Ukali na tishio kutumia nguvu wanavyofanya Raisi Samia na Mchengerwa "kulinda" amani ya Tanzania ni vigumu sana mtu kuamini Tanzania ni nchi ya amani!

Ukali na tishio kutumia nguvu wanavyofanya Raisi Samia na Mchengerwa "kulinda" amani ya Tanzania ni vigumu sana mtu kuamini Tanzania ni nchi ya amani!

JPM alisingiziwa mabaya mengi sana
Nani muasisi wa haya yote?? Nani aliyeanzisha kikosi kazi cha kuteka kuua na kubambikia wapinzani wao kesi??

Mwanzo Hangaya alijitenga na kundi lile. Akaanza kuhujumiwa na kundi lile. Wazee wa Chama wakamuambia ili uweze kutawala bila vikwazo basi rudisha lile kundi kazini.

Kajifanya chura kiziwi lkn mwisho madaraka yakamlevya. Akaamua kulirejesha kundi lile kazini ingawa sio wote. Upande ule wa kuwabambikizia Wafanyabiashara kesi bado linataabika.
 
Unasema hv kwakuwa ww n mwananchi wa kawaida mtaani tuu na huna fursa fulani kama hao viongozi wa juu, ila ungekuwa rais au level yoyote hapo juu usingesema haya.

Jiulize, hao Marais wote, je kuna rais gn amepita bila kusikia jambo baya?
Enzi za JK watu wamenyooshwa, JPM Ndo moto kabisa, mama nae anapiga kwenye mshono.

JPM alisema wazi kuwa anataka upinzani wa kweli maana alijua wazi kuwa walikua wanapewa rushwa kubwa na yeye alikua hataki siasa za rushwa .
Lakini pia alikua mkali kwa kila mtu amayewaonea au kula mali za umma na alilinda rasilimali za nchi kwa nguvu zote mpaka kifo .
Hawa madalali hawana hata maoni na nchi hii . Asilimia kubwa ni wageni tu kuanzia teuzi zao . Hivi umemsikia nani amehojiwa kwenye ripoti ya CAG ?

Makusanyo ni mangi sana leo kuliko wakati wowote tangu tupate uhuru . Pesa zimakwenda wapi? tunaona zaidi waliopo juu wanaojilimbikizia mali bila hata kuulizwa wakati kuna tume ya maadili na TAKUKURU . Sasa mtu kama huyo hawezi kuwa na kibali cha kutumia nguvu watu wamwelewe .

Na haiwezekani tukaendelea tu na Mbinu ile ile ya Mkapa sijui Kikwete sijui Magufuli miaka yote .
Dunia ina mmiliki halisi ambaye ameumba kwa malengo yake ndio maana samia ana roho moja kama watu wengine na anahofu na huzuni pamoja na mali nyingi alizojiwekea lakini bado hawezi akishi miaka mia mbili . Walioishi sana nao pia waliondoka kwa sababu madaraka yao hayaondoi kusudi la Mungu.

Dunia ilitoka kwenye vipindi vingi vizuri na vibaya lakini havikudumu . Kibaya zaidi lilikua ni utumwa lakini haukudumu kwa sababu ya teknolojia . Kwa hiyo ipo siku watu wataweka maandamano ya Maroboti yatakayojibu mapigo kwa watakaojaribu kuyazuia . Hapo ndipo wanasami wataheshimu uhai wa watu kuliko vyeo na Mungu atabaki kuwa mkuu kuliko watawala .

Leo Samia kwa katiba tuliyo nayo ni mkuu kuliko Mungu aliyemuumba yeye na kila kitu . Anajisikia yupo juu ya nafsi za watu na hata rasilimali alizoumba Mungu ni za kwake na familia yake anapanga tu ampe nani anayemtaka na amnyime nani asiyetaka na hata kuondo uhai wa mtu yeyote bila kuulizwa na yeyote na kuogopa chochote maana hata Mungu anayetajwa kwenye dini anasema asimwaingilie .

Tawala za namna hiyo haziwezi kudumu milele mana hata shetani kiburi ndicho kilichomwondolea nafasi yake kubwa .

Samia atadondoka wakati asioutarajia na hatapata wa kumsikiliza .
Maana akikosa madaraka hata wale mashehe wanaomsifia hawatakuwa naye kamwe . Hata pata upendeleo kwenye nyumba za ibada Kwa sababu watamuona kama mtu aliyekaa damu za watu .
 
Ifike mahala vyombo vya dola na taasisi za usalama ziache kupokea tu amri dhidi ya wananchi wanaopaswa kulindwa.

Vyombo vya usalama vianze kuchuja mambo na kutoa kuonya kwa wahusika juu ya amri wazitoazo.
Tatizo jeshini sio rahisi. Ila wanapolaumiwa ni kwamba wanavyopiga watu, wandishi, wapita njia nk, hayo sio maelezo wanayopewa. Wanafanya hivyo kujipendekeza
 
Hakuna jeshi la UN

Kule Koo ongo na Sudana na hata hapa Tanzania hukawaona wakiwa na vifaru vilivyoandikwa UN?

UN inategemea mgongo wa Marekani na nchi za Ulaya kuvamia nchi yoyote wanayotaka . Na Tanzania ni dakika moja maana ndio nchi bikra iliyobaki yenye Rasilimali nyingi . Wanavamia na kuipiga kwa shinikizo la Marekani na washirika wake kisha vifaru vya UN vinasambaa mitaani kulinda wapotaji wa rasilimali zetu .
 
Unataka tuanze kusema tuchukue silaha? Kama ingekuwa ni kuchukua silaha kupambana na CCM na jeshi lao la polisi, huenda hata mie ningefanya hivyo. Lakini ukichukua silaha unawachokoza tu JWTZ ambao hawana kosa katika yote haya, lakini itabidi wao ndio watumwe kukabiliana na wewe, na itabidi watii amri ya Amri Jeshi Mkuu. Ila uwezo wa kuzuia nchi kufika huko uko mikononi mwao.

Jeshi la wananchi katika watu wanaowachukia namba moja ni Polisi .

Wanajua wazi kuwa polisi wanaonea sana watu .
Hivyo siku wakiingia mtaani ujue Watawapimzisha polisi na CCM na mafisadi wote na nchi itarejea kwa wananchi .

Jeshi likiingia mitaani ujua mpaka polisi watakungutwa Mikanda mpaka hali itulie na wananchi wakiwaona wanajeshi watawashangilia kwa furaha na CCM haitakuwepo tena .

Kenya wanajeshi walikaa mbali .

Katika watu wanaofuatilia sana saisa ni wanajeshi tofauti na polisi ambapo hawaelewi hata maana ya Demokrasia na sera za vyama hawana habari nazo . Wanajua ni CCM tu inaongoza bila kujua kuwa kuna uchaguzi unawapa watu mdaraka kwa kura .
 
Awamu iliyojaa viongozi vilaza wasio na uwezo ni hii aise, huyo nae eti ni kiongozi...Ila hii nchi aise shamba la bibi.
 
Jeshi la wananchi katika watu wanaowachukia namba moja ni Polisi .

Wanajua wazi kuwa polisi wanaonea sana watu .
Hivyo siku wakiingia mtaani ujue Watawapimzisha polisi na CCM na mafisadi wote na nchi itarejea kwa wananchi .

Jeshi likiingia mitaani ujua mpaka polisi watakungutwa Mikanda mpaka hali itulie na wananchi wakiwaona wanajeshi watawashangilia kwa furaha na CCM haitakuwepo tena .

Kenya wanajeshi walikaa mbali .

Katika watu wanaofuatilia sana saisa ni wanajeshi tofauti na polisi ambapo hawaelewi hata maana ya Demokrasia na sera za vyama hawana habari nazo . Wanajua ni CCM tu inaongoza bila kujua kuwa kuna uchaguzi unawapa watu mdaraka kwa kura .
Katika vitu ninavyotamani kutokea nchini ni JWTZ kuchukua nchiili tuanze upya.

Tuanze upya, na tusahau mambo ya CCM, Chadema , ACT wazalendo sijui nk. Tuanze upya kwamba Tanzania tutaruhusu vyama vinnn tu vya siasa, na vilivypo vyote viwe disbanded.

Tuanze upya JWTZ wasimamie nchi kwa miaka miwili wakati tukiandaa Katiba mpya, na mali zote za CCM na vyama vingine kurudishwa serikalini.

Tuanze upya kwa masharti kwamba katika vyama vipya vitakavyojitokeza haviruhusiwi kuwa na asilimia zaidi ya 20% ya wanachama wa zamani wanaotoka chama kimoja

Tuanze upya kwamba hata kama Raisi, Makamu wa raisi spika nk hawawezi kufunguliwa mashitaka kwa sasa, haitatuzuia kuunda tume kuchunguza ufisadi na ukosefu wa haki za binadamu waliofanya ili japo hawatafungwa wapigwe marufuku kujihusisha na siasa, au kutaifishwa mali zao za ufisadi

Tuanze upya kwamba tukianza upya hakuna mtu atakaekuwa juu ya sheria, hataraisi anaweza kushitakiwa na kufungwa akipatikana na hatia, awe madarakani au amemaliza muda wake
 
B
Kule Koo ongo na Sudana na hata hapa Tanzania hukawaona wakiwa na vifaru vilivyoandikwa UN?

UN inategemea mgongo wa Marekani na nchi za Ulaya kuvamia nchi yoyote wanayotaka . Na Tanzania ni dakika moja maana ndio nchi bikra iliyobaki yenye Rasilimali nyingi . Wanavamia na kuipiga kwa shinikizo la Marekani na washirika wake kisha vifaru vya UN vinasambaa mitaani kulinda wapotaji wa rasilimali zetu .
Bado hakuna Jeshi la UN.
Kwa muktadha wa hoja yako, Katiba ya Tanzania haijakataza Amiri jeshi kudeploy TPDF ndani ya Tanzania.

Hivyo wanaweza kuwa deployed kama ilivyotokea kule Mtwara kipindi Cha gesi, Korosho, Tanga Handeni.

Jeshi halipo loyal kwa Wananchi Bali Amiri jeshi hata kiapo Chao kipo hivyo.

Halafu mkuu hizi mnazoandika sio vitu vizuri.
Tanzania ni amani na amani ni Tanzania
 
Nimewasikiliza Raisi Samia na waziri wake Mchengerwa wakiongea kuhusu "kulinda" amani ya Tanzania, kwa namna ya ukali na kuonyesha watatumia nguvu kubwa kuilinda hiyo "amani", kiasi kwamba najiuliza, kama Tanzania ni nchi ya amani, kwa nini muongee kwa ukali namna hii na kutoa vitisho vya ajabu kiasi hicho kwa watu wanaoishi ndani ya nchi ya amani?

Huko Mbeya Mchengerwa ameongea kama yeye ndio Raisi wa Tanzania, mabavu, na vitisho utafikiri yeye ndioanaamrisha majeshi ya Tanzania

Ni wazi kama Tanzania ni nchi ya amani, na kuna tatizo au jambo limejitokeza, basi utatumia njia za amani kushughulikia mambo yanayoletwa mezani. Kwa nini utumie ukali na kutishia watu kwamba watakiona cha mtema kuni ikiwa unatambua kwamba hao watu ni sehemu ya nchi yenye amani?

Ni wazi basi ni nani hapa anaetaka kuondoa amani ambayo Watanzania tumeizoea sana nchini. Iweze Raisi Samia katika nchi ya amani anawaambia JWTZ wajiandae na mapambano wakati wa uchaguzi? Tanzania nchi ya amani unawaambia JWTZ wakae tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu? Kupambana na nani, wananchi? JWTZ Vs WTZ?

Katika nyumba yenye amani, ikitokea mtu mmoja analeta jambo, hata kama hulipendi au anatumia njia usizopenda kuliwakilisha, wewe mwenye kutambua thamani ya amani utashughulikia hilo jambo kwa amani, la sivyo wewe unaweza kuwa mbaya kuliko huyo mtu unaemtuhumu kuwa anatishia amani.


View: https://www.youtube.com/watch?v=mxArtpEEGng


View attachment 3317549

Tanzania ina amani tele kbs ila haina haki tu, hapo wanaenda na bosheni la kutunza aman ili ku brainwash watanzania!!
 
Back
Top Bottom