UKAWA Hamasisheni watu wajiandikishe Kawe, Kilombero na Katavi

UKAWA Hamasisheni watu wajiandikishe Kawe, Kilombero na Katavi

matasha

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
378
Reaction score
400
Matokeo ya serikali za mitaa yamenipa moyo sana. UKAWA ni kama wameshashinda Uchaguzi mkuu ila wanapaswa kufanya yafuatayo. Kuhamasisha watu wajiandikishe hasa vijana, kuhamasisha watu wapige kura na kuimarisha UKAWA yenyewe.

Ninawaomba sana UKAWA wanaoishi maeneo ya Kawe, Kilombero na Katavi mhamasishe watu wote hasa vijana wakajiandikishe. Kwa mujibu wa tangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na kwamba zoezi la kujiandikisha kwenye majimbo haya matatu ni la majaribio, halitarudiwa na litakamilika tarehe 21.12.2014. Halima Mdee jitahidi kawe hata kama ni kuwatembelea watu majumbani kuwahamasisha, kilombero Chadema ina nguvu sana makamanda jitahidini sana na Katavi pia.

Angalizo: Udhaifu mkubwa wa UKAWA ni kwamba tuna wafuasi wengi sana ukilinganisha na CCM ila hatujawahamasisha vya kutosha wajiandikishe na kupiga kura. Tukitumia nafasi hii kama walivyofanya Jubilee Kenya tutashinda. Kenya Raila alikuwa na ufuasi mkubwa ila tatizo wengi hawakujiandikisha na kupiga kura na hilo ndilo lilimwangusha.
 
Umenena vema sana mkuu...

Sidhani kama watu wengi wanajua kuwa hautorudiwa kwa maeneo tajwa
 
Tume imetoa tangazo magazeti ya leo kwamba halitarudiwa maeneo hayo. Chondechonde makamanda awa maeneo hayo jitahidini sana maana hakutakuwa na uandikishaji mwingine kabla ya uchaguzi mkuu
 
Halima Mdee analijua hilo, inabidii ahamisishe, watu wa DAR ni starehe kwenda mbele.Mikoani wako tayari kwa mabadiliko lazima watajitokeza sana.
 
na wewe hamasisha majirani zako familia yako pamoja na ndugu jamaa na marafiki waende mapinduzi yanaanza na wewe
 
Kujiandikisha ni haki yetu siyo mpaka tuhamasishwe na ukawa tuheshimiane tafadhari.
 
Naunga mkono hoja, tume wanaandikisha kimyakimya ili wananchi wengi wasijiandikishe ili kuipa ushindi ccm mwakani. Chondechonde wana ukawa fanyeni mikutano ya kuhamasisha watu wakajiandikishe maeneo hayo mwakani uandikishaji hautarudiwa tena. Nawaombeni makamanda wa kilombero na kawe hamasisheni hili na hakikisheni na wenyewe mjiandikishe.
 
ngoja nianze kuwasambazie ujumbe ndugu jamaa na marafiki
 
Asanteni kwakukumbushana mwakani tujitahidi tunakamilisha anguko la ccm rasmi
 
Mimi na wewe ndio tutaleta mapinduzi kwa kura zetu
 
Hili zoezi linaendeshwa kimya kimya sana nilikuwa maeneo fulani nikasikia watu wamejiandikisha na kupata kadi za mpiga kura nikabishana sana kumbe kuna ukweli bwana. Kwanini hawalitangazi sasa zoezi lenyewe? kama hapa Ifakara inamaana wakifanya hivyo watu wengi sana hawajiandikisha kwasababu hawajui na hakuna tangazo lolote lililotolewa na hakuna uhamasishaji na zimebaki siku tatu kuanzia leo.
 
.... Mimi Mwenyewe Niliweka Post Kama Hii Jana, Nasikitika Sana Kuona Ukawa Wako Kimya Kana Kwamba Hakuna Kinachoendelea
 
Matokeo ya serikali za mitaa yamenipa moyo sana. UKAWA ni kama wameshashinda Uchaguzi mkuu ila wanapaswa kufanya yafuatayo. Kuhamasisha watu wajiandikishe hasa vijana, kuhamasisha watu wapige kura na kuimarisha UKAWA yenyewe.

Ninawaomba sana UKAWA wanaoishi maeneo ya Kawe, Kilombero na Katavi mhamasishe watu wote hasa vijana wakajiandikishe. Kwa mujibu wa tangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na kwamba zoezi la kujiandikisha kwenye majimbo haya matatu ni la majaribio, halitarudiwa na litakamilika tarehe 21.12.2014. Halima Mdee jitahidi kawe hata kama ni kuwatembelea watu majumbani kuwahamasisha, kilombero Chadema ina nguvu sana makamanda jitahidini sana na Katavi pia.

Angalizo: Udhaifu mkubwa wa UKAWA ni kwamba tuna wafuasi wengi sana ukilinganisha na CCM ila hatujawahamasisha vya kutosha wajiandikishe na kupiga kura. Tukitumia nafasi hii kama walivyofanya Jubilee Kenya tutashinda. Kenya Raila alikuwa na ufuasi mkubwa ila tatizo wengi hawakujiandikisha na kupiga kura na hilo ndilo lilimwangusha.
Mbona gazeti la Nipashe kama sikoei limendika kuwa kwa jimbo la Kawe wanafanya majaribio kwenye kata 2 tu za Bunju A na Mbweni tu??? Ukweli ni upi?
 
pia watu wange takiwa wajulishwe hili zoezi ni kwa watu wote au nikwawale ambao hawana vitambulisho vya kupigia kura
 
Kujiandikisha ni haki yetu siyo mpaka tuhamasishwe na ukawa tuheshimiane tafadhari.

Hakuna rangi mtaacha kuiona mwaka huu! Hizo porojo zako peleka lumumba kwa misukule wenzio.VIJANA TUPO TAYARI KUJIANDIKISHA NA KUIPELEKA CCM KUZIMU
 
Back
Top Bottom