'ukabila', 'utamaduni' na ndoa . . .

'ukabila', 'utamaduni' na ndoa . . .

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
35,987
Reaction score
24,234
Samahani kama nitakuwa nimerudia mada.

Najaribu kuangalia, je kuna umuhimu wa kuoana watu wa kabila moja ama tamaduni zinazoshabihiana?

Kuna migogoro mingine katika ndoa huchangiwa tu na kuwa watu wa tamaduni tofauti hivyo kutafsiri jambo tofauti na mweza wako.

Wakati nakua, kuna siku walikuja wageni 14 at per mida ya jioni, nakumbuka bi mkubwa kapika ndizi zake akaleta mezani. Wageni wakala afu wakakaa kusubiri 'main course' baada ya 'stater' ya ndizi nyama. Sikuwahi muona bi. Mkubwa kakasirika vile. Anyway kwa wasukuma wa enzi zile ndizi si chakula cha watu kula wakapanda kitandani.

Kuna wakati niliishi Kagera, siku moja nikiwa bize na shuguli zangu nikaanza kupiga mluzi huku niko vere bize. Kuna mama mmoja alini-attack kama nimekula mbuzi wa kafara, sikumwelewa kwa kweli. Wakati nilikotoka ni sawa kupiga mluzi mwanamke kwa mwanamme. Tena inaweza kuwa advantage kuwa huyu mwanamke ni mchapakazi anaweza kufanya kazi na mbwa. Kumbuka mfugaji hakosi mbwa asilani kwa kule kwa BK ilionekana nimevunja mwiko, je ningefanya hivyo mbele za wakwe? Si ingekuwa talaka 3?

Kuna uzi pia namuona Snipper alalalamika mkewe hamkaribishi maji ya kuoga, labda wametoka makabila tofauti ama tamaduni tofauti.

Kuna mitafaruku mingine huchochewa tu na tofauti za makabila. Mfano kuna makabila ambayo mtoto ni wa mama na mengine mtoto ni wa baba. Au kuna makabila wanaabudu tabia za kiume zaidi 'masculine'na zile za kike huonekana weak.

Najua kuna ndoa za watu wa kabila moja au utamaduni zimevunjika, lakini natamani kujua nafasi ya kabila/utamaduni tofauti katika mitafaruku ya ndoa.

Na kama kabila/utamaduni vina nafasi

Je, ni busara kurudi katika kabila au utamaduni unaoulewa kupata mwenza?

Je, wazee wetu waliona mbali ku-insist watu waoe kwenye makabila yao?
 
Last edited by a moderator:
Dah!Zombie anataka kuchukua jumla sasa . . . .Lol!
'
Back to topic . . . . Kimsingi kila jambo lina faida na hasara,ila mambo ya tamaduni naona siku hizi yamekosa nguvu
'
Zamani yalikua na nguvu kwa kuwa watu waliishi kikabila zaidi ya sasa
'
Siku hizi kama mkeo/mmeo hajui taratibu za kabila lenu unamuelekeza wakati mnaenda kwa wazee
'
Muda huo ni muhimu kwa kuwa mnaenda kijijini,baada ya hapo hakuna tena mambo ya utamaduni,wote mnaishi kimjinimjini!
 
Nikisema utamaduni simaanishi kuvaa lubega

Ni yale mambo madogo madogo.

Mfano: unakuta mtu kakulia katika mazingira ambayo ni kawaida mme akiwa mita 20 kutoka nyumbani na mkewe, kusalimiwa na kupigiwa goti, kuwekewa maji ya kuoga, kuwa mwanamme ni msemaji wa mwisho katika kaya.

Unakutana na mke wa tamaduni tofauti ambaye hawezzi kufanya hayo.

Au mfano extended family, kuna makabila ni mabingwa wa extended, ukiishi na mtu aliyezoea familia ndogo yaweza kuwa mwanzo wa kununiwa kila siku.

Au kuna makabila mahari inatolewa kwa wajomba, akikutana na mkurya si kitawaka moto? Tena binti awe mweupe katolewa ngombe 30?

Au nafasi ya mwanamme anayemzalisha mwanamke aliyeolewa kwenye nyumba ntobo, kama ni wa kabila/tamaduni tofauti patakalika hapo kweli?

Hata kama mnakaa mjini, maamuzi ya maisha ya kila siku yana-reflect makuzi yetu ambayo kwa kiasi kikubwa nafasi ya utamaduni wa kabila umo ndani yake.

Dah!Zombie anataka kuchukua jumla sasa . . . .Lol!
'
Back to topic . . . . Kimsingi kila jambo lina faida na hasara,ila mambo ya tamaduni naona siku hizi yamekosa nguvu
'
Zamani yalikua na nguvu kwa kuwa watu waliishi kikabila zaidi ya sasa
'
Siku hizi kama mkeo/mmeo hajui taratibu za kabila lenu unamuelekeza wakati mnaenda kwa wazee
'
Muda huo ni muhimu kwa kuwa mnaenda kijijini,baada ya hapo hakuna tena mambo ya utamaduni,wote mnaishi kimjinimjini!
 
Ndoa ni utamaduni na zao la utamaduni; ni vizuri INGAWA si muhimu ukaoa mwanamke ambae mnalingana utamaduni ( yaani kabila moja au makabila karibu, jirani, rafiki, n.k). Hii inafaida moja kubwa kwamba WOTE MNAFAHAMU nini kintakiwa kufanyika kwenu wakati wa raha, shida, kutoelewana, etc) Hili linapunguza unnecessary conflicts/misunderstanding...Utamadunu hapa nauchukuliwa katika level ya juu kuliko UKABILA. Ndio maana unashauriwa kuoa mwanamke/mwanamme unaemfahamu vizuri sio historia yake tu bali na hata mambo yote yanayomzunguka kama binadamu.
 
Jambo la muhimu ni kuishi kulingana na nyakati na mazingira
'
Kongosho ngoja nikuambie kitu,mfano leo ukaolewa na Mchina what would u do?
'
Wakwe zako wanajua wewe ni Mwafrika na wakwe wa mumeo nao wanajua mumeo si Mwafrika
'
Hapa ni lazima kila mmoja aelewe na aukubali utofauti uliopo baina yenu
'
Dunia ya leo ina muingiliano wa makabila na jamii tofauti,kama una oa/olewa kwenye kabila jamii tofauti ya yako ni jukumu lako kulitambua hilo
'
Ujifunze tamaduni walau kidogo za mwenzako nae ajifunze zako na muishi mkizingatia tofauti hizo
'
Unaweza kuwa kikwenu ni lazima mume awe anachukuliwa kama mfalme katika familia,halafu umeoa mwanamke aliyekulia Milborne halafu ulazimishe afanye kama mila zenu wakati kwa mujibu wa makuzi yake huo ni unyanyasaji
'
Mazingira yamebadilika sana hayaruhusu uishi kikwenu sana,kama mtu anataka aishi kikwao asije mjini
'
Maana ukija mjini utafanya kazi na "makabila",utapanga nyumba nao,wataoa wanao n.k
'
Cha msingi ni kubadilika ili uweze kuishi na jamii tofauti tofauti!
 
Last edited by a moderator:
The Boss ,jambo linaweza kuwa la muhimu lakini lisiwe la lazima
'
Mfano;kuvaa viatu ni muhimu lakini sio lazima kwani unaweza usiwe na viatu na maisha yakaenda
'
Lakini jambo ambalo ni lazima ni la muhimu pia
'
Mfano;kunywa maji ni lazima na ni muhimu pia,huwezi kukosa maji na maisha yakaendelea
'
Pia usahihi na umuhimu hauna tofauti sana katika matumizi
'
Kwani jambo linaweza kuwa sahihi na likawa la muhimu pia and vise versa!
'
Nadhani kwa kiswahili changu cha std 7 ni hivyo!
 
Last edited by a moderator:
Ndoa ni utamaduni na zao la utamaduni; ni vizuri INGAWA si muhimu ukaoa mwanamke ambae mnalingana utamaduni ( yaani kabila moja au makabila karibu, jirani, rafiki, n.k). Hii inafaida moja kubwa kwamba WOTE MNAFAHAMU nini kintakiwa kufanyika kwenu wakati wa raha, shida, kutoelewana, etc) Hili linapunguza unnecessary conflicts/misunderstanding...Utamadunu hapa nauchukuliwa katika level ya juu kuliko UKABILA. Ndio maana unashauriwa kuoa mwanamke/mwanamme unaemfahamu vizuri sio historia yake tu bali na hata mambo yote yanayomzunguka kama binadamu.

Utamaduni hutoka kwenye kabila,ukikuta kabila tofauti na utamaduni nao hua tofauti!
 
Utamaduni hutoka kwenye kabila,ukikuta kabila tofauti na utamaduni nao hua tofauti!

Soma vizuri sijakataa, nilichosisitiza ni kwamba utamaduni ni zaidi ya kabila: Ndio maana kuna wengine wanaweza mbali sana wakasema kwa mfano UTAMADUNI WA WAAFRIKA, UTAMADUNI WA WAZUNGU...Kabila linabaki kuwa muhimu..
 
Chalenji huja tu pale mnapooana Taifa moja na lingine mfano Wewe Mwafrika uolewe/uoe Mwingereza hapo ndipo changamoto zinakuwa nyingi.
lakini kuoana M'bongo kwa m'bongo fine tuu changamoto za kitamaduni huwa ni very very ndogo almost negligible.
Lakini kuna watu akili zao zimekariri kuwa hutakiwi kuoa/kuolewa na mtu kutoka mkoa flani just bcoz amekariri tuu.
 
Soma vizuri sijakataa, nilichosisitiza ni kwamba utamaduni ni zaidi ya kabila: Ndio maana kuna wengine wanaweza mbali sana wakasema kwa mfano UTAMADUNI WA WAAFRIKA, UTAMADUNI WA WAZUNGU...Kabila linabaki kuwa muhimu..

Utamaduni wa Wazungu ndo upi?Utamaduni wa Waafrika ndo upi?Kwenda mbali sana ndo kufanya nini?Kama haukatai kuwa kabila tofauti na utamaduni tofauti nini maana ya kusema utamaduni ni zaidi ya kabila?Utamaduni ni nini?
 
Utamaduni ni utaratibu wa maisha kwa ujumla; ikijuisha lugha, vyakula, muziki, dansi, mila, desturi, teknolojia, sayansi na mambo mengine mengi. Ukichukulia utamaduni traditionally ndio wewe unavyojua. That is a parochial way of understanding culture; multidimensionally, culture is broader than that mostly defined by contexts.
 
Kuna uzi pia namuona Snipper alalalamika mkewe hamkaribishi maji ya kuoga, labda wametoka makabila tofauti ama tamaduni tofauti.

Hii "labda" inatoka wapi wakati ungeliweza kumwuuliza?
 
Najaribu kuangalia, je kuna umuhimu wa kuoana watu wa kabila moja ama tamaduni zinazoshabihiana?

Kuna migogoro mingine katika ndoa huchangiwa tu na kuwa watu wa tamaduni tofauti hivyo kutafsiri jambo tofauti na mweza wako.

waswahili hulonga mchezakwao hutuzwa....................kwahiyo ukicheza na wakabila lako uwezekano wa maelewano nao ni mkubwa lakini kuna mipaka yake pia. Nina jamaa yangu kutoka huko uchagani; eneo la machame, kamkimbia mke wake baada ya kutonywa na mabinti zake ya kuwa mke wake kanunua sumu ili amlishe afe arithi mali na wote wanatoka kijiji kimoja tena walisoma wote shule ya ukwanza na upili!
 
...

Najua kuna ndoa za watu wa kabila moja au utamaduni zimevunjika, lakini natamani kujua nafasi ya kabila/utamaduni tofauti katika mitafaruku ya ndoa.

Na kama kabila/utamaduni vina nafasi

Je, ni busara kurudi katika kabila au utamaduni unaoulewa kupata mwenza?

Je, wazee wetu waliona mbali ku-insist watu waoe kwenye makabila yao?
inarahisisha maisha lakini sioni kama ni lazima.

all i can say is kama kuna mambo madogo yanayoweza kuwa 'deal breakers' then ni vizuri kumwambia mwenzio ili kuepusha shari. mf hio ya w/ke kukatazwa kupiga mluzi ni mpya kwangu
 
Eiyer, pamoja na shule na uelewa tulioupata kwa kutembea, usidhani tumekuwa huru asilimia 100 na tamaduni zetu. Ona hapa chini

Social cognitive theory, used in psychology, education, and communication, posits that portions of an individual's knowledge acquisition can be directly related to observing others within the context of social interactions, experiences, and outside media influences.
images
 
Last edited by a moderator:
NAjua sio lazima
Mapenzi kwa ujumla ni kuchagua kile unachoweza kukivumilia kwa maisha yako na ukilinganisha na uwepo wa mpenzi

Ndio maana kuna wanaovumilia kukaa na watu wanaowapiga.

Nilichokuwa nazungumzia ni ile urahisi wa watu mnaotokea kwenye tamaduni moja kuishi pamoja.

inarahisisha maisha lakini sioni kama ni lazima.

all i can say is kama kuna mambo madogo yanayoweza kuwa 'deal breakers' then ni vizuri kumwambia mwenzio ili kuepusha shari. mf hio ya w/ke kukatazwa kupiga mluzi ni mpya kwangu
 
kwa haya makabila tuliyomiks hivi haya sijui kama imebaki tamaduni za kufuata kiviiile!
mfano mimi
mume wangu babake ni mchaga mamake mhaya
mimi mamangu mngoni(aliyelelewa unyakyusani toka ana mwaka)babangu mngoni aliyelelewa dar es salaam toka ana miaka 5 sijui!
hapo unaweza kuimagine hawa cutees wangu nawafundisha utamaduni wa aina gani!
so kwa wakati fulani kulingana na muda tulio nao pengne hili halina nafasi saaaana!
tunaenda kimjini mjini kwa kiasi kikubwa mengne yanabaki kuwa tabia binafsi za mtu sio utamaduni wa kabila husika!
BTW muda si mrefu Kongosho utaniuliza rangi ipi ndo poa kumiski kwenye harusi!
shikamoo ZOMBIE:yo:
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom