UKAWA acheni utoto!

Ndio hapo nimeshangaaje na kusikitika mwanzoni nilisema hawa wanatumiwa na isitishe wamehongwa sasa kila kukicha wanaona lengo lao halitiimi inabidi waanze plani B. waliyoiandaa ya kuvuruga mchakato mzima wa Katiba.

Sikutegemea Lipumba awaka very low kiasi hicho kwa kuwaita wenzie interahamwe huku akijua fika kuwa Interahamwe ni kundi la kihutu lililoongoza mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.. Hivi ukiunganisha nukta hupati jibu Kagame alishawahi kumtusi Kikwete anawasaidi FDRL ambalo ni kundi la Kihutu lililohusika na Mauaji ya Kimbali. Kisa tu alitoa ushauri wazugumze.

Sasa Lipumba kaona bora atamke Interahamwe kwa sababu wimbo ni ule ule wa kuwaambia Watanzania wote Wanaopenda amani, umoja na muungano uendelee leo wamekuwa ni wenye chuki na wanaojiandaa na mauaji ya Kimbari. kama INTERAHAMWE.

KWELI KUWA MZEE SIO KIPIMO CHA HEKIMA.

Lipumba yuko sahihi sana..ccm ni chronic killers, nitawachukia daima walimuua dada angu mwenye ujauzito kule kwe2 Mtwara, Nyerere alimuua Kolimba, walimuua mjumbe wa tume ya Warioba wamekosakosa Dr.Ulimboka kwa uchache wake ni hayo maana orodha haitaisha.
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Malalamiko yako ni kuwa UKAWA wamekula posho au wameondoka bungeni??? Nani kahalalisha posho wanazoendelea kula hao walio baki bungeni wakati wanachi kijadili sicho tulicho watuma???? Jamani, mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni tu.
Naona aheri ya UKAWA kuliko Lukuvi kuendelea kuwa bungeni.
 
yaani ukawa kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious msirudi kabisa bungeni tena. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia mtatukuta barabarani. Karibuni sana!! Waacheni wanaotaka katiba ya tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa kutorudi tena bungeni. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha utoto mkubwa!

huna jipya nape siku hizi! Mnataka kulazimisha 2 iwe 4.
 
It is better to be unhappy and know the worst, than to be happy in a fool's paradise... Tafakari
 
mkuu hivi pale mnajadili nini?rasimu ya warioba au rasimu gani?maana kwa uelewa wangu ilitakiwa ijadiliwe rasimu ya warioba ambayo tumeigharamikia mabilioni kwa mabilioni kuipata, au nyie hamuoni uchungu na pesa zetu?
Anyway kwasababu hamlipi kodi hamuwezi kuwa na uchungu na hizo pesa, na ndio maana mmeanzisha yenu mnayoyajua. Mimi ni raia huru nisiye na chama lakini nakuambia walichofanya hao jamaa ni sahihi kabisa. Na kama nyie mna ubavu basi endeleeni kujadili hiyo katiba, tuone itakuwa katiba ya nani.. Mtaipata 2/3 ya kura kuipitisha?labda mchakachue kanuni kama ilivo kawaida yenu, otherwise......
Endeleeni na kikao cha kutengeneza katiba ya chama chenu....

kuna waliohama wakaenda nccr mageuzi na kurudi baada ya nyerere alipofariki. Sasa ndio waumini wakubwa wa baba wa taifa. Mmmmm?
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

