UK Alumni Association Tanzania

UK Alumni Association Tanzania

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Wapendwa wana-TzECA,

Natumaini bado mpo na hamjambo.
Mimi Joseph Payne, mzungu ambaye alikuweko Edinburgh zamani, akaenda Dar es Salaam akasikika akiimba Bongo Fleva na mwishowe akawa mtu maarufu, n.k.

Nataka kukujulisheni nyote - lakini hasa wale waliohitimu shahada katika vyuo vya Uingereza na ambao wamesharudi kuishi Tanzania - kwamba linaanzishwa shirika la wahitimu wa vyuo vya Uingereza nchini Tanzania (UK Alumni Association Tanzania).

Tafadhali tembeleeni UK Alumni in Tanzania Network connects you with other UK alumni across Tanzania to foster support and mutual success. kwa maelezo zaidi na kujisajili kuhudhuria tafrija ya uzinduzi wa shirika hilo itakayofanyika baadaye mwezi huu hapa hapa Dar es Salaam. Kuna tangazo pia hapo chini katika ujumbe huu.

Fanya haraka iwezekanavyo, maana baada ya tarehe 16 inawezekana kwamba hawatakubali tena ombi lako.

Asanteni sana, na kila la heri.

Joseph
 
Back
Top Bottom