Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Nimewasikiliza Raisi Samia na waziri wake Mchengerwa wakiongea kuhusu "kulinda" amani ya Tanzania, kwa namna ya ukali na kuonyesha watatumia nguvu kubwa kuilinda hiyo "amani", kiasi kwamba najiuliza, kama Tanzania ni nchi ya amani, kwa nini muongee kwa ukali namna hii na kutoa vitisho vya ajabu kiasi hicho kwa watu wanaoishi ndani ya nchi ya amani?
Huko Mbeya Mchengerwa ameongea kama yeye ndio Raisi wa Tanzania, mabavu, na vitisho utafikiri yeye ndioanaamrisha majeshi ya Tanzania
Ni wazi kama Tanzania ni nchi ya amani, na kuna tatizo au jambo limejitokeza, basi utatumia njia za amani kushughulikia mambo yanayoletwa mezani. Kwa nini utumie ukali na kutishia watu kwamba watakiona cha mtema kuni ikiwa unatambua kwamba hao watu ni sehemu ya nchi yenye amani?
Ni wazi basi ni nani hapa anaetaka kuondoa amani ambayo Watanzania tumeizoea sana nchini. Iweze Raisi Samia katika nchi ya amani anawaambia JWTZ wajiandae na mapambano wakati wa uchaguzi? Tanzania nchi ya amani unawaambia JWTZ wakae tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu? Kupambana na nani, wananchi? JWTZ Vs WTZ?
Katika nyumba yenye amani, ikitokea mtu mmoja analeta jambo, hata kama hulipendi au anatumia njia usizopenda kuliwakilisha, wewe mwenye kutambua thamani ya amani utashughulikia hilo jambo kwa amani, la sivyo wewe unaweza kuwa mbaya kuliko huyo mtu unaemtuhumu kuwa anatishia amani.
View: https://www.youtube.com/watch?v=mxArtpEEGng