MTOTO yeyote ana tabia ya kuzira akiona kama hajatendewa haki.hii tabia ikionyeshwa na mtu mzima inaonekana kuwa ni uzembe
mtu mzima hupigania haki yake na siyo kuzira.kwa mtu mzima kuzira huonekana kama KUGIVE UP.
Hawa UWAKA sijui UKAWA mi nawaona kama wanafiki wasio na nia ya kumkomboa mwananchi.
However mi naamini kuwa wakirudi watasamehewa na wananchi kuliko kukimbia.kufanya kosa siyo kosa bali kurudia kosa.Rudini mfanye kazi mliyotumwa na wananchi
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Thread yako hii inavutia kwa sababu jina lililotumika tunaliona majukwaani kila siku. Sijui kama ni Nape kweli maana ubora wa thread hii uko chini sana. Kama ni wewe kweli hukustahili kuja kwa mtindo wa matusi. Ungekuja kwa mtindo wa analysis ili tuchangie maoni yako na huenda kwa nafasi yako uyatumiye kukwepa uzembe uliofanywa na chama chako. Kuna uzembe wa hali ya juu sana umedekezwa ndani ya CCM. Uzembe wenyewe ni kukubali hata ujinga (ignorance) usikike hadhalani.

Hapo Bungeni kuna tatizo kubwa kabisa kwa mtu mwenye elimu na ufahamu. Kuna wabunge ambao kazi yao imekuwa ni kushangilia tu! Hawana muda wa kuangalia au kusikiliza ukweli. Hiyo siyo siasa na hiyo siyo nchi. Wazungumzaji wanawinda kushangiliwa tu na bahati nzuri wanafahamu washangiliaji wengi ni CCM kwa hiyo mtu anajisemeya hata matusi ili ashangiliwe na ndivyo inavyokuwa, watu wenu wa CCM wanashangilia hata matusi! Huu ni mkakati mbovu kabisa ktk siasa ndani ya bunge. Siasa tunaigiza seriousness lakini hapo bungeni tunaonyesha uzembe na kushangilia. Ni kweli hii ni nchi ya viwango duni kiasi hiki? Munaingiza watu bungeni kupiga vigelegele halafu munapongezana! Shame!

Hao UKAWA unaowasema siyo wapuuzi kiasi hicho. Binafsi siwaoni kwamba ni mashujaa lakini nawaona kama watu waliokwisha ona ni wapi tunaishia. Kwa nini uendelee na safari wakati unajua mbele hakuna matumaini.

Kama kweli wewe ni Nape lazima ufahamu mwisho wa katiba ni Kura ya maoni. Kura inayohitaji 2/3 majority, bara na visiwani. Huku bara najua itachakachuliwa, Z'bar haitawezekana na hiyo 2/3 haipatikani na katiba haipiti, kwa nini upoteze muda na mbinu za aina hii? Mara zote nawalaani CCM kwa kuwa ni chama kikubwa nchini lakini kinashindwa kutumia nguvu hiyo kutoa maamuzi au kutumia mbinu za kisomi/kielimu. Hata kama chama hakina wasomi wa aina hiyo bado kinaweza kuwaazima na wakakisaidia badala ya kutegemea kelele za vigelegele. Wapiga vigelegele hawajengi chama!
 
Ama hakika uvumilivu unahitajika sana kwenye mambo ya siasa,yaani unaona kabisa mtu anapotosha umma tena kwa makusudi lakini unalazimika kukaa nae safu moja bungeni ... this is wonderful!! Hakika uvumilivu ni tunu.
 
kwa Nape ni ngumu sana kukujibu

Mkuu, nimeona nikikupa like, haitoshi!!
Siyo Nnape tu hata hayo followers wake naona wanarukaruka kujibu post za mstari mmoja, hawataki kujibu kwa hoja!!

Wana CCM, fuateni ushauri wa mwenyekiti wenu, changanyeni na za kwenu, mbona mmebakiza za kamati kuu tu? plan A ilikuwa kutumia idadi kubwa ya wajumbe kupitisha maoni yenu, imeshindwa hiyo. wapi Plan B?

SP
 
Lisu katukana mpaka basi baada ya matusi kuisha wametoka kwenye bunge wakatafute matusi mengine.

