TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,542
- 28,520
Ufafanuzi mwingine...
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-uchaguzi-serikali-za-mitaa.html#post11378108
Nyingine inaweza kuwa hii ya idadi ya waliojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi huo: Home
Watanzania milioni 11,491,661 kati ya milioni 18,587,742 (asilimia 62) wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Jumapili ijayo.
Mikoa ya Katavi na Kagera imefanya vizuri kwa kuandikisha wapigakura wengi zaidi huku mikoa ya Dar es salam na Kilimanjaro ikiandikisha idadi ndogo.
Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa uchaguzi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Luanda alisema Watanzania hao ni sawa na asilimia 62 ya walioandikishwa wanatokana na taarifa za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ambayo yalionyesha kwamba asilimia 40 ya Watanzania wote wana umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Akizungumzia kuhusu mikoa iliyofanya vizuri, alisema Katavi umeandikisha wapigakura asilimia 79 wakati Kagera ni asilimia 78.
Kwa mujibu wa Luanda, mikoa iliyoandikisha wapigakura wachache ni Dar es Salaam asilimia 43 na Kilimanjaro asilimia 50.
Luanda alibanisha kuwa Halmashauri zilizovuka lengo ni ya Mji wa Mpanda(107%) na Mji wa Babati (101%) wakati zilizoandikisha kwa asilimia ndogo ni Kilindi (21%) na Same (22%).
"Katika uchaguzi huo karatasi za kupigia kura zitaandaliwa na Halmashauri husika na ambayo itakuwa sifa ya jina la mgombea, jina la chama, nembo ya chama na Nembo ya halmashauri na ingizo jipya ni Nembo ya Chama ili kuwasaidia wale wasiojua kusoma," alisema Luanda.
.....................
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-uchaguzi-serikali-za-mitaa.html#post11378108