mchuku wa mangi
Member
- Jun 25, 2022
- 12
- 8
Mwaka 2025 siyo mbali kama Mwenyezi Mungu anakuweka hai,ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa kumpata Rais, wabunge na madiwani na kuna majimbo ya uchaguzi ambayo hakika makada watatoana jasho kweli kweli.
Jimbo la Mwanga ni moja ya majimbo nane ya uchaguzi mkoani Kilimanjaro ambalo kwa sasa mbunge wake ni wakili msomi Joseph Thadayo aliyerithi mikoba hiyo kutoka kwa profesa Jumanne Maghembe ambaye zama zake za kisiasa zinaelekea ukingoni.
Za chini chini zinatonya kuwa mchuano utakuwa mkali kwa makada watatu akiwamo Thadayo mwenye ,profesa maghembe ambaye anatajwa kuwa ameanza harakati za kujijenga ndani ya chama ili kupambania kombe huku mmoja wa wafanyakabiashara wakubwa na mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC), Seleman Mfinanga naye akitajwa kuja kwa kasi ya kutisha.
Wote watatu wanatajwa kuwa na nguvu kiuchumi na kisiasa lakini yote kwa yote mwamuzi ni kura ya maoni ndani ya chama na atakayechanga karata zake vizuri ndiye atayeibuka kidedea japo mwamuzi wa mwisho ni Kamati Kuu ya CCM.
"Thadayo lazima akaze kweli kweli maana kwa mwenendo uliopo kwa sasa asipokuwa makini anaweza asitetee kiti chake japo bado wana mwanga wanamkubali sana kutokana na kushughulikia changamoto nyingi za wananchi",anasema mmoja wa wananchi wa Shighatini.
Pamoja na huyo wapo wanaomtaja Mfinanga naye kuwa na nguvu kutokana na nafasi yake ya MNEC ambayo inamwezesha kuwa na mtandao mkubwa ndani ya chama katika wilaya ya Mwanga huku wengi wakimtaka maghembe apumzike wakidai hana jipya.
Wacha tusubiri,muda utaongea