UKAWA isiwe sababu ya kurudisha jimbo la Mwanga CCM

kidika

Member
Jun 22, 2014
49
22
Wanabodi-

Naomba niandike machache na msingi sana juu ya wilaya ya Mwanga kisiasa na hali inayiendelea kwasasa kwenye Ukawa.

Kumezuka katabia kabaadhi ya vyama vilivyomo kwenye Ukawa kuanza kudandia majimbo ambayo hawajawahi kufanya kazi za kisiasa zozote zile. Kwasasa hapa Mwanga Nccr nao wanataka jimbo la Mwanga kisa nao wapo kwenye Ukawa, hii ni aibu na hatari sana kwakazi kubwa iliyofanywa na Chadema Wakiongozwa na Kamanda Kilewo tokea 2011 na hatimaye wapare wameelewa nini maana ya mabadiliko sasa wanataka kukatuzwa ndoto zao za chachu ya mabadiliko iliyokuwa imefutika siyo tu mwanga bali pare yote mpaka same.

Viongozi wetu wawe makini sana na jambo hili kwakuww litawarudisha watu wengi nyuma waliyoamua kujitolea na kufilisika na wengine hata kupelekea kufungwa na kuachana na wenza wao. Ukienda maeneo ya Lang'ata,Kirya,kileo,ngujini,kilomeni,kifula,shighatini,mwaniko,kighare,chomvu,kirongwe,tologha,kwakoa hawawezi kusikia hadithi nyingine isipokuwa Chadema pekee.

Sijui ni kauli ipi itatumika kuiweka Nccr pale Mwanga, kama kunawatu ambao angalau wangepaswa kunyanyua mdomo juu ya Mwanga ilikuwa ni Cuf not Nccr. Hawa hawana hata kiongozi wa wilaya,kata,kijiji ndiyo sasahivi wanapita kwenda kutafuta viongozi tena wanapita kwenye viongozi wa Chadema kuwalaghai kuwa jimbo hilo limeachiwa wao Nccr.

Kama Ukawa wanania ya kuongoza Tanzania yetu wasigawane majimbo kama pipi, ninauhakika kama Nccr wakipewa hilo jimbo ccm hawatafanya Kampeni na itakuwa furaha kwao huku wanachadema wakiachwa kwa majonzi makubwa kwani kazi waliyoifanya kwa muda mrefu waroho wachache wameamua ipotee.

Tutalaani sana vyama hivi vya Ukawa kwa kuipoteza Mwanga, wapiganaji wengi wataumia sana, sidhani kama itakuwa ni haki Kwa wanachadema wa Mwanga.

Viongozi wa Ukawa kuweni na huruma na Wananchi wa Mwanga msiwafanye waendelee kuwa mateja ya ccm wapeni chaguo lao.

Acheni biashara ya kutaka kufurahishana kama wanaukwa, msigawe majimbo kwa idadi ya namba mtapoteza majimbo mengi na mtashindwa kuongoza serikali.

Ushauri wangu:
Busara na weledi unahitaji kuhusu mwanga kuliko kufanya maamuzi ya kutaka kugawa mwanga kwakutumia kumuenzi Marehemu Dr.Mvungi. sidhani hata yeye kama angalikuwa hai angekubali Mwanga ipotee kwa kigezo hicho kisichokuwa na mbele wala nyuma.
 
Ulichokiongea ni ukweli mtu mkuu, kwasasa watu wameamua kunyamaza na kukaakimya wamebaki na sintofahamu juu ya maigizo hayo.
 
Acheni kulalamika kama watoto wadogo mnataka majimbo yote wasimamishe chadema sasa nini maana ya uwepo wa ushirikiano
 
CHADEMA Mwanga lazima ipitie jimbo hilo, Maghembeeee afanya kazi ya kufundisha iwapo bado kichwa iko
 
Anaesimama ni wa Chama au wa Ukawa. Mnatuchanganya sasa! Maana kumeanza kuwa na mgawanyiko, Chama na Ukawa. Ukawa ni Mnyama gani saaa?
 
Kwani Mwanga wanaishi wapare peke yao? Hakuna watanzania wengine huko......inavyoonekana huko wanachagua mtu na sio uwezo wa mtu
 
KILEO ACHA WOGA WA KIKE,
Wewe ulikuwa unajenga CHADEMA mikoa mingine ikiwamo DAR es Salaam, Mwenzako Mwanasheria Msuya alikuwa anajenga nyumbani Mwanga. Iweje uanze kuogopa mapema, eti usipochaguliwa wewe wa CHADEMA CCM watashinda, shamee broo tulia. Msuya aongoze jahazi la UKAWA Mwanga ooyyeeeeeee
 
KILEO ACHA WOGA WA KIKE,
Wewe ulikuwa unajenga CHADEMA mikoa mingine ikiwamo DAR es Salaam, Mwenzako Mwanasheria Msuya alikuwa anajenga nyumbani Mwanga. Iweje uanze kuogopa mapema, eti usipochaguliwa wewe wa CHADEMA CCM watashinda, shamee broo tulia. Msuya aongoze jahazi la UKAWA Mwanga ooyyeeeeeee

Chukua LIKE
 
Ikitokea hili ndio tutajua kama Kileo ni kamanda wa kweli au wa kuchonga.

Kileo ebu kuwa mpole, cheo ni dhamana tu na kugombea ubunge sio kama mkopo wa benki kusema kuwa lazima ugombee kwa sababu ulishatumia pesa nyingi.

Kama msemavyo "UKAWA ndio mpango mzima",ebu msigeuke saizi.Songa mbele Kamanda.
 
Sasa si hata akisimamishwa mgombea wa NCCR hao wafuasi wa CHADEMA wataambiwa na viongozi wao waichague NCCR na kampeni itafanywa kwa kushirikiana.

Na kama mmewaaminisha hao wapare kuwa mabadiliko ni CDM pekee,mliungana na NCCR ili iweje?

Acheni ubinafsi.
 
KILEO ACHA WOGA WA KIKE,
Wewe ulikuwa unajenga CHADEMA mikoa mingine ikiwamo DAR es Salaam, Mwenzako Mwanasheria Msuya alikuwa anajenga nyumbani Mwanga. Iweje uanze kuogopa mapema, eti usipochaguliwa wewe wa CHADEMA CCM watashinda, shamee broo tulia. Msuya aongoze jahazi la UKAWA Mwanga ooyyeeeeeee

Hivi Henry Kilewo alishawahi kuishi Mwanga? Muda wote namuonaga Kinondoni
 
panahitaji upambuzi yakinifu hapo, sio hoja ya kuidharau hii, sote tunajua jinsi watz wanavokariri, hapo kama wameimbishwa cdm, kuwapeleka ukawa yaweza kuwa kazi kiasi chake
 
sasa si hata akisimamishwa mgombea wa nccr hao wafuasi wa chadema wataambiwa na viongozi wao waichague nccr na kampeni itafanywa kwa kushirikiana.

Na kama mmewaaminisha hao wapare kuwa mabadiliko ni cdm pekee,mliungana na nccr ili iweje?

Acheni ubinafsi.

issue hapa, ni kwamba cdm wamewekeza muda mrefu mpaka wananchi wamewaelewa, mwanga hakuna nccr, ni cdm na ccm tu. Sasa haya mambo ya ukawa yanatuchanganya tu. Bora wangekubaliana hukohuko kwenye mambo ya urais.
 
issue hapa, ni kwamba cdm wamewekeza muda mrefu mpaka wananchi wamewaelewa, mwanga hakuna nccr, ni cdm na ccm tu. Sasa haya mambo ya ukawa yanatuchanganya tu. Bora wangekubaliana hukohuko kwenye mambo ya urais.

Kila jambo lina changamoto zake,so hii ni changamoto kwa UKAWA lakini sidhani kama wanaweza fanya uamuzi wa aina hiyo.
 
CHADEMA KWA MWANGa KAMA KWELI MMEWAPA NCCR BASI TULIKURUPUKA KIMAAMUZI TENA SANA!
-NIMEUMIA SANA!
##MUMGU IBARIKI CHADEMA .
##MUNGU IBARIKI UKAWA.
 
Back
Top Bottom