UKAWA, hili ni bao la mkono mchana kweupe

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Kama mnafuatilia vizuri ni kwamba mkuu wetu mtukufu anafanya ziara zake mikoani kila siku,lakini awapo jukwaani hulitumia vizuri kwa dakika kadhaa kukinadi chama chake na hata kubishambulia na kuviponda vyama vya upinzani nchini. Hufikia hata kuwaita baadhi ya waliokua makada wa CCM na kuwaomba warudi kukijenga chama tena hadharani.Lakini kinyume kabisa na katiba kwa wale ambao hawakuchaguliwa hawaruhusiwi kufanya siasa hadi hapo 2020 wakati wa kutangaza wagombea wao.Sitaki kuuliza ni vipi wananchi watavifahamu hivyo vyama wakati wa kampeni tu maana sio swali tena ni mjadala uliopo wakati huu.

Sasa hapa kwa mtu mwenye uelewa wa kawaida usiohitaji PhD atajua kua kuna siasa ya chini kwa chini kuhakikisha kua upinzani unafutika nchini ili chama utawala kiendelee kusalia madarakani pamoja na ukongwe wake. Mimi hua nafikiri kua sera nzuri na utendaji wa mtu ndio kivutio kikubwa kwa wananchi kukupenda chama chake na sio kuwashawishi kwa kuwaponda wapinzani.

Huu ni mtihani mkubwa na mgumu sana kwa UKAWA na vyama vingine vya upinzani katika ustawi wake nchini, Vinalazimishwa kua "Dormant" kwa lazima na ikizingatiwa msajili wa vyama anavitaka kisheria vyama vyote kupitia kwa wananchi kutafuta uungwaji mkono kwa kueneza itikadi na kunadi Sera zao.Hapa ndipo mtu unafikia mahali kutafuta nini lengo kuu hasa la chama cha siasa mahali popote.

Naufananisha utalatibu huu na bao la mkono ambapo mfungaji ameshaona hakuna namna ya kutumia mguu(Katiba) kuufunga mpira huo bali analazimisha kwa mikono ili mradi refa atangaze goli tu mwisho wa mchezo.
 
Usidhani wananchi wa leo ni wajinga hata wao wanajiuliza iweje Magufuli tu ndiye anayefanya mikutano?

Jibu la haraka haraka linalowajia kichwani ni kuwa "vyama vingine vinaonewa", na hulka ya binadamu ni kum support anayeonewa.

Mfano mzuri angalia maeneo ambayo wapinzani walikuwa wananyanyaswa kama Mbeya, DAR, Arusha, Pemba, Kilimanjaro nk linganisha na Dodoma, Singida uone CCM waliambulia nini sehemu hizo.

Worse enough kwa kujua au kutokujua tamko lake limekifunga mikono hata chama chake kujitanua sehemu walizoshindwa kwa vile Magufuli peke yake hawezi kufanya mikutano kwenye majimbo yote.
 
Usidhani wananchi wa leo ni wajinga hata wao wanajiuliza iweje Magufuli tu ndiye anayefanya mikutano?

Jibu la haraka haraka linalowajia kichwani ni kuwa "vyama vingine vinaonewa", na hulka ya binadamu ni kum support anayeonewa.

Mfano mzuri angalia maeneo ambayo wapinzani walikuwa wananyanyaswa kama Mbeya, DAR, Arusha, Pemba, Kilimanjaro nk linganisha na Dodoma, Singida uone CCM waliambulia nini sehemu hizo.

Worse enough kwa kujua au kutokujua tamko lake limekifunga mikono hata chama chake kujitanua sehemu walizoshindwa kwa vile Magufuli peke yake hawezi kufanya mikutano majimbo yote.
Hivi ni kweli unaweza kukilinganisha CCM na SACCOS za Wachagga?
 
duuh, haya sasa, sitaki ukabila, na sitaki kuamin yale 'maneno' aliyosingiziwa ya baba wa taifa, eti "makabila makubwa siyo ya kuwapa nchi"

nadhani siyo kabila bali ni aina ya mtu,
lawama nyingi ziwaendee viongoz wa dini ambao nadhan wana nafas kubwa ya kumfunga paka kengele.

wametulia tuli... tofauti na miaka iliyopita.
sijui nao wametishwa.
hatuoni zile nyaraka na matamko..
 
Zamani walikiita chama cha wakatoliki, leo hii imekuwa chama cha wachaga [emoji1][emoji1][emoji1]
 
duuh, haya sasa, sitaki ukabila, na sitaki kuamin yale 'maneno' aliyosingiziwa ya baba wa taifa, eti "makabila makubwa siyo ya kuwapa nchi"

nadhani siyo kabila bali ni aina ya mtu,
lawama nyingi ziwaendee viongoz wa dini ambao nadhan wana nafas kubwa ya kumfunga paka kengele.

wametulia tuli... tofauti na miaka iliyopita.
sijui nao wametishwa.
hatuoni zile nyaraka na matamko..
Kama wana nia ya dhati wapewe tu katiba si ipo vingine vyote ni bora lakini sio FISIEM huyu ni mnyama haramu mwenye chapa ya shetani inayowakilisha ufisadi na unyonyaji ni mnyama aliyezoea vya kunyonga na vya kuchinja kwake ni batili.

ILAANIWE CCM NA WANACHAMA WAKE WOTE
 
Ba Ngosha & Co. Wameunderestimate nguvu ya Social Media. Tuone AmshaAmsha ikihamia Rasmi Facebook..History is there to be learned #Egypt/Tunisia
 
Nilitarajia ziara za Mtukufu Rais ziwe za kukaguwa na kuzindua miradi ya maendeleo. Badala yake imekuwa ya kujinadi yeye binafsi na chama chake na kuwaponda wapinzani huku akikiuka kauli zake mwenyewe, za kwamba sasa si muda wa kuhubiri siasa Bali maendeleo. This is not fair
 
Kama mnafuatilia vizuri ni kwamba mkuu wetu mtukufu anafanya ziara zake mikoani kila siku,lakini awapo jukwaani hulitumia vizuri kwa dakika kadhaa kukinadi chama chake na hata kubishambulia na kuviponda vyama vya upinzani nchini. Hufikia hata kuwaita baadhi ya waliokua makada wa CCM na kuwaomba warudi kukijenga chama tena hadharani.Lakini kinyume kabisa na katiba kwa wale ambao hawakuchaguliwa hawaruhusiwi kufanya siasa hadi hapo 2020 wakati wa kutangaza wagombea wao.Sitaki kuuliza ni vipi wananchi watavifahamu hivyo vyama wakati wa kampeni tu maana sio swali tena ni mjadala uliopo wakati huu.

Sasa hapa kwa mtu mwenye uelewa wa kawaida usiohitaji PhD atajua kua kuna siasa ya chini kwa chini kuhakikisha kua upinzani unafutika nchini ili chama utawala kiendelee kusalia madarakani pamoja na ukongwe wake. Mimi hua nafikiri kua sera nzuri na utendaji wa mtu ndio kivutio kikubwa kwa wananchi kukupenda chama chake na sio kuwashawishi kwa kuwaponda wapinzani.

Huu ni mtihani mkubwa na mgumu sana kwa UKAWA na vyama vingine vya upinzani katika ustawi wake nchini, Vinalazimishwa kua "Dormant" kwa lazima na ikizingatiwa msajili wa vyama anavitaka kisheria vyama vyote kupitia kwa wananchi kutafuta uungwaji mkono kwa kueneza itikadi na kunadi Sera zao.Hapa ndipo mtu unafikia mahali kutafuta nini lengo kuu hasa la chama cha siasa mahali popote.

Naufananisha utalatibu huu na bao la mkono ambapo mfungaji ameshaona hakuna namna ya kutumia mguu(Katiba) kuufunga mpira huo bali analazimisha kwa mikono ili mradi refa atangaze goli tu mwisho wa mchezo.
Vyama vya Upinzani ( VVU) zilikodishwa kwa mafisadi kwa miaka kwa gharama ya 13bilioni tshs. Sasa mnalalamika nini?
 
Zamani ilikuwa ngumu sana kwa mtu kuhudhuria mikutano ya ccm bila kwenda na Loli lakini sasa hiv.....
HIVI KINANA akiitisha mkutano watajaa kama wanavyo jaa kwa jpm?
 
Back
Top Bottom