Ujumbe wa mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu haupaswi kupuuzwa

Michael Uledi

Senior Member
Mar 29, 2023
132
322
Ujumbe Mahususi wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Dodoma,Ndugu Ngozi kwa wenye akili unapaswa kubebwa kwa uzito mkubwa!Ujumbe huu unakuja baada ya Mh Ngozi kutokea kwenye Vikao vya CCM ambayo vilikuwa vinaendelea Jijini Dodoma mpaka jana!

Ujumbe huo ambao umebeba "Salamu mahususi" kwa Wanachama wa CCM kote Nchini umeonya baadhi ya makundi ndani ya Chama ambayo yamekuwa yakizorotesha kazi nzuri ya Mh Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa either kwa sababu za kisiasa au tamaa ya madaraka kuelekea mwaka 2025.

Ni ukweli ulio wazi kuwa kuna kundi kubwa la wanaccm ambalo limeamua "kumute" na kutomsemea Mama Samia Suluhu Hassan kuhusu kazi zake nzuri ambazo anazofanya!

Zaidi Mh RAIS amekosa kabisa watetezi kutoka ndani ya Chama ambao wanaweza kutetea,kushawishi na kuzilinda kazi nzuri za Utekelezaji wa Ilani ya CCM kiasi kwamba wengine wameamua kuzikataa hata kazi nzuri ambapo amekuwa akizifanya na kuzindua za miradi ya Kitaifa na kusema sio zake!

Tabia hizi za hovyo hazikubaliki na hazina maslahi kwa Chama na Serikali ya CCM kuelekea mwaka 2025.Pamoja na mambo mengine muhimu niseme tu kwamba wakati umefika sasa kwa Mh Rais kuamua kutumia ile Style ya "Usinizoeee au Mnikome" katika kuendesha Serikali!

Hakuna wakati ambao wanaccm wameonyesha wazi wazi kubeza kazi nzuri za Utekelezaji wa Ilani kama awamu hii japo ni wazi kuwa awamu ya Sita ndio awamu iliyotekeleza miradi mingi ambayo inagusa wananchi wa kawaida moja kwa moja!

Ujumbe wa Ndugu Ngozi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu unapaswa kupewa jicho kubwa kabla haijaleta madhara kwa wahusika! Mwenyekiti wa CCM wa awamu ya tano, hayati John Pombe Magufuli aliwahi kuwafutia Uwanachama baadhi ya wanaccm kwa makosa kama haya!

Msije mkadhani haiwezekani kwenu,inawezekana na haitishibdikana!Ujumbe huu unapaswa kupewa "attention" kubwa!

Kidumu Chama cha Mapinduzi.


IMG-20230523-WA0060.jpg
 
Asiwapangia watu misimamo yao kama yeye kaamua kuwa katika kundi la kuona mazuri ya SSH (honorable causa) na hakuna ambaye ana lalamika yeye kuwa katika kundi hilo basi na wangine Wana haki hiyo hiyo ya kuwa tofauti sio lazima Wana ccm wote waamini falsafa ya honorable causa na hii ndio demokrasia
 
Back
Top Bottom