UKAWA na kuonesha makutano yao live

UKAWA na kuonesha makutano yao live

wamisako

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Posts
917
Reaction score
872
Nachukia sana palee ninapokua naona chama kimoja tu ndio kinaonyesha mikutano live kwenye TV. Hivi jamani sie ambao tuko mbali hatuwezi kuwafata tutaskiaje sera?? Kuna watu wanahitaji mabadiliko kweli lakini akipigwa swali kwanini unahitaji mabadiliko hana jibu.

Sio wote tuna upeo mkubwa wa kufikiria mambo, kuna watu wengi sana wanalilalamikia hili suala na wanashangaa Ukawa kwanini isifanye hivi kwenye kipindi hiki cha siku zilizobaki zote. Watu bado wanahitaj kujua sera za kila chama ili wafanye maamuzi sahihi October 25, lakin kila wanapofungua TV channel zaidi ya mbili zinaonesha mkutano wa chama kimoja.

Kuonesha kwenye TV na kitangaza redioni ni moja wapo na kusambaza sera za chama na watu kuskiliza na kuchanganua kwa umakini. Taarifa ya habari haitoshi maana hutumia muda mchache sana hivo ni vigumu kujua mambo mengi yaliyozungumziwa.

Ukisikia bao la mkono, sio lazima waibe kura, hata kuonesha kwenye TV linaweza kuwa bao la mkono, Ukawa jipangeni.
 
Kurusha live ni gharama sana, huwezi jua bajeti hao imekaaje?
 
Huo ni mkakati wa ukawa.mgombea wao sio mzuri kwenye kuongea,wanaogopa anaweza kuharibu akiwa live itamshusha hivyo wameona bora watoe vipande vilivyotengenezwa kwa ustadi mkubwa. Msubiri tu atakuja
 
bajeti ya chopa ipo lakini bajeti ya kurusha mikutano live ikosekane??? nitakuwa wa mwisho kuamini hili
 
Umeongea point yao, finishing ya uhakika sasaiv ndo muhimu zaidi. Halaf watu watawanyike waende vijijini
 
Mbona inarushwa jamani. Tatizo nyie mnaangalia tvccm tuu
 
Jana mwanangu wa miaka 10 alisema sorry dad kwa sasa mimi nampenda Magufuli.... lakini alisema hivo baada ya kuona star tv Magufuli akiita mtoto mmoja aje pale jukwaani.... watu wengi wanao kaa nyumbani kama ma house girls, mashamba boi kwa sasa wanatizama sana star tv ili kuona wasanii lakini on the process ni wapiga kura na wanabadilishwa kuchagua ccm.... bado kuna wanao taka taarifa kwa kuwa wako mbali na kwa ujumla wake binadamu anacho kisikia na kukiona mara kwa mara ndo anacho kiamini..... ukawa amkeni kwenye hili.... hasa kwa hizi siku chache zilizo baki...
 
Sio kurusha tu kwenye TV hata ofisi wamepanga na ruzuku wanapata
 
Mabadiliko hayaepukiki, kibali kimetoka kwa Muumba wa Mbingu na nchi. Mfumo dhalimu lazima ung'ooke!
 
That nigga is very smart.sidhani kama haelewi anachokifanya.
 
Ukawa wakionyesha Live inamaana watashindwa kutengeneza nyomi ya photoshop
 
bajeti ya chopa ipo lakini bajeti ya kurusha mikutano live ikosekane??? nitakuwa wa mwisho kuamini hili

Wanaogopa wakiweka Live watu watabaki nyumbani na kuacha viwanja empty...
Ccm wenzao wamefanikiwa kuonyesha Live na pia kujaza nyomi
 
na nyie mnaotengeneza nyomi lenu la kusomba watu na malori na wale wanaohudhuria shoo ya fiesta ya bure?
 
UKAWA mwendo ni uleule wa kukimbiza mwizi kimyakimya,kelele October 26 na kuendelea.
 
Jana mwanangu wa miaka 10 alisema sorry dad kwa sasa mimi nampenda Magufuli.... lakini alisema hivo baada ya kuona star tv Magufuli akiita mtoto mmoja aje pale jukwaani.... watu wengi wanao kaa nyumbani kama ma house girls, mashamba boi kwa sasa wanatizama sana star tv ili kuona wasanii lakini on the process ni wapiga kura na wanabadilishwa kuchagua ccm.... bado kuna wanao taka taarifa kwa kuwa wako mbali na kwa ujumla wake binadamu anacho kisikia na kukiona mara kwa mara ndo anacho kiamini..... ukawa amkeni kwenye hili.... hasa kwa hizi siku chache zilizo baki...

Tatizo hizo tv station unazoangalia,achana na TeeBc na nyota tv
 
Tatizo hizo tv station unazoangalia,achana na TeeBc na nyota tv
mkuu sio mimi.... mi niko bize mbaya... ukija home wanaangalia... huwez wazuia.... wanataka muona diamond na hadija kopa on the stage.... hili suala ni pana zaidi yangu... ukawa amkeni....
 
Huo ni mkakati wa ukawa.mgombea wao sio mzuri kwenye kuongea,wanaogopa anaweza kuharibu akiwa live itamshusha hivyo wameona bora watoe vipande vilivyotengenezwa kwa ustadi mkubwa. Msubiri tu atakuja

Anayetengeneza nani na wanarusha wapi.
Huiui kitu wewe
Wanatumia vifaa vya kisasa na kutrusha live Kwa kupitia channel itv
Mikutano yote ins kuwa hivyo
 
Uchunguzi uliofanyika unaonyesha mikutano ya live inamharibia zaidi Lowassa kuliko kumjenga. Hapo maswali kuhusu afya yake huibuka zaidi kuliko wakati wowote ule.
 
Kamanda changeni pesa mikutano ionekane live kwenye TV.

Siyo suala la kutamani tu.

Ni suala la pesa makamanda.
 
Uchunguzi uliofanyika unaonyesha mikutano ya live inamharibia zaidi Lowassa kuliko kumjenga. Hapo maswali kuhusu afya yake huibuka zaidi kuliko wakati wowote ule.

Da idawa hata wewe?
 
Back
Top Bottom