UKAWA kumpata mgombea Urais Jumamosi

UKAWA kumpata mgombea Urais Jumamosi

Masanilo

Platinum Member
Joined
Oct 2, 2007
Posts
22,283
Reaction score
4,556
Breaking News

Ndani ya Masaa 48, mgombea urais kupitia UKAWA atajulikana. Mazungumzo yanaelekea kufikia muafaka. Stay tuned.

Mungu bariki UKAWA.

Mungu bariki Tanzania.

Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA), katika kikao walichokaa jana wamepanga kutangaza mgombea Urais atakayeungwa Mkono na vyama vyote vinavyounda Umoja huo.

Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi mpya katika jengo la LAPF Makumbusho, Kijitonyama.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Wabunge wote wa Kambi rasmi ya Upinzani.
 
Unaanza kuongea visivyokuwepo, kwani vikao vya ukawa ni siri
 
Hamna ratiba?yaan watu wanakurupuka tu!kaazi kweli
 
Ukawa wanapoteza muda tu na wangejua bora hata wasisimamishe mgombea
 
Kwa namna mazungumo yanavyo endelea ni dhahiri kwa namna yoyote ile mgombea wa urais kupitia UKAWA atatoka Chadema.

Vigezo

1. Chadema ndio chama chenye mtandao mkubwa uliopenya mpaka Vijijini kwenye ngazi ya msingi miongoni mwa vyama vyote vilivyo katika ukawa. Hakuna ubishi kwamba baada ya ccm Chadema ndio chama kinachofuata kwa mtandao.

2. Kama matokeo ya serikali za mitaa ni kigezo cha kutoa mgombea urais, Chadema ndio chama kinacho ongozwa kwenye matokeo ya serikali za mitaa miongoni mwa vyama vinavyo unda ukawa. Pekee Kimeshinda 30% kabla ya kuchanganya na matokeo ya vyama vingine vya UKAWA.

3. Chadema Kina mtaji wa kura za urais wa 2010 kwa kushika nafasi ya pili, ndio chama kilichotoa mgombea bora aliyepata kura nyingi miongoni mwa vyama vya upinzani. Dr Slaa alishika nafasi ya pili nyuma ya JK tena kwa kuchakachukiwa.

4. CUF wamesha weka mgombea urais Zanzibar ambaye ni maalim seif. Kwa dhana ya ushirikiano na mashirikiano ya Ukawa CUF watakuwa wenye dhamira mbaya naya hovyo kama watang'ang'ania kusimamisha mgombea Bara kama ambavyo Prof Lipumba alivyo anza harakati za misikitini naza udini kuwa yeye ndio anafaa kuwa mgombea.

Kama CUF watang'ang'ania na kutaka kusimamisha mgombea maana yake ni kwamba hawana dhamira na kitu kinachoitwa ukawa bali watakuwa wabinafsi wasiotaka kuona watanzania wana ondokana na dude liitwalo ccm.

Nani kikwazo mpaka sasa.

UKAWA wanaweza kuwa wamechelewa kutaja mgombea urais wao mpaka sasa kwa sababu zifuatazo.

1. Undumila kuwili wa Prof Lipumba, mpaka sasa amekosa busara za kiungozi kwa ku fight na kujiona yeye au chama chake kina sifa ya kutoa mgombea Bara.

2. Hofu ya kijinga ya CUF kutokukubali kwamba Chadema ni chama chenye nguvu na mvuto kuliko chama chao.

3. Ziara anazo fanya Prof Lipumba mikoani ni ushahidi kuwa anafanya maandalizi ya kampeni za urais wa CUF lakini sio wa UKAWA

4. Hatua ya CUF kutangaza mgombea urais wao bila kukubaliana na wenzao wa UKAWA kuna ibua mashaka ya dhamira zao juu ya Ukawa.

Kwa hatua ya sasa mchawi wa UKAWA ni nani?!

Jibu ni rahisi sana! Mchawi ni Prof Lipumba wa chama cha wananchi CUF
 
Lema na wenzake wengi wanatamani kuchukua fomu za kugombea urais lakini wanaogopa kuitwa wasaliti

Wenzako wenye uchungu na CCM yao wapo Dodoma hoi, hata makofi na vigelegele havipigwi kwani hali ni tete
 
Ukawa wanapoteza muda tu na wangejua bora hata wasisimamishe mgombea

Wenzenu Dodoma wanatoana macho, kwanza wabunge wenu wamegoma kwa kuwashushia kiinua mgongo na lowasa anasema msipo mpitisha patachimbika
 
Wanasubiria muhanga wao Lowassa- uliwahi kusikia CDM wanamsema vibaya Lowassa face to face? Agenda yao ni kuupelaka urais kasikazini, haijalishi how
 
MsakaGamba

Nashindwa nijibu kitu gani ila naamini kuwa kila chama kina haki ya kuchagua mgombea urais wake na mwisho wa siku washiriki wote wa Ukawa watamchagua mwenye sifa kama ulizozitaja hapo juu
 
Last edited by a moderator:
Jambo la kusema mgombea kupitia ukawa atafahamika ni kupoteza muda, unadhani hao watu wana mwingine zaidi ya huyo SLAA? Chadema kumuachia CUF, NCCR au NLD hilo halipo
 
Kikao kimemalizika na kutoka na azimio hilo, kwamba Jumamosi atajulikana rasmi mgombea
 
MsakaGamba, Lipumba yuko very strategic. Kwa makubaliano ya Ukawa mwache aendelee na kampeni zake
 
Last edited by a moderator:
Jumamosi atajulikana rasmi, tayari kikao kimemalizika
 
Back
Top Bottom