UJUMBE MZITO KWA MAGUFULI NA CHAMA CHANGU CHA CCM
Mheshimiwa Rais wangu, Pole sana kwa majukumu yako ya uchaguzi. Unajitahidi sana kufanya campaign ya ushindi, kwa bahati mbaya mambo hayaendi vizuri. Napenda ni kosoe na nitoe ushauri, tunao muda wa kuwe kufanya mabadiliko yenye manufaa, na yakatuletea ushindi.
Mpaka dakika hii, hali sio nzuri, na kama hatutajirekebisha, basi tujitayarishe kushindwa, na utakuwa kiongozi aliyefanya CCM kiangushwe na Mtu mmoja pekee anayeitwa LISSU. Chadema hakina Ubavu, nguvu yao leo ni Lissu na Jana alikuwa Lowassa.
Mheshimiwa Raisi, Hii timu yako ya akina Bashiru, Polepole, Kabudi na wengineo, hawana mazoea ya kazi kama hii ya campaign. Please stop using those who are Book or Classroom smartness, but we need those with Street Smartness, watakaoweza kuweka mikakati madhubuti na wanajulikana kwa kazi zao nzuri.
Mheshimiwa Rais, Leo Lissu kila anapohutubia, analitumia jina la Baba wa Taifa vizuri sana, tena kwa manufaa yake, na linawavutia sana wananchi. Lakini huyu huyu Lissu, alidiriki kumkebehi BABA wa TAIFA na kumuita Dikteta na kumshutumu kwa mabaya. Cha kushangaza Hii timu yako unayoiona ni kabambe, wameshindwa kuitumia dosari hiyo na kuzitafuta video clips za Lissu akimkebehi Marehumu Baba Wa Taifa, na kuwaonyesha wananchi, rangi ya huyu mgombea urais wa Chadema.
Rais, hii timu yako iliyokushauri kuwakata Wagombea Ubunge na Udiwani walioshinda kwa kura nyingi, na kuwaweka vipenzi wao, kumesababisha manunguniko mengi, na kuwakasirisha wapiga kura wengi, ambao hivi sasa wameshawishika kuwapigia kura wabunge ama madiwani wa upinzani. Dhulma hii itatutesa sana.
Mheshimiwa, Kama ni kweli hushauriki, tunakuomba USHAURIKA, na kama ni ushauri mbaya wa watu wako, fanya Mabadiliko kwa haraka sana.
Bado tunao wakati wa kuweza kufanya mabadiliko, yatakayo tuletea ushindi wa kishindo kikubwa. Tunahitajika mabadiliko kufanyika haraka sana, WARUDISHE FRONT LINE WALE VIGOGO WANAOPENDWA NA KUAMINIKA NA WANANCHI, KAMA KINA 1) KIKWETE, 2) KINANA 3) MAKAMBA SNR na JNR,
Mheshimiwa Rais tunahitaji kuamka, tumo kwenye ndoto ya ushindi, tusio na uhakika nao. Unfortunately we have surrounded ourselves with people who are not expert in the TRADE of campaign and winning Elections.