Mkuu JokaKuu,
Ukomavu wa kisiasa pale mtu anapokuwa jukwaani au kwenye mihadhara ni pamoja uchaguzi wa maneno ya kutumia katika hotuba zake.
Mheshimiwa Zitto sina uhakika kama ana "hard copy" ya anachokizungumza majukwaani na hasa yake
aliyoyasema pale Mbagala, maana wenzie anaoongozana nao wanafanya hivyo.
Atumie walau muda kupitia hotuba au maoni yake kwani yamejaa jazba na maneno ya kashfa.
Hata kama amesema raisi JPM alikwenda Rwanda kwa Kagame kujifunza kubinya demokrasia, lakini nina uhakika wa 100% angesema maneno yake kule Kigali leo hii angekuwa kizuizini.
Hivyo ukimya wa raisi JPM haumaanishi kwamba watu watumie maneno ya kashfa kwa kiongozi wa nchi alie madarakani.