Ujumbe wa baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA kuipasua CCM vipande vipande)

Katika hali isiyoya kawaida, viongozi wakubwa wa Chama cha mapinduzi CCM pamoja na Makada wakongwe wa Chama hicho, wamejikuta hawapati usingizi kutokana na kile kinachoitwa 'Ukandamizaji wa Demokrasia nchini' unaoonekana kuegemea upande mmoja wa upinzani, upande ambao umeonekana kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania, na sasa hata baadhi ya Vijana wa CCM pamoja na moja ya makada wakongwe wamediriki kutamka kuwa wataiunga mkono BAVICHA kulaani ukandamizaji huo wa demokrasia, kwani kwa kukubaliana na dhuluma hiyo, hakuleti afya hata ndani ya Chama chao cha CCM, na wanaamini kuwa Bila upinzani makini, nchi hii haiwezi kusonga mbele, na CCM itajisahau kuisimamia serikali yake.

Viongozi waandamizi wa Chama cha mapinduzi CCM wameendelea na vikao vya siri kutafuta namna ya kuishauri Serikali iangalie upya kauli yake kuhusu kuzuia shughuli za kisiasa nchini, kwani kauli hiyo haiwezekani kutekelezeka kabisa, na serikali ilipaswa kujifikiria mara mbili kabla ya kutoa kauli hiyo.

Chama cha mapinduzi kipo Njia panda, ama kiahirishe shughuli yake hiyo ya kumkabidhi uenyekiti Mhe. John Pombe Magufuli, au kilazimishe kufanyika kwa mkutano huo, jambo ambalo litahatarisha amani ya nchi kwa kupelekea machafuko ya kisiasa, pamoja na kukigawa chama hicho cipande vipande.

Akizungumza kwa nyakati tofauti, Mhe. Patrick Ole Sosopiambaye ni makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ameweka msisitizo juu ya kuheshimu demokrasia nchini, na amewataka vijana wote nchini kuwa majasiri na mstari wa mbele katika kutetea na kusimamia maslahi mapana ya Taifa, na kutokuweka maslahi binafsi na ya vyama mbele... badala yake waungane kwa umoja wao, kulaani ukandamizwaji wa Demokrasia nchini, kwani bila demokrasia, nchi hii itakuwa ni nchi yenye jamii isiyo hoji, jamiii isiyojua taifa lao linakwenda wapi.

Mmoja wa viongozi wakubwa wa CCM nilipopata wasaa wa kuzungumza naye katika mazungumzo ya faragha, alinihakikishia kuwa, hali ya kisiasa ndani ya Chama cha mapinduzi CCM ni tete, kuna hali ya sintofahamu kubwa, mafrakano, makundi yanayopingana, na alitabiri mgawanyiko ndani ya chama hicho hivi karibuni, lakini aliniasa kuwahamasisha vijana wanaopenda amani ya nchi ambayo ni zao la Haki, kutokukubali kurudishwa nyuma, na alisema kuwa, Endapo BAVICHA watashikilia msimamo bila kuyumbishwa yumbishwa na propaganda na vitisho vya hapa na pale, watakuwa wamelikomboa taifa hili.

Wasomi na wataalam wa masuala ya kisiasa wamewasihi vijana wote wa vyama vya siasa kuungana na BAVICHA, kuitetea demokrasia, na kuvitaka vyombo mbalimbali pamoja na asasi za kiraia kuwaunga mkono BAVICHA, kuhakikisha Demokrasia inalindwa nchini.
Na umri huu bado huijui ccm? Tulia peke yake amewashinda, sembuse chama dola
 
BAVICHA niwapi imesema italeta machafuko? Shirikisha ubongo

Ubongo hana n ahawezi tena kuupata kwa sababu uliioza ukatupwa. Aliuacha Lumumba stooni akajazia kinyesi dani ya fuvu lake la kichwa ili afanye vyema kazi ya buku saba. Ukimwambia ubongo na yeye ana ile bidhaa nyingine kwenye fuvu, hata hawezi kuelewa. Unapoteza muda.
 
mtaandika kila aina ya mabandiko lakini mwisho wa siku bado CCM itafanya mkutano hawatasogea kabisaa hao bavicha. kwa Ulivyoandika kwa ushabiki eti mheshimiwa!!
 
Chanzo cha udikteta ni UBINAFSI. Sasa iweje chama fulani cha siasa kifanye mikutano wakati vyama vingine vinazuiliwa.
 
Kama wewe nI kidume nenda Dodoma kafanye unayotaka kuyafanya unaona mkono wa she ria unavyofanya kazi utawekwa mahali salama na jamii yako itapata tabu kwa ujinga wako na kutafuta sifa usizopata watu wa mwigulu wanakusubili
 
CCM ni wamoja na ni Wamoja zaidi hasa pale unapodhani wewe wana matatizo hilo liondoe ktk mawazo yako/yenu.
 
vijana nchi hii kwa ujumla wao wakiungano na hao BAVICHA bila woga wowote kwa gharama ya damu zao NCHI inaenda kubadilika. Kinyume cha hapo mambo yatakuwa kama jana tu.
 
Kwani watakaoanzisha hayo machafuko ni wale wanaoipinga sheria mama au wanaotaka iheshimiwe? Mimi S ioni tatizo kama tutaifuata na kutiki sheria mama
 
Back
Top Bottom