohama vyama na kupewa bakhshishi wajiandae na kupelekwa mahakamani kulipa gharama zote ili mchezo huu mchafu ufikie kikomo.
Tz nchi ya Chama Kimoja -CCM
Acha ulimwengu ujue
TUANZE SAFARI YA UKOMBOZI SASA
TUPIGE KELELE ULIMWENGU UJUE
 
Kuna wakati marehemu Mtikila alishawahi kusema hapa Tanzania hakuna uchaguzi huru mpaka iundwe tume huru ya uchaguzi tulimuona anaropoka lakini sasa tayari tumeona maana halisi ya Mch Mtikila, angalizo langu ni nunuanunua tuuuuuu!!!!
 
mi naona wamechelewa sana kususia chaguzi hizi ila so mbaya, ccm watamsogeza lipumba sasa ili aonekane nae ni mpinzani
 
Niliiangalia clip moja ikimuonesha aliyekuwa mgombea wa Chadema Jimbo la Ukonga akipambana na makarani wa Uchaguzi kuwataka wamrudishie simu mmoja wa mawakala. Zogo lile lilimalizwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Nilijiuliza sana kwa nini mawakala walikuwa wanna surrender simu zao sikupata majibu. Sasa naanza kuona mwanga, kuwa zile simu zingekuwa silaha muhimu sana wakati process ya uchaguzi ikiendelea. Chama Twawala Buana, khaaa!
 
"SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA" haka kamsemo naona kanaanza kueleweka
 
Wakibaki peke yao bungeni basi na bunge live mtarudishiwa!

Watatonywa waichachafye serikali kadri wawezavyo lakini hatimaye wapige kura za ndiyo!

Yaani usanii ambao hamjawahi kuuona!
 
Niliiangalia clip moja ikimuonesha aliyekuwa mgombea wa Chadema Jimbo la Ukonga akipambana na makarani wa Uchaguzi kuwataka wamrudishie simu mmoja wa mawakala. Zogo lile lilimalizwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.

Nilijiuliza sana kwa nini mawakala walikuwa wanna surrender simu zao sikupata majibu. Sasa naanza kuona mwanga, kuwa zile simu zingekuwa silaha muhimu sana wakati process ya uchaguzi ikiendelea. Chama Twawala Buana, khaaa!
wale ni uvccm. walikuwa pale kuhakikisha mgombea wa ccm anashinda na sio. chaguo la wana ukonga ild sio tume huru.
 
Kuendelea kushiriki uchaguzi ambao unafahamu kabisa, hata ukishinda huwezi kutangazwa mshindi, ni kupoteza muda.

Vyama vya Upinzani vilifanya vizuri kushiriki ili kupata uthibitisho. Sasa hakuna haja tena na kuendelea kushiriki uchaguzi ambao unasimamiwa na kamati ya CCM.

Kwa sasa nguvu zielekezwe kwenye kupata Tume ya Uchaguzi. Kwa sasa kimsingi, hatuna Tume ya Chaguzi bali tuna kamati ya makada wa CCM ambao wanajiita ni Tume ya Uchaguzi. Ni kikundi cha kuwalaghai wananchi wa Tanzania na Jamii ya Kimataifa kuwa Tanzania huwa tunafanya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom