Ujumbe wa mwanangenzi vitali Maembe kwa msanii Roma

Ghulaam

JF-Expert Member
May 10, 2016
1,847
1,440
Pole sana Roma!
Mara ya kwanza nilikuambia Hongera, lakini leo nakwambia POLE!
wimbo wako unatuonesha kuwa unajuta kuimba Ukweli, Unajuta kusimama upande wa Watu na Unaonesha kuwa Mtindo uliotumika kukunyamazisha na kukubadilishia Muelekeo umefanikiwa.

Mdogo wangu, Mwanaharakati wa Haki za binadamu hatorudi nyuma hata kwa gharama ya Uhai wake.
'Mbegu huota, kukuwa na kutoa Matunda baada ya kutupwa chini, kufa na kuoza'

Uliimba nyimbo nzuri kaka, lakini usiwatishe au kuwakatisha tamaa wapambanaji wengine wa haki za Binaadamu kwa kutumia Muziki!

Dunia ni tamu, Maisha ni Matamu kwa wenye chochote, hivyo nikitafuta sababu ya kurudi nyuma sitaikosa na itakuwa ni ya maana kwangu.
Lakini nawezaje kunyamaza wakati wanyonge wengi hawapati haki zao kama binadamu.
Naweza nyamaza kwa kufikiri kuwa nawasaidia Viongozi, lakini hata nao Viongozi wetu na watunga Sera wana haki ya kupata Ushauri kutoka kwa wasanii na kupata hisia za wanajamii ili wafanikishe Maendeleo.
kama naimba Masaibu yangu pekee nikipozwa nitanyamaza, lakini kama naimba hisia na ukweli, sauti ya wanajamii sitageuka nyuma mpaka tone la mwisho la Damu yangu.

Msikilize FELA KUTI, Wapambanaji waoga au wabinafsi hawakosi sababu ya kurudi nyuma.

"Watu wangu wanaiyaishi Majonzi, Machozi na Damu!
Hiyo ndiyo alama yao wakati wote!

Kila mtu anakimbia kimbia
Watu wanatawanyika ovyo ovyo!
Wengine wanapoteza Mkate
Wengine wanakaribia kufa Wengine wanakufa!

Lakini...
Tumekuwa waoga sana
Tunaogopa kitu ambacho hatukioni
Tunaogopa hewa inayozunguka
Tunaogopa kupigania uhuru wetu
Tunaogopa kupigania haki yetu
Tunaogopa kuipigania furaha yetu.
Siku zote tunajipa sababu za kuogopa!
Tunaanza kujiambia....
Sitaki kufa
Sitaki kujeruhiwa
Nina mtoto mmoja
Nna Mama Nyumbani
Nna baba Nyumbani
Sina nyumba
Nataka kujenga Nyumba
Sitaki kujichosha
Nataka kuinjoi
Sitaki kuondoshwa

Hizo zote ni sababu muhimu lakini je, hivyo ndiyo watu waliopewa vipaji waisaidie jamii wanapaswa kufikiri?

Usimkatie tamaa mtu aliyepotea njia, Usijiunge na Upotevu wake, mrudishe kwenye mstari kwa gharama yoyote.
Usipambane kwa Chuki, pambana kwa Upendo. Mwisho wa siku tunataka kukaa na adui Meza moja tukiwa marafiki na kuijenga nchi.
Na hiyo ndiyo kazi ya Muziki.
 
Hata sikuelewi mkuu, au wewe ndo ulimteka? Maana naona unajitahidi kumuondolea credibility. sijasikia popote kwenye ngoma yake akikatisha tamaa.

Inaonekana nia ilikuwa ni kumuondolea imani kwa washabiki wake na wananchi kwa ujumla.

Hata hayo mashairi umeyatafsiri ndivyo sivyo.
 
Huyu Vitali Maembe anajiundia hoja isiyokuwemo katika Wimbo wa Roma na kisha kujijibu mwenyewe!.

Bob Marley alivyokoswa Koswa kupigwa risasi aliimba wimbo wa Ambush in the Night, ni nini cha ajabu Roma kuimba Maswahibu yaliyomkuta?.

Fasihi ya Roma iko juu sana, na upeo wa Mashairi yake unaonyesha ni kijana mwenye I.Q kubwa pengine ndiyo maana umeshindwa kumuelewa!!
 
Muandikaji ni mwanafasihi usiwe mvivu kusoma

Angalia maneno ya Mwanamuziki Fela kuti

Unapoamua kujitoa sadaka hupaswi kufikiri utaishije utaishi kwa namna maisha yatakavyokuwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa nyimbo ya Roma waliomteka ni siri-kali tena kile kijamaa kikuda chenye roho ya kutu , kikipata sapoti kutoka kwa Kingpin wa kuharibu demokrasia ndio maana hata upelelezi hawajafanya kawa sababu watekaji ndio hao hao
 
Huyu Vitali Maembe anajiundia hoja isiyokuwemo katika Wimbo wa Roma na kisha kujijibu mwenyewe!.

Bob Marley alivyokoswa Koswa kupigwa risasi aliimba wimbo wa Ambush in the Night, ni nini cha ajabu Roma kuimba Maswahibu yaliyomkuta?.

Fasihi ya Roma iko juu sana, na upeo wa Mashairi yake unaonyesha ni kijana mwenye I.Q kubwa pengine ndiyo maana umeshindwa kumuelewa!!
Soma alichokinukuu kutoka kwa nguli wa muziki Fela

Kisha sikiza wimbo wa Zimbabwe nukta kwa nukta

Kimsingi hamjamdharau popote soma elewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bangi ikikupeleka kwenye alucinations na kukufanya uone au uhisi vitu ambavyo havipo ni bora uache
 
We umejificha nyuma ya keyboard weka ID inayojulikana alafu uanze kuisema serikali tukuone kama kweli we kidume.

anakwambia haogopi kufa ila nani kati yenu atampa mwanae malezi !!!, mkewe nan atampa mahitaji !!
Wakati alivyokuwa hospital hukwenda hata kumuona .

We unaongea tu hujui adha aliyoipata
 
Akifa kwa malaria nani atatoa malezi?

Aliyeandika ni msanii Vitali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni upumbavu sana. Kujiona jasiri nyuma keyboard. Harafu unashutumu aliyejitahidi japo kuimba hadharani. Pumbavu sana. Huu ni unafiki wakijinga sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom