brownjosephati
JF-Expert Member
- Jun 7, 2024
- 615
- 758
Kama ulikuwa hujui kuwa FREEMAN MBOWE jina lake alipewa na MWALIMU NYERERE, basi wacha nikufahamishe.
Watu wengi hudhani kuwa familia ya MBOWE na ile ya MWALIMU NYERERE ni maadui kwa sababu FREEMAN MBOWE ni mpinzani wa kisiasa.
Hili si kweli. Ukweli ni kwamba familia hizi mbili ni marafiki wa karibu sana—urafiki ambao ulianzia enzi za MWALIMU NYERERE na unaendelea hadi leo ninavyokuandikia makala hii.
Zimekuwa familia zinazoheshimiana sana. Na la kushangaza kwa wengi ni kwamba FREEMAN MBOWE humchukulia MWALIMU NYERERE kama baba yake.
Siyo tu kwa sababu MWALIMU ni BABA WA TAIFA, bali ni kutokana na urafiki wa karibu sana uliokuwepo kati ya baba yake FREEMAN MBOWE na MWALIMU NYERERE.
Mtu unayemuona kwenye picha akipeana mkono na MWALIMU NYERERE ni baba mzazi wa FREEMAN MBOWE. Anaitwa AIKAEL ALFAYO MBOWE. Picha hiyo ilipigwa mkoani Kilimanjaro wakati MWALIMU alikuwa ziarani huko.
Mzee AIKAEL alikuwa tajiri mkubwa mkoani Kilimanjaro na mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa kwa chama cha TANU.
Mzee AIKAEL ALFAYO MBOWE alihamasisha wananchi wa Arusha na Kilimanjaro wakiwemo machifu kujiunga na TANU. Kwa kifupi, alikuwa mmoja wa wapigania uhuru wakubwa hapa nchini. Kutokana na mchango huo, MWALIMU NYERERE alimpenda sana na hatimaye wakawa marafiki wa karibu sana.
Urafiki wao ulikuwa wa dhati kiasi kwamba mzee AIKAEL aliweza kufika IKULU muda wowote aliotaka, kumuona na kuzungumza na MWALIMU NYERERE.
Mzee huyu ndiye mtu aliyekwenda IKULU mara nyingi zaidi ya wazee wengine enzi za utawala wa NYERERE. Na mara nyingi aliambatana na mwanawe, FREEMAN MBOWE.
Hapo ndipo dhana ilipozaliwa kuwa FREEMAN MBOWE amelewa IKULU kwa sababu alizoea kuingia IKULU tangu akiwa mtoto mdogo. Urafiki huo mkubwa pia ulipelekea familia hizi mbili kuwa karibu hata zaidi.
Ukaribu huu unaonekana pia katika maisha ya MAKONGORO NYERERE na FREEMAN MBOWE, waliocheza pamoja mara nyingi wakiwa watoto. Mwaka 1983, MAKONGORO NYERERE alipoamua kuoa, alimkabidhi barua ya posa kwa mzee AIKAEL ALFAYO MBOWE rafiki wa karibu wa baba yake.
Hivyo basi, mzee MBOWE akawa mshenga katika ndoa hiyo, kwa ombi maalum la MWALIMU NYERERE.
Ndoa hiyo ya MAKONGORO NYERERE na AISHA ilifungwa rasmi, na leo hii mkewe ni Jaji kitaaluma.
Na jambo lingine la kuvutia: wakati FREEMAN MBOWE anabatizwa tarehe 9 Desemba 1961—siku ambayo Tanzania ilipata uhuru baba wa ubatizo wake hakuwa mwingine bali ni MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE. Na jina "FREEMAN" alipewa na MWALIMU mwenyewe.
Makala hii imeletwa kwenu ✍️✍️