Wewe ni mmoja wa watu wanaoamini waTZ wote tumezaliwa na Nyerere? hata siku moja. Nyerere alizaliwa lwake na ana watoto wake. FINITO!
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!
With due respect to your leadership position I advice you to restrain from using your own intuitions in issues which have remarkable concequences to our nation well being. You should know better that failure to exist(as is expected in parliament) with people with different views removes the basic cridential of a political democratic leader. In other words it is childsh to encourage constitution assembly without the opposing voice.(regardless of their number). I would expect a person of your position to be well adviced to know the importance of oposing voices and encourage the opposition to join back the ongoing debate. Opposing ideas in democratic system are its strength. Imposition of ideas equals dictatorship which is not a political option desired.
 
hawa jamaa kama hawana chembe ya unafki...waungane tu CUF+CDM+NCCR=2015 then Tanganyika will back kiulainiiiii.....!
 
Najisikia aibu kuchangia hoja dhaifu ya Kiongozi mkubwa wa chama,naona kama ni ukosefu wa nidhamu.
Napenda kukufahamisha Mh.Kiongozi mkubwa wa chama kuwa hao uliowaita "UWAKA" wanatetea rasimu halali ya Tume ya Warioba ambayo inaungwa mkono na Watanganyika/Wazanzibari wengi nje ya mjego kuliko unavyofikiria.Jaribu kufuatilia uone.
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!
Nape Nnauye wewe kwa umri mdogo lakini kwa mamlaka ni mtu mkubwa.Katibu wa Uenezi na itikadi wa CCM si mtu mdogo hata kidogo.
Naamini si sahihi kuingia na kujibu hivi ulivyojibu kwani ni wazi kabisa kuwa watu waliotoka katiak bunge wengi wanakuzidi akili,maarifa na hata uchambuzi wa mambo ya siasa lakini kwa kuwa madaraka hulevya tayari ushalewa na unaona UKAWA hawana hoja.
Wakati mwingine kwa cheo chako unatakiwa ku retreat na kutafakari kwa kina hoja zao na ikiwezekana kuangalia namna ya kuendelea mbele.
Naamini lengo la CCM si kupata katiba mpya na ndio maana mmemshambulia mno Warioba bila kujua ya kuwa alichaguliwa na mkubwa wetu wa nchi.
Je mkubwa wetu hakuona mapungufu ya Warioba katika utendaji mpaka akamwacha amalize kazi?
Mli invest a lot kwa hila katika mabaraza ya kata lakini wenye nia njema waliliona na pre emptive measure zikachukuliwa.
Jipangeni upya!!!!!!
 
Sioni kama kususa ni busara na
wanahoja za msingi, kwanini
hawakupinga tangu ile sheria
iliyoanzisha mchakato? Na
kwanini wamekaa hadi siku 60
ndo watoke? Je pesa waliotumia
na kisha wakasusa hawaoni
kama wanatuingiza hasara
wananchi? Hivi kama wanasusa
ni kwavipi watatutetea ka kweli
wanalengo hilo? This is totally
wrong dear Ukawa.

Wee nawe,si upeleke jukwaa la mashairi,huku umefuata nini?
 
:israel::rapture:Msishabikie kila kitu,walichokifanya UKAWA ni upuuzi mtupu,
Ivi kweli kama wanata katiba ya watanzania kwa nini mtoke na msiseme mnaenda kufanya nini?ni wahuni kwa kufanya matendo ya wahuni!
huko mmlipokwenda ndo mnaenda kujadili na kuandika katiba ya watanzania?ujinga huo watanzania tumewaona hamna maana ya katiba ya watanzania bali matakwa yenu ya kitoto!
Mlimnukuu sana Nyerere na kumsifia,Je Nyerere angekimbia wakoloni tungepata Uhuru?Jifunzeni vitu sio mnashawishiana kwa hoja za kike za kususa mambo!
Hi imedhihiri nyie ni wapotoshaji na mnalazimisha vitu kwa nguvu ya mwili na si akili!
Iweje hoja ya kwenye gazeti ndio mtumie kutoka nje?Nyie mnamapenzi na nchi hii nyie?
hata kidogo,Nyie ndio mmeonekana hamfai
R.I.P UKAWA-----Interahamwe WAKUBWA ndio NYIE
 
