Ujumbe wangu kwa wagombea wote wa kata ya Makutupora

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Mar 14, 2013
165
39
Salaam wananchi wenzangu wa Kata ya Makutupora.

Ni mara chache sana natumia jukwaa hili kueleza mambo yanayotendwa kwenye kata yetu yenye rasilimali zote muhimu kwa maendeleo ya umma wetu.

Leo nitumie fursa hii kuwaeleza yale yaliyofanyika kwa kipindi hiki cha vuguvugu la uchaguzi ndani ya vyama mbalimbali vya siasa na mtazamo wangu wa nini kifanyike baada ya uchaguzi ambao tunategemea utafanyika mwishoni mwa mwezi November.

Nianze kwa kuwapongeza wale wote mliotia nia ndani ya vyama vyenu na kuomba kupewa fursa ya kupeperusha bendera za vyama vyenu,bila kujali kama vyama vyenu vimewapa ridhaa ya kuwania nafasi yoyote au laa, kwangu mimi mmetimiza haki yenu ya kikatiba na mmeonyesha umuhimu wa demokrasia ndani ya vyama vyenu na nje ya vyama vyenu.Vilevile mmetoa funzo kwa viongozi waliopita na watakaopata fursa ya kutumikia wananchi wa Kata yetu kongwe na pendwa ya Makutupora.

Acha niwapongeze mliopewa fursa ya kupeperusha bendera ya vyama vyenu,kwa kata yetu ya Makutupora niwapongeze wagombea wote waliopewa fursa na chama Cha Mapinduzi (CCM0 kwa kuwa ninyi mnangoja kuapishwa na kuanza kazi mara moja ya kuwatumikia wana wa Makutupora.

Uwe umeshinda kwa kutumia nguvu za makundi ya waharifu, uwe umeshinda kwa kutumia ushawishi ndani ya chama kuanzia tawi hadi mkoa,uwe umeshinda kwa nguvu ya wananchi ama umepewa neema na viongozi wa chama ninakupongeza kwa ushindi wako ambao tafsiri yake ni ushindi wa wananchi wa kata ya Makutupora kwa maana unakuja kututumikia sote.

Sasa twende pamoja nikueleze yakupasayo kutenda kuanzia utakapo apishwa wewe mshindi,fahamu makutupora ina wananchi wengi wenye sifa za kushika nafasi uliyopewa na wenye sifa, fahamu tumekuamini kwamba utatuvusha na kufanya mengi ambayo hayajafanywa na watangulizi wako.Tunaimani sana kwamba umekuja kwa wakati sahihi mno,fahamu zipo changamoto nyingi utakutana nazo lakini fahamu tumekuweka hapo ili utekeleze matakwa ya wananchi na takwa letu la kwanza ni Maendeleo tu.

Kiongozi fahamu ndani ya mtaa wako kuna makundi ya waharifu,na kundi hili la waharifu huenda linalelewa vyema na wananchi wenye nguvu ya ushawishi ndani ya chama chako na wana nguvu ya fedha na huenda wana mamlaka makubwa sana na maamzi juu yako.

Kiongozi fahamu kwamba ndani ya mtaa wako kuna wamama, vijana na watoto wenye mahitaji maalum,hivyo ni matarajio yao kwako kwamba utakusanya rasilimali vitu/fedha na watu kuwapa badiliko katika maisha yao.

Kiongozi naomba ufahamu ndani ya mtaa wako/kata yako kuna mipango iliyokwisha kupagwa na mingine inatekelezwa hvyo ni wajibu wako kuifatilia na kuhakikisha mipango hiyo inatekelezwa kwa wakati,fahamu tumechoka na kucheleweshwa kwa utekelezaji wa mipango yenye tija kwa kata ya makutupora.

Kiongozi nataka ufahamu kwamba ndani ya mtaa/kata kuna idadi kubwa ya watoto ambayo haina uwiano na miundo mbinu tuliyonayo,hivyo ni wajibu wako kusukuma hoja za msingi ili tuone miundo mbinu ikijengwa kwa kasi kwa maslahi ya wana wa Makutupora.

Achana na tabia ya kuwambia wananchi wasichangie katika kuanzisha,kupanua na kuendeleza miladi mbalimbali yenye tija kwetu,tabia hii ife kifo chema na uiziike kabisa.

Kiongozi naomba kukujulisha kwamba utakutana na mchwa ndani ya mtaa/kata yako ambao hula mbao,misumari, mabati na vifaa vyote vinavyoletwa kwa fedha ya wananchi ili kujenga miundo mbinu mbalimbali.

Aidha fahamu mchwa hawa wamekuwepo tangu miaka ya 1990 na wengine wamezaliwa na wanatafuna kwelikweli kuanzia ndani ya chama mpaka huko serikalini,mchwa hawa watakutisha na kwa kweli wanatisha mno kwa sura zao,rangi zao na misuli ya macho na mikono yao.Utakutana na JIWE,nondo na chuma cha pua,usiogope tupo maelfu ya wananchi njoo uwashitaki kwetu nasi tutawashughulikia ndani ya chama chetu na nje ya chama.

Kiongozi fahamu kwamba Shule ya sekondari ya Makutupora bado ina hitaji umeme ili kuwezesha shughuli za masomo kuendelea bila shida,aidha tunahitaji shule ya msingi weyula kupanuliwa ili kukidhi ongezeko la watoto wetu.

Kubwa nalotaka ujue ukiweza pambana na waharifu,tumechoka kula vibudu na nyama zinazoletwa kwenye mabucha yetu kwa njia zisizo rasmi,aidha pambana na kundi la mwenye kundi,mweleze tumechoka kuibiwa na kuona mitaa yetu kila uchwao kuna ng`ombe wamekamatwa walioibwa na wazee wa mzee.

Kiongozi ninaomba utambue kwamba kuna vijana waliotelekezwa na wamekata tamaa na wamekuwa walevi wa gongo,choya ,bangi na wameanza kujiunga na makundi ya uharifu.Utaweza kufanya neema kwako kwa kubuni miladi mbalimbali itakayowafanya washiriki na kufaidika moja kwa moja hivyo kuwaondoa katika kupotea kwao.

Ndugu Kiongozi naomba ufahamu tumechoshwa na ukabila na tabia za kutenga watu wenye uwezo wa kuleta chachu ya maendeleo, hivyo tumia safu ya wananchi wakusaidie katika kutatua kero zetu ili tufike nchi ya ahadi uliyoitaja wakati unaomba nafasi ndani ya chama chetu.

Vilevile shughulika na ahadi zako na pambana kuhakikisha walivyokula mchwa vinaludi kwa wanachi,fatilia vyanzo vyote vya mapato na washirikishe wananchi namna ya kutumia vyanzo hivi.

Tutafika tunapotaka kufika endapo tutakuwa wamoja na tutania na kufanya kwa pamoja,hakika MAKUTUPORA mpya inakuja na wenye nia ovu na Kata yetu watafute pa kuishi, nasema nina imani kubwa na Wenyeviti wote na natumaini hamjaja kushiriki uporwaji wa ardhi za wanyonge,hamjaja kuwakandamiza Mayatima na Wajane,Msijifanye miungu watu.

Ninawatakia mafanikio makubwa katika kutekeleza ilani ya chama na matakwa ya Wana wa Makutupora.

SILAHA YA MNYONYE NI UMOJA.
KWA PAMOJA TUTAFIKA NCHI YA AHADI.
NI MTUMISHI NISIYE NA FAIDA NIMEANDIKA KWA NIABA YA WANANCHI
 
Back
Top Bottom