Ukawa,la madiwani sawa ila vipi kuhusu hili!?

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
May 24, 2013
1,072
2,000
WanaJf,

Mtakumbuka kuwa uchaguzi wa mameya jijini DSM umeahirishwa kufuatia rafu za chama tawala kuleta madiwani toka Zanzibar ili tu kuzuia nguvu ya upinzani isishinde.Ktk mazingira sawia ya kidemokrasia,ukawa ndio wanapaswa kutoa mameya wa Kinondoni,Ilala na yule wa Jiji.Lakini inavyoonesha Ccm hawataki kuliona hili likitokea na kitendo cha kuahirisha huu uchaguzi eti kusubiri mwongozo toka Tamisemi ni kama janja Fulani hivi ya kujiandalia ushindi.

Kama mtanzania mwenye Uhuru wa kutoa maoni yangu,ninapata wasiwasi sana na huu uteuzi wa mawaziri toka nje ya wabunge wa majimbo wa Ccm.Wengine humu tumekuwa tukiwakejeri wanaccm kuwa wamechagua wabunge wasio na uwezo kiasi kwamba hadi Rais analazimika kuteua mawaziri toka nje pengine bila kulifikiria hili.Ikumbukwe pia uteuzi huu wa baraza ukiutazama ni kama una shinikizo fulani hivi toka kamati kuu ya chama tawala.

Kama ilivyokuwa kwa madiwani,mawaziri hawa walioteuliwa huenda wakalazimishwa kuwa wajumbe wa halmashauri za jiji la DSM.Hebu fikiria,eti kati ya nafasi 10 za wabunge wa Rais,tayari ameshateua zaidi ya sita ndani ya miezi miwili tu.Hii ni rekodi ambayo hata Vasco da Gama na udhaifu wake wote hakuifanya.

Wito wangu kwa Ukawa;wanadsm wameshaamua kuchagua mabadiliko.Nawaomba msikubali uvunjwaji wa demokrasia kama ule wa Tanga mjini.Na kiukweli hawa wateuliwa msipowadhibiti ndio watakaowapokonya ushindi.Hapa simaanishi Rais azuiwe kuteua,la hasha!! Bali itazamwe namna gani hawa wateule hawauathiri huu uchaguzi.Vinginevyo msishangae kuwakuta ukumbini siku ya uchaguzi kina Mhe. Ndalichako,Possy,Mahiga,Mpango,Tulia na wengineo ilihali ni wajumbe wa Kibondo,Kasulu,Iringa,Mbeya na kwingineko!!
 
Last edited:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom