Alphonce Mawazo
R I P
- Sep 10, 2013
- 335
- 478
"Ingewafaa sana watoto wetu kama tungewarithisha elimu bora, kwa bahati mbaya kama taifa chini ya utawala wa ccm tumeshindwa na kwa makusudi elimu imekorogwa korogwa na wasioitakia nchi yet mema.
Urithi namba mbili ingefaa sana kama tungewarithisha ardhi na mifugo, hili pia tumeshindwa maana wazawa wamewekwa rehani na wageni wamepewa kipaumbele kwa kusainishwa miaka mia kasoro mitano, wakubwa wametunga sera mpya ya ardhi inayoiruhusu serikali kupora na kunyakua ardhi ya hoi hae au masikini itakavyoona vyema na kumpa mgeni maarufu kama muwekezaji.
Kuna urithi ambao tutake tusitake tutawarithisha ambao ni MACHAFUKO NA VURUGU KUBWA au VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE maana dunia ya leo hakuna mjinga tena aliyetayari kujifia ndani eti tu kwa kuheshimu SHERIA ZA KIBAGUZI NA KANDAMIZI zenye kumwonea huyu na kumwacha yule, na siku hiyo ikifika hakuna atakayekuwa salama.
Ni vyema sasa tukaangalia chama chenye sera zenye tija kwa mnyonge ambacho kwa hakika kwa sasa ni chadema na washirika wake wa ukawa" Magufuli ambaye ni mbunge wenu hajawahi kulia kwa ajili yenu juu ya ardhi na mifugo ingawa nyie huku ndo wahanga wakubwa, yeye anajisifia lami utafikiri ndo urithi wenu...hamna maji ingawa ziwa ni kilomita mbili, ni lazima mtazame mbali zaidi watoto Hawa watatulaani maana wanakuja kuwa wachota maji wa wazungu na wapishi Wa wakubwa."nimefupisha kwa ajiri ya muda ingawa ilikuwa hotuba ya saa moja na nusu...nawasilisha