Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo

Ukarabati kichekesho Rusahunga - Rusumo

Mabibi na mabwana kipindi cha kampeni ndiyo hiki. Wapo wanaojinasibu na ubora wa miundombinu waliyojenga nchi nzima.

Labda kama ni miundombinu kiini macho!

Hivi karibuni baada ya kelele za kutosha waziri wa wizara husika japo bunge lilishavunjwa aliwahi mbio mbio kabla ya hatari:

Kabla ya Lissu, Waziri wa Ujenzi atembelea barabara ya Rusahunga - Rusumo

Baadaye akafuatiwa na katibu mkuu wa wizara husika. Huyu pamoja na kukiri aibu iliyokuwapo kuhusiana na hali ya barabara hii, aliagiza kazi ya usiku na mchana 12Bn/- zikiwa zimetolewa kwa ajili ya kipande hiki cha 92km.

Kufuatia hatua hizi pichani ni kichekesho cha millenia. Hakuna kazi kazi ya usiku na mchana. Kama kazi hii inahusisha 12Bn/- ambazo zimeshatolewa, labda kama ni upigaji mwingine tu:

View attachment 1556644

View attachment 1556647

View attachment 1556648

View attachment 1556657

View attachment 1556685
View attachment 1556657

View attachment 1556745

View attachment 1556644

Ikumbukwe kuwa Dodoma wadogo waliahidiwa 112km kwa 112Bn/- kwa ajili ya kupendezesha jiji ili wamchague mgombea wa chama pendwa!
Inayojenga halo ni mayanga. Wanazuga tu pesa yote imeenda chato
 
Tatizo ni Engineer au tatizo ni Ufisadi? Maana hata kama design imefanyika vizuri, watu wakitaka kupiga lazima walipue kazi ili wabaki na chenji ya kutosha. On the other hand, hizo picha hazimaanishi kwa kazi ndio inaishia kujaza hayo mashimo pekee, kuna hatua zingine zinaweza kufuata hadi kufikia hatua ya mwisho ya kuweka changarawe, ila si lami. maana lami ni around bilioni 1 per kilometer,so labda wangetenga around 92bn tungeweza kuwa na matumaini
 
Hii barabara ni inachangia pato kubwa kwa taifa kuliko uwanja wa ndege uliojengwa chato.
 
Yaani maendeleo ya nchi yanapimwa na maendeleo ya DAR ES SALAAM...... KITUKO CHA MWAKA HIKI.
DAR KUKIJENGWA FLY OVER NCHI NZIMA INAAMBIWA IFURAHI KISA FOLENI IMEPUNGUA.... NONSENSE how does it help us tulio huku maporini
Kwa sababu Dar ndo inachangia zaidi ya 70% ya kipato cha nchi nzima kwa kifupi hata hivyo visima mlivyoahidiwa kuchimbiwa mostly ni kipato toka Dar na pia Dar soko la hao kuku unaofuga,mahindi unayolima huko bush ...so relax Dar ndo Tz Tz ndo Dar,nyie subirini visima na umeme wa rea unawatosha
 
Dar ndiko yaliko madini ya nchi hii, kilipo kilimo cha mazao ya chakula na biashara, vivutio vyote vya utalii, uvuvi wote unaopelekea biashara yote ya minofu ya samaki, mazao yote ya misitu, kunapozalishwa gesi, umeme hata maji ya kunywa?

Uchumi wa nchi hii chimbuko lake ni Dar es Salaam?

Hivi unazijua takwimu za uchumi wa nchi hii wewe? Au ni ubingwa wa kuandika utopolo tu?

Ulichoandika jombi ni kuonyesha tu ujinga wako uliopitiliza.
 
Tatizo ni Engineer au tatizo ni Ufisadi? Maana hata kama design imefanyika vizuri, watu wakitaka kupiga lazima walipue kazi ili wabaki na chenji ya kutosha. On the other hand, hizo picha hazimaanishi kwa kazi ndio inaishia kujaza hayo mashimo pekee, kuna hatua zingine zinaweza kufuata hadi kufikia hatua ya mwisho ya kuweka changarawe, ila si lami. maana lami ni around bilioni 1 per kilometer,so labda wangetenga around 92bn tungeweza kuwa na matumaini

Be informed hakuna hatua yoyote iliyofuata baada ya hiyo kazi. 12Bn/- disappeared in thin air.
 
Back
Top Bottom