Wana jamvi
Naandika haya kwa sababu na amini kuna wajumbe wa UKAWA wanapita humu, na hili ni jukwaa la GT, hivyo kupata maoni mbalimbali
1. UKAWA wametoka nje, je wamesha ambia jamii lolote juu ya uamuzi huo, yaani baada ya kutoka nje wananchi watarajie nini?
2. je UKAWA wana plan B ya madai yao? nikisema hivyo naamnisha juu ya kauli ya waziri Lukuvi na maneno ya matusi ya wajumbe. mfano wakiambiwa lukuvi kajiuzuru uwaziri leo, na mwenyekiti amewaonya wajumbe UKAWA watarudi au watafanya nini?
3.je UKAWA wapo solid? kwa maana ya umoja na mshikamano imara ya kufanya maamuzi kwa pamoja, hivyo wananchi tuwa amini? kwa sababu wananchi tusio na vyama tunafaham na wafuasi wa vyama wanajua tofauti iliyopo kwenye vyama vya upinzani. na CCM wanaweza tumia hilo
4. lini watatueleza wananchi, madhumi na mpango wao, na matakwa yao ili waweze kurudi bungeni hiyo tarehe 24/4 au baada ya hapo?

maoni binafsi
Mosi, Kusimamisha bunge la katiba lisiendelee na vikao vyake, hii inaweza kwa kwenda mahakamani, au kwa njia yoyote iwezekanayo, yenye kufuata utaratibu na haki.
Pili, UKAWA wasirudi bungeni tena, jambo linalotakiwa kufanyika ni kupitishwa kwa refrendam, juu ya kama ni serikali 2 au 3, ili hilo liamuliwe na wananchi nje ya bunge, wakirudi huko aisiwepo mjumbe wa kusema wananchi wanataka 3 au 2, bali wanatakua wametoa yao.
Tatu, Endapo bunge litaendelea na wao wakiwa nje, waweleze wananchi kua wanasubiria kura ya rasimu, na hivyo muda wote huo watembee nchi nzima kuelezea katiba na mahitaji ya katiba mpya.

Nne, kama kuna wakati viongozi wa vyama vya upinzani walifikiria, kupigania mabadiliko, kuungana, kushirikiana au wana lengo la kuleta mabadiliko kwenye ardhi ya JMT hii ni nafasi yao kubwa sana ( once and for all). Endapo watashindwa kushikamana na kushirikiana kwenye hili, hakika yangu hawatapata nafasi nyingine na wala wananchi hawata waamini tena, kamwe, asilani!!. Hivyo viongozi waache vyama hadi katiba ipatikane ya wananchi. wawaunganishe watatnzania kwa umoja wao kwa wananchama wao na kwa wasio na vyama. Faida ni kubwa kwa wananchi, taifa na vyama kuliko majina na maslahi yao ndani ya vyama.

Naomba kuwasilisha

SP
 
Yaani UKAWA kwanini mmesubiri mpaka mmelipwa posho ndio mmetoka bungeni? Kwanini hamkutoka toka mwanzo? Huu ni utoto!

Lakini kama mko serious MSIRUDI KABISA BUNGENI TENA. Mlishatishia kwenda barabarani nikawaambia MTATUKUTA BARABARANI. Karibuni sana!! waacheni wanaotaka katiba ya Tanzania waendelee na bunge la katiba. Nawasihi muonyeshe seriousness kwa KUTORUDI TENA BUNGENI. Mkirudi mtakuwa mmeonyesha UTOTO MKUBWA!

Kinachosikitisha kwa viongozi wetu ni posho posho posho! Vichwa havifikiri zaidi ya posho.

Kwa cheo ulichonacho kutoa hoja ya posho inasikitisha kwa kweli. Hatuwezi kutarajia chochote cha maana kutoka kwao
 
Back
Top Bottom