UKAWA mnaujua huu mchezo mmbaya wanaofanya CCM?

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,496
1,035
Ndugu wana jamvi siku hazigandi na kama mjuavyo uchaguzi wa serikali za mitaa umekaribia na siku za kujianndikisha zilizotolewa ni chache sasa mnaweza amini kuna vijiji vingine havina taarifa ya uandikishwaji wa wapiga kura kwenye daftari ? Na sema hivi nikiwa na hakika kwa vile kipindi cha nyuma kuna magari yalikuwa yakipita na kutoa matangazo kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi na ikibidi walikuwa wakiwahamasisha viongozi wa kidini kuhamasisha waumini wao kujitokeza kwa wingi kwenye daftari la wapiga kura ni nini kimejificha nyuma ya pazia mpaka leo hii baadhi ya maeneo zoezi linapelekwa kimyakimya au hii ndio demokrasia?
Chonde ukawa amkeni toeni matangazo kwenye media zinazosikika vyema huko vijijini kutoa hamasa au tumieni wale wawakilishi wenu kupita nyumba hadi nyumba kutoa elimu huu ndio wakati wa lala salama.
 
Back
Top Bottom