Ujumbe wa baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA kuipasua CCM vipande vipande)

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Katika hali isiyoya kawaida, viongozi wakubwa wa Chama cha mapinduzi CCM pamoja na Makada wakongwe wa Chama hicho, wamejikuta hawapati usingizi kutokana na kile kinachoitwa 'Ukandamizaji wa Demokrasia nchini' unaoonekana kuegemea upande mmoja wa upinzani, upande ambao umeonekana kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania, na sasa hata baadhi ya Vijana wa CCM pamoja na moja ya makada wakongwe wamediriki kutamka kuwa wataiunga mkono BAVICHA kulaani ukandamizaji huo wa demokrasia, kwani kwa kukubaliana na dhuluma hiyo, hakuleti afya hata ndani ya Chama chao cha CCM, na wanaamini kuwa Bila upinzani makini, nchi hii haiwezi kusonga mbele, na CCM itajisahau kuisimamia serikali yake.

Viongozi waandamizi wa Chama cha mapinduzi CCM wameendelea na vikao vya siri kutafuta namna ya kuishauri Serikali iangalie upya kauli yake kuhusu kuzuia shughuli za kisiasa nchini, kwani kauli hiyo haiwezekani kutekelezeka kabisa, na serikali ilipaswa kujifikiria mara mbili kabla ya kutoa kauli hiyo.

Chama cha mapinduzi kipo Njia panda, ama kiahirishe shughuli yake hiyo ya kumkabidhi uenyekiti Mhe. John Pombe Magufuli, au kilazimishe kufanyika kwa mkutano huo, jambo ambalo litahatarisha amani ya nchi kwa kupelekea machafuko ya kisiasa, pamoja na kukigawa chama hicho cipande vipande.

Akizungumza kwa nyakati tofauti, Mhe. Patrick Ole Sosopiambaye ni makamu mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ameweka msisitizo juu ya kuheshimu demokrasia nchini, na amewataka vijana wote nchini kuwa majasiri na mstari wa mbele katika kutetea na kusimamia maslahi mapana ya Taifa, na kutokuweka maslahi binafsi na ya vyama mbele... badala yake waungane kwa umoja wao, kulaani ukandamizwaji wa Demokrasia nchini, kwani bila demokrasia, nchi hii itakuwa ni nchi yenye jamii isiyo hoji, jamiii isiyojua taifa lao linakwenda wapi.

Mmoja wa viongozi wakubwa wa CCM nilipopata wasaa wa kuzungumza naye katika mazungumzo ya faragha, alinihakikishia kuwa, hali ya kisiasa ndani ya Chama cha mapinduzi CCM ni tete, kuna hali ya sintofahamu kubwa, mafrakano, makundi yanayopingana, na alitabiri mgawanyiko ndani ya chama hicho hivi karibuni, lakini aliniasa kuwahamasisha vijana wanaopenda amani ya nchi ambayo ni zao la Haki, kutokukubali kurudishwa nyuma, na alisema kuwa, Endapo BAVICHA watashikilia msimamo bila kuyumbishwa yumbishwa na propaganda na vitisho vya hapa na pale, watakuwa wamelikomboa taifa hili.

Wasomi na wataalam wa masuala ya kisiasa wamewasihi vijana wote wa vyama vya siasa kuungana na BAVICHA, kuitetea demokrasia, na kuvitaka vyombo mbalimbali pamoja na asasi za kiraia kuwaunga mkono BAVICHA, kuhakikisha Demokrasia inalindwa nchini.
 
Asee Ukawa naipenda tena Sana Sana lkn hizi fix za bavicha kuleta machafuko nchini ataziamini ambae akili yake ina mushkeli, Uchaguzi Mkuu tulilalamika wee kimya, Zanzibar tukapiga kelele wee kimya, kuvurugwa kwa mahafali ya Chaso mambo yakawa vile vile mikwara mingi afu kimya, sa mikwara mingine mipya imeletwa tena . Kama tumeamua kuwa kimya na tuendelee kua kimyaa tu. Mikwara ya BOB MAZISHI haina msaada wowote muda huu.
 
BAVICHA niwapi imesema italeta machafuko? Shirikisha ubongo
 
Swali langu, kama matukio kibao yamefanyika na matamko kibao yametolewa na WASOMI, WANASIASA MAARUFU, VIONGOZI WA DINI lkn bado watawala hawakuyatilia maanani unadhani kitu gani kitawafanya sasa waogope kufanya mkutano wao wa chama? NIPE FACTS MKUU
 
Wanapiga mikwara ili watu watishike waseme wakae meza moja wafanye mazungumzo. Watu wamekaza kama walivyokaza bunge la bajeti mpaka limeisha
 
Asee Ukawa naipenda tena Sana Sana lkn hizi fix za bavicha kuleta machafuko nchini ataziamini ambae akili yake ina mushkeli, Uchaguzi Mkuu tulilalamika wee kimya, Zanzibar tukapiga kelele wee kimya, kuvurugwa kwa mahafali ya Chaso mambo yakawa vile vile mikwara mingi afu kimya, sa mikwara mingine mipya imeletwa tena . Kama tumeamua kuwa kimya na tuendelee kua kimyaa tu. Mikwara ya BOB MAZISHI haina msaada wowote muda huu.
Huo ni mtazamo wako maana mdomo ni wako
 
Back
Top Bottom