UKAWA kuweni macho, mnachezewa shere

UKAWA kuweni macho, mnachezewa shere

The August

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2018
Posts
1,079
Reaction score
2,027
Katika dunia kuna watu wanaitwa waamini kupita kiasi (mwandishi mmoja aliwaita True Believers) kwa kiingereza rasmi hawa ni Fanatics. Ni watu wenye kuamini jambo kuliko kawaida. Kuamini kwao jambo kuna wafanya hata tafakari (Crtical Thinking) waweke pembeni.

-Na imani hii hujengwa sana na Chuki. Chuki dhidi ya kitu au mfumo fulani. Wakiaminishwa mtu au mfumo fulani ndio chanzo cha hali zao mbaya au matatizo yao. Mfano Sheikh maaruf aliyeitwa Sheikh Ilunga (Mungu amrehemu) aliweka fikra aliyoiita Mfumo Kristo. Huyu aliamanisha matatizo ya waislam yanatokana na wakristo kushika system ya utawala. Hivyo ili uislam ufanikiwe ni lazima wapambane na mfumo huu. Kule Israel, wana Israel wanaaminishwa chanzo cha wao kutotanuka ni ulimwengu wa kiarabu, hivyo adui wa kwanza wa wayahudi ni Muarabu. Hapa kwetu Tanzania, harakati za kisiasa za upinzani zinajengwa katika imani ya chuki kuwa Tatizo kuu la nchi hii ni CCM. Ili mabadiliko chanya ya kimaisha yatokee ni lazima CCM ipingwe kwa namna yoyote. Hivyo jambo lolote linalohusishwa na CCM ni lazima lipingwe.

-Moja wa kundi zuri la watu hawa ni wale waitwao 'masikini wapya'. Hawa ni watu walishawahi onja ladha ya maisha mazuri bahati mbaya yakakatishwa. Ni watu ambao wanaishi na kumbukumbu za maisha mazuri. Hivyo wanayatamani tena. Watu hawa wanahitaji tu kiongozi kuwajengea chuki na kuambiwa mchawi wenu ni fulani. Mtu huyo kwao ni kama Mungu. Chochote asemacho au afanyacho humuamini pasi na shaka. Kiongozi huyu huwapa sumu shida ni mfumo. Mfano wao ni watu waliofukuzwa kazi, wastaafu, wanafunzi wa vyuo (ndoto za boom bado zipo). Ni tofauti na masikini wa kuzaliwa. Hawa hawajawai onja maisha mazuri. Hawaamini kuwa ni mfumo au mtu ndiye chanzo chao kuwa hivyo, bali ni jambo la kuzaliwa. Ndio maana vijijini ni kijani tupu.
(Power of psychology).

-Hawa ndio waamini. mfano wale wanajitoa muhanga, au wanaojiua mpirani, au washiriki wa harakati za kisiasa. Lakini bahati mbaya ni wajanja wachache ndiyo wanufaikao na mfumo huo kama ukibadilika lakini wajanja zaidi hunufaika wakati wa harakati hiyo... Nataka kusema nini.

Zitto Kabwe ni msomi, ni mwenye akili sana (intelligent) hii inaboreshwa sana na tabia yake ya kusoma sana Vitabu. Vitabu vinaongeza maarifa, vitabu vinafanya mtu aijue dunia kiundani.

Msomi huyu anajua vyema kutumia fursa kuu iliyopo katika siasa za Tanzania. Chuki ya watu dhidi ya CCM. Fursa hii inachagizwa na uhaba wa upinzani wenye dira na uwezo mkubwa wa kuishi kwa agenda.

CCM walimjua kitambo hii ni 'asset' muhimu na imekuwa ikiwasaidia katika nyakati mbalimbali. Sitaki kuelezea ninachokiamini (kuwa huyu ni mtu wao miaka yote), ila nataka tutafakari nanyi matukio na visa mbalimbali ambavyo bwana huyu vimemuhusu lakini mwisho wake ni haueleweki na ni faida kubwa kwa serikali ya CCM. Nitaeleza machache sana. Mengine tutayatafakari baadae.

1.5 Trilion.

Katika kipindi cha bajeti, mambo kadhaa huibuka. Mambo haya mara nyingi huzima mjadala wa bunge. Iwe kwa makusudi au bahati mbaya, lakini husaidia bajeti kuisha na kupitishwa bila mjadala magazeti na kwenye mitandao ya jamii. Tunakumbuka suala la babu wa liliondo lilivyozima mjadala wa bajeti.

Sakata hili lilibuliwa na CAG. Na likashika hatamu kipindi cha Bunge la bajeti mwaka jana. Hakika mjadala wa 1.5 T ulikua mkubwa kiasi hata bajeti haikujaliwa tena. Kiranja wa suala hili alikua ni zitto kabwe.

Akili ilipo: Mtoa hoja alijua kuwa suala hili bunge lile halikuwa mahala pake kujadiliwa na kusingekuwa na effect yoyote ya mjadala ule. Bunge la mwezi huu ndio linajadili hoja hii. Hivyo harakati zote hizi unaweza zitafsiri kama babu wa Liliondo kufunika mjadala wa bajeti.

CAG v Spika.

Nilicomment sehemu moja kuwa CAG ni lazima atareport bungeni. Zitto anajua fika kuwa Speaker anayo mamlaka kama mkuu wa muhimili anazo nguvu fulani fulani. Anayo mamlaka makubwa. Mamlaka haya hayajaribiwi kabisa. Kwenda mahakami kufungua kesi hii ni kuendeleza harakati ambayo faida yake nitaieleza kwenye hitimisho lakini faida ya awali, mjadala huu unalengo la kufifisha mjadala wa sheria ya vyama vya siasa.

ZITTO v SHERIA YA VYAMA.

Zitto ni mbunge wa takribani miaka 20 sasa. Anajua taratibu nyingi za kibunge. Muswaada wowote kuna hatua za kibunge kuupinga. Mahakama ni hatua ya Pili baada ya kwanza kushindwa.

Mchezo ulipo: Mwaka fulani CWT waliitisha mgomo. Mgomo huu waliuitisha siku ya Ijumaa. Unaweza jiuliza kuwa wao hawajui effect yake. Ni makosa ya kimkakati. Unaweza dhani ni mapunguani ila watu wako kazini. Ndio mgomo ule uliitishwa na kusitishwa sbb uliitishwa muda usio sahihi. CWT walijivua kuwa wao wamechukua hatua, ni hadaa kwa walimu.

Kwenda mahakami kupinga muswada wa vyama vya siasa ni danadana na hadaa za kisiasa. Watu waamini na kutulia kuwa zipo juhudi za kupinga huku muswada ukiendelea na taratibu za kupitishwa...

TARGET:

Baada ya kuwa nje ya Ukawa mwaka 2015, CCM wanahitaji mtu wa 'juu' katika UKAWA ya 2020. Zitto ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuwa na wazo la Unganiko la vyama na asasi mbalimbali kudai demokrasia (Democratic Front). Wazo hili lilipokewa vyema na wadau. Na hata mkutano wa Zanzibar,2019 ni matokeo ya juhudi na hamasisho la Mh Kabwe. Mikakati yote ya awali, Mh Kabwe anayo. Hadi sasa tayari CCM wanae mtu ndani ya UKAWA. Harakati zote za Kabwe kuanzia 2015 na hakika ni yeye ndiye aliyejua vyema kucheza na siasa za nyakati hizi za JPM. Siasa zinazohitaji akili kubwa kuzimudu kama mpinzani. Hakika ni zitto ndiye aliyezimudu. He is intelligent enough kudeal na upinzani na wapinzani.

UKAWA KAENI MACHO, BINAFSI SIJAWAHI MUAMINI KAMWE ZITTO.

Ni maoni tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji120]
IMG_20190117_222516.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Post ndefu nikadhani una jipya kumbe ni kutuambia Zitto humuamini. Ni hivi wengi wetu hatumuamini Zitto lakini hilo halipunguzi ukweli kwamba ana uwezo wa uongozi kuliko Magufuli. Tutamvumilia na mapungufu yake kwani ccm kwetu haitulipi
Uongozi na Umamluki.

Nimeipenda sana hii.Umeandika kile ambacho ninakiwaza kila wakati.Hongera mkuu
 
Back
Top Bottom