G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,558
- 35,887
Mtu mmoja ameuawa asubuhi hii na wengine wawili kufanikiwa kutoroka baada ya kujaribu kumteka mgombea udiwani wa kata ya Bwisha Ukara kwa tiketi ya CHADEMA.
Inadaiwa watu hao wamezingirwa baada ya mgombea huyo kupiga ukunga na ndipo walipozingirwa na kushushiwa kipigo ambapo mmoja ameuawa huku wawili wakifanikiwa kutoroka.
Hilo ni tukio la kwanza la mauaji yanayohusishwa na mambo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo kunatabiriwa kuwepo kwa visa vingi vya vurugu kutokana na sintofahamu ambazo zimeanza kujitokeza.
Habari hii imethibitishwa na Katibu wa kanda ya Victoria- CHADEMA ndugu Zacharia T. Obad