UKAWA, hili ni bao la mkono mchana kweupe

UKAWA, hili ni bao la mkono mchana kweupe

Hivi ni kweli unaweza kukilinganisha CCM na SACCOS za Wachagga?
Siku zinavyokwenda mbele ndivyo uwezo wako wa kujadili hoja unavyo potea na kuwa mropokaji tuu.
Lakini wenye akili washajua tatizo liko wapi, kama mnaye muabudu anaweza kutamka hadharani mbele ya wanachama wake anaowaongoza "fyatueni tuu watoto bila idadi mie nitasomesha bure" halafu umati huo unalipuka kwa furaha na shangwe unategemea nini kutoka kwa watu wa aina hiyo?
 
Usidhani wananchi wa leo ni wajinga hata wao wanajiuliza iweje Magufuli tu ndiye anayefanya mikutano?

Jibu la haraka haraka linalowajia kichwani ni kuwa "vyama vingine vinaonewa", na hulka ya binadamu ni kum support anayeonewa.

Mfano mzuri angalia maeneo ambayo wapinzani walikuwa wananyanyaswa kama Mbeya, DAR, Arusha, Pemba, Kilimanjaro nk linganisha na Dodoma, Singida uone CCM waliambulia nini sehemu hizo.

Worse enough kwa kujua au kutokujua tamko lake limekifunga mikono hata chama chake kujitanua sehemu walizoshindwa kwa vile Magufuli peke yake hawezi kufanya mikutano kwenye majimbo yote.
...na ndiyo sababu kuu kwamba Donald Trump ndiye atakua rais ajaye wa Marekani.
 
Huyo tushamuonya lakini ndio hulka yake achana nae
Namjua kwa uchafuzi wa hali ya hewa mkuu! Unaweza ukawa unalipwa kwa unafki wako lakini kuna muda unatumia akili. Haya ndio maana hua hayana life span ndefu, siku akikosa anacholipwa na mauti humfikia.
 
Viongozi wa dini wana matatizo makubwa 2

1.Wanapewa misamaha ya kodi

2.Wanapewa Mirungura

3.Serikali imefumba macho wanapowaibia kabwera kupitia sadaka na zaka

4.Baadhi wanatunzwa na Serikali kuanzia nyumba, umeme, maji, chakula hadi boxer

5.Udini umewajaa. waaangalia huyu Isaya au ABDULLAHMAN?
 
Kuna neno au propaganda chafu nilizoea kuisoma hapa jf zaidi ikitoka lumumba na wakati mwingine kusemwa bungeni kutokea wabunge wa ccm nayo ni hii ' kuwanyesha vijana viloba ili waandamane'

Magu amelisema si mara moja au mbili. Hivi anaamini hivi ndivyo ilivyo ? Yaani watu (wapinzani) wanawanyesha vijana pombe ili waandame?
 
Kuna neno au propaganda chafu nilizoea kuisoma hapa jf zaidi ikitoka lumumba na wakati mwingine kusemwa bungeni kutokea wabunge wa ccm nayo ni hii ' kuwanyesha vijana viloba ili waandamane'

Magu amelisema si mara moja au mbili. Hivi anaamini hivi ndivyo ilivyo ? Yaani watu (wapinzani) wanawanyesha vijana pombe ili waandame?
Haviitwi VIROBA....4G au full network[emoji12] [emoji13] ngumu kumezwa
 
haa haa naona cuf wanaanza kunywea. cdm wasipofanya mikutano na maandamano kuanzia 1 septemba wajifute rasmi. wakumbuke siasa sio lelemama...
 
Mtukufu anataka vyama vya upinzani viwe Vyama vya Kushiriki Uchaguzi, lakini visilete upinzani wowote.
 
Hivi ukiandika bila kwa kujibu hoja tu bila lugha chafu utapungukiwa nini? Kwani shule yako ina kazi gani kichwani?
Vijana wa lumumba wanapata UDC kwa maneno ya aina iyo mkuu hata wanapiga wazee. So usiwalaumu wao walaumu hao wanaowapa udc.
 
Kama mnafuatilia vizuri ni kwamba mkuu wetu mtukufu anafanya ziara zake mikoani kila siku,lakini awapo jukwaani hulitumia vizuri kwa dakika kadhaa kukinadi chama chake na hata kubishambulia na kuviponda vyama vya upinzani nchini. Hufikia hata kuwaita baadhi ya waliokua makada wa CCM na kuwaomba warudi kukijenga chama tena hadharani.Lakini kinyume kabisa na katiba kwa wale ambao hawakuchaguliwa hawaruhusiwi kufanya siasa hadi hapo 2020 wakati wa kutangaza wagombea wao.Sitaki kuuliza ni vipi wananchi watavifahamu hivyo vyama wakati wa kampeni tu maana sio swali tena ni mjadala uliopo wakati huu.


Sasa hapa kwa mtu mwenye uelewa wa kawaida usiohitaji PhD atajua kua kuna siasa ya chini kwa chini kuhakikisha kua upinzani unafutika nchini ili chama utawala kiendelee kusalia madarakani pamoja na ukongwe wake. Mimi hua nafikiri kua sera nzuri na utendaji wa mtu ndio kivutio kikubwa kwa wananchi kukupenda chama chake na sio kuwashawishi kwa kuwaponda wapinzani.


Huu ni mtihani mkubwa na mgumu sana kwa UKAWA na vyama vingine vya upinzani katika ustawi wake nchini, Vinalazimishwa kua "Dormant" kwa lazima na ikizingatiwa msajili wa vyama anavitaka kisheria vyama vyote kupitia kwa wananchi kutafuta uungwaji mkono kwa kueneza itikadi na kunadi Sera zao.Hapa ndipo mtu unafikia mahali kutafuta nini lengo kuu hasa la chama cha siasa mahali popote.


Naufananisha utalatibu huu na bao la mkono ambapo mfungaji ameshaona hakuna namna ya kutumia mguu(Katiba) kuufunga mpira huo bali analazimisha kwa mikono ili mradi refa atangaze goli tu mwisho wa mchezo.
Utalatibu ndio nini...???

Rudi ufipa maana hujaelimika...
 
Back
Top Bottom