Ujumbe wa Mwenyekiti Tundu Lissu (Sehemu ya Kwanza)
“Ndugu zangu,
Kwa wiki kadhaa sasa nimewekwa kwenye total isolation — upweke wa kulazimishwa. Wale wafungwa wenzangu waliokuwa nami kwenye selo moja, ambao walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, wametolewa wote; nimeachwa peke yangu.
Selo yangu sasa imewekwa kamera za ufuatiliaji (CCTV) zinazorekodi kila kitu ninachofanya, hadi wakati ninapokojoa au kubadilisha nguo. Sina faragha yoyote tena. Hili si suala la usalama bali ni kudhalilishwa kwa utu wangu kama binadamu.
Naomba jambo hili lipigiwe kelele kwa nguvu zote, kwa sababu ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na ni kosa kisheria chini ya Kanuni za Umoja wa Mataifa za Matunzo ya Wafungwa (Mandela Rules), ambazo zinasema wazi kuwa:
• Utu wa binadamu unabaki kuwa wa heshima hata akiwa gerezani (Kanuni ya 1),
• Upweke wa muda mrefu au unaomnyima mfungwa mawasiliano ni ukatili na mateso (Kanuni ya 43 na 44).
Pia ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 12 na 13, zinazolinda hadhi ya mtu na kumzuia kuteswa au kudhalilishwa.
Niko tayari kuvumilia hali yoyote kwa ajili ya imani yangu katika haki na uhuru wa watu wetu, lakini udhalilishaji wa utu wa binadamu hauwezi kukubalika — si kwangu tu, bali kwa yeyote anayebeba jina la mwanadamu.”