Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,685
- 149,894
Nawashauri viongozi na wabunge wote wa UKAWA kuanza upya harakati za kudai Tume Huru ya Uchaguzi,haki ya kuwa na mgombea binafsi na haki ya kikatiba ya kupinga matokeo ya uraisi mahakamani.
Kwa akili ya kibinadamu,wengi wetu tunawaza uchaguzi ni 2020 na hatuwazi zaidi ya hapo.Huu ni mtazamo potofu kabisa kwani hakuna binadamu alieongea na mungu kujua kesho itakuaje hivyo ni bora kujiweka tayari wakati wowote.
Naamini hata katiba yetu inatambua uwepo wa dharura kama hizi na bila shala itakuwa imetoa fursa uchaguzi kufanyika katika mazingira hayo (sijasoma katiba yote lakini naamini katiba haiwezi kuwa kimya juu ya dharura kama hizi).
Isitoshe,UKAWA leo hii mko pamoja hivyo ni bora mkatumia umoja huu kudai mambo haya yatekelezwe sasa kwani si ajabu kesho na kesho kutwa mkawa mmesambaratika na hivyo mkajikuta nguvu mlionayo leo haipo tena maana katika siasa lolote pia laweza kutokea.
Vile vile msidhani adui yenu anapenda huu umoja wenu uendelee na zaidi hamjua anapinga nini ili msiendelee kuwa pamoja na msisahau kuwa nanyi ni binadamu ambao hamjakamilika hivyo kuna baadhi yenu wanaweza kabisa kurubuniwa.
Mwenye masikio na asikie.