Sitachoka
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 3,030
- 1,303
Dodoma. Kiasi cha Sh8.2 bilioni kimetumika kufanya ukarabati mkubwa wa Ukumbi wa Bunge pamoja na miundombinu yake kwa ajili ya shughuli za Bunge la Katiba litakalokutana kwa zaidi ya siku 70.
Mbali ya gharama hizo, imeelezwa pia kuwa kila mbunge wa Bunge hilo maalumu la Katiba atalipwa Sh300,000 kwa siku katika kipindi chote litakapokuwa linakutana.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah aliwaambia waandishi habari Mjini Dodoma jana kuwa posho hizo za wabunge zimechanganuliwa katika sehemu mbili.
Alisema Sh220,000 ni kwa ajili ya posho ya kikao, usafiri na dereva na Sh80,000 ni posho ya kujikimu na kwamba hicho ndicho kiwango kilichoidhinishwa na Rais Jakaya Kikwete.
"Tuliposikia kuwa wabunge watalipwa posho ya Sh700,000 kwa siku na sisi hatukujua ilitokea wapi kwa sababu Rais hakuidhinisha malipo ya aina hiyo," alisema Dk Kashililah.
Gharama za ukarabati
Kuhusu ukarabati wa ukumbi na miundombinu yake iliyogharimu Sh8.2 bilioni, Dk Kashililah alisema viti vipya 678 vilivyofungwa kwenye ukumbi huo vimegharimu takribani Dola za Marekani milioni moja (sawa na Sh1.6 bilioni) pamoja na gharama za usafiri.
Alisema gharama nyingine zimetokana na marekebisho ya mfumo wa sauti ambao ulikuwa ukilalamikiwa na wabunge kutokana na kutosikika vizuri kwa baadhi ya vipaza sauti.
Dk Kashililah alisema ukarabati huo umehusisha, mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijiti na kuboresha mitambo ya Idara ya Kuhifadhia ya Kumbukumbu Rasmi za Bunge ili iweze kuhimili idadi ya wabunge hao zaidi ya 600.
Alisema gharama nyingine zimetokana na ukarabati wa mifumo ya kuimarisha usalama pamoja na kuweka vioo visivyopenya risasi katika baadhi ya kumbi.
Alisema fedha nyingine zimetumika kukarabati paa la Ukumbi wa Bunge ambalo lilikuwa linavuja.
Pia fedha hizo zimetumika kurekebisha mitambo ya kufua umeme, maji, kuzima moto na viyoyozi na kumalizia ujenzi wa jengo ambalo litakuwa likitumika kwa ajili ya sehemu ya mazoezi, benki na ofisi za wabunge zaidi 100.
Dk Kashililah alisema kiasi hicho kimetumika kwa ajili ya kununua samani za ofisi za wabunge na kuongeza eneo la mgawaha na kuboresha miundombinu kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Alisema fedha zote zilizotumika katika ukarabati huo zimetokana na bajeti ya mipango ya maendeleo iliyopitishwa na Bunge mwaka jana na kwamba si jambo geni huku akisema kazi zote zimefanywa kwa mara moja.
Ratiba ya Bunge la Katiba
Kwa upande wa ratiba ya Bunge la Katiba, Dk Kashililah alisema litaanza shughuli zake rasmi kesho kwa kusomwa kwa tangazo la kuitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Siku hiyo pia kutafanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa muda ambaye kazi yake kubwa itakuwa ni kuandaa kanuni za Bunge Maalumu la Katiba ambalo litakuwa na wajumbe 629.
Alisema baada ya kupatikana kwa kanuni, Ijumaa kutafanyika uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake kwa kuzingatia sheria ya Mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa mwaka jana.
Alidokeza kwa kusema pia kuwa wateuliwa, Katibu na msaidizi wake wa Bunge hilo na kwa mujibu sheria hiyo, ataanza kazi baada ya kuapishwa na Rais na baada ya kuapishwa naye atamwapisha mwenyekiti wa Bunge hilo.
Baada ya mwenyekiti kuapishwa, atawalisha kiapo wajumbe wengine wa Bunge hilo, kazi ambayo itafanyika kwa siku tatu hadi Jumatatu asubuhi na mchana wake, Rais Kikwete atalizindua rasmi.
Chanzo:Mwananchi