Ukabila na umimi/usisi.......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukabila na umimi/usisi..........

Discussion in 'Great Thinkers' started by M'Jr, May 18, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Katika siku za hivi karibuni dhana ya ukabila/udini na umimi imekuwa inachukua nafasi kubwa sana hasa baada ya msuguano wa kisiasa kuonekana unakuwa mkubwa hapa nchini. Nakumbuka katika hotuba kadhaa za baba wa taifa alikuwa akijaribu kukemea hili kwa nguvu sana hasa suala hili la udini na ukabila.

  Ukabila
  Katika hili ntatoa mifano michache ambayo inazungumzwa sana kwa kipindi hiki ili kuonyesha dhana ya ukabila inavyochukua nafasi katika siku za hivi karibuni. Nakumbuka katika uchaguzi wa mwaka 1995 kulizuka dhana ya ukabila ambayo ilienezwa ikikihusisha zaidi chama cha NCCR Mageuzi wakati huo kikiwa chini ya Mh. Lyatonga kuwa ni chama cha "wachaga" baadae dhana hiyo ikafutika hasa baada ya uchaguzi ule kumalizika lakini sasa imeibuka tena na kipindi hiki ikihusisha zaidi chama cha Chadema ambapo awali ilikuwa ikiita chama cha "wachaga" lakini sasa imepanuka zaidi na kukiita chama cha "Kaskazini" kinachonitia hofu kidogo hapa ni namna dhana hii inavyokuwa kwa kasi na wakati mwingine napata woga kidogo kuwa "watanzania tumeshafika hapo"

  Hivi tunapochagua kiongozi ni nini tunakuwa tunaangalia kutoka kwake? Je ni kabila lake, wapi anatoka au ni uwezo wake wa kufanya kazi? Inanisikitisha kidogo kwasababu ni dhana ambayo sasa inawaingia mpaka wasomi wakubwa ambao mi nilitegemea wangekuwa nguzo ya umoja na mshikamano wetu kama nchi.

  Udini
  Hivi majuzi baada ya tume ya katiba kutangazwa na kuapishwa niliendelea kusikia minong'ono kuwa "mbona waislam ni wengi kuliko wakristo" Dah hii nayo ikanifanya nitetemeke maana niliona sasa huku tunakokwenda siko na tena kigezo walichokuwa wanakitumia wenye hoja hiyo ni majina nikawa najiuliza hivi kwa mfano jina la "Jaji Augustino Ramadhani" unamuita mkristo au Muislam?

  Mi mtazamo wangu ni kwamba nafikiri bado tuna uwezo wa kurekebisha hili hasa kwa wanasiasa maana ukiangalia kwa kiwango kikubwa dhana hii inachangiwa na wanasiasa ambao wako tayari kufanya lolote ili kuwa bora wenzao huku wakiteketeza umoja na mshikamano tulionao watanzania. Mwisho nasema kwamba;

  "Yule anayewasema wenzie ni wakabila na wadini, yeye ndiye mkabila na mdini maana kama asingekuwa mkabila na mdini asingeona ukabila na udini bali uwezo wa kufanya kazi wa watu"
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hizi ni dhana mbili wanazotumia watu waliofilisika kimawazo na kisera (kama alivyosema Nyerere R.I.P).

  Huwa hawana pa kuangukia na wanazichagua ili kupata huruma za watu kuwa unaona dini yetu haijawahi kumtoa kiongozi wa juu nichagueni au nipeni uongozi niwakomboe au kabila letu limedharauliwa sana nichagueni muone maendeleo; kabila letu ni dogo sana na hatuna sauti nipeni uongozi nilikomboe au kabila letu ni kubwa sana na sisi ndo tunatakiwa kutoa kiongozi kwa sasa. Ni dhana mufilisi na wanaziendeleza na kuzidakia bila kujua madhara yake kwenye vichwa vya watu

  Maana unapopandikiza mbegu hizo kwenye vichwa vya watu ipo siku wale unaowaambia kuwa wanaonewa watanyanyuka na kusema sasa imetosha tumeonea sana wacha tujikomboe.

  Kuna jeshi ambalo lipo tayari muda wowote kujitolea kufanya hayo wanayoyapandikiza vichwani mwa watu bila kutarajia
   
 3. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mkuu kinachonitisha ni namna ambayo dhana hiyo imeanza kuongelewa na watu ambao mi nilitegemea wangekuwa mstari wa mbele kupingana nalo tena wanaongea wakiwa vifua mbele kabisa.

  Dah shame on them!
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu sitaki kumhukumu mtu ila haya mambo yameanzia mbali.

  Na hizo dhana zinavyotumiwa sijui kama wanajua madhara yake. Kuna vijana ambao hawana kazi kwa wingi sana na ambao kwa sasa ni hatari sana iwapo watapata mtu ambaye atawapa wazo mbadala la kufanya.

  Ni dhana potofu ambazo ningetegemea hata viongozi wetu wa juu wazipigie kelele ila inaonekana na wao wanajihusisha kuziongelea
   
 5. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mr Rocky,

  Wakati mwingine nachukia siasa mkuu kwasababu inawabadilisha watu na kuwafanya kuwa wanyama wasio na utashi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  M'Jr,

  Huwezi kuikimbia wala kuichukia maana ni kama maisha yetu ya kila siku hao wanasiasa ndio wanaoamua mustakabali wetu wakikaa kwenye viti vyao vya kuzunguka huwa ndio waamuzi wa nini kifanyike.

  Nafikiri tufike mahali hao wanaohubiri hayo mambo waambiwe kabisa usoni mwao kuwa hizo ni sera mufilisi na zimepitwa na wakati.

  Maana tukianza kujuana makabila hapa ni balaa; inawezekana mke wangu akawa mnyakusya na nikiwachukia wanyakyusa ina maana nianze na mke wangu kule ndani kitu ambacho hakitawekezekana kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...