"ujumbe umepokelewa" - DC Mnali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"ujumbe umepokelewa" - DC Mnali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Teamo, Feb 27, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Waliomwadhibu wangeachwa peke yao wakauke kama vigae na nyongo zao.

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, alilitangazia taifa kuwa dili ya Richmond ilikuwa safi na taifa halikupata hasara yoyote.

  Baada ya ukweli kujulikana sambamba na hasara kubwa kubainishwa, mawaziri walijiuzulu, mkataba ukavunjwa na kwa ajili hiyo serikali yote ilivunjwa ikaundwa upya.

  Huu ni mwaka wa ngapi, Hosea yupo palepale. Sasa anawakamata wenzake. Anaendelea kulipwa fedha za wale wale wananchi aliowadanganya.


  Sasa hivi wanasikia serikali inafanya mpango wa kumlipa gumegume mmoja tu shilingi bilioni 222 ili achapishe vitambulisho, kazi ambayo Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali anasema anaweza akaifanya kwa shilingi bilioni 95 tu. Kwa nini walimu wasisimame kidete kudai kuokolewa kwa shilingi bilioni 127 ambazo ni zaidi ya kuboresha maisha yao wote!Waliwaambia serikali haina fedha, sasa fedha hizi hapa zimeonekana. Kama Spika Samuel Sitta amezuia hoja ya kumjadili Lawrence Masha ili haya yote yasijitokeze, kwani Urambo kwenye jimbo lake hakuna walimu? Hakuna wanafunzi? Hakuna wazazi? Akija nendeni nyumbani kwake si mbunge wenu (kijana wenu) mkamuulize awaeleze ilikuwaje?

  DC, Albert Mnali hakuwachapa walimu wote aliokutana nao na aliowachapa hakuwachapa kwa ualimu wao. Aliwachapa walevi, watoro, na ambao hawakutimiza wajibu wao. Anayetetea uozo huu ni sehemu ya uozo wenyewe.
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Matatizo mengi yanayoikabili TZ kwa sasa yanaweza kutatuliwa kwa kujituma katika utendaji kazi na kachapana viboko inapobidi.China imeendelea kwa kuweka vipaombele sera za uongozi wa nchi na maslahi ya taifa.Mafisadi na wahujumu uchumi China hunyongwa hadi kufa kosa likidhibitishwa na mahakama,sasa viboko na kunyangwa ipi adhabu kali.Nchi hii haiwezi kuendelea kwa uongozi wa kisanii bali kwa viongozi kuwa na nia njema ya kuendeleza nchi na kuachana na tamaa ya kujilimbikizia mali na upendeleo katika uongozi.
   
 3. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nimeona kwenye mwananchi la leo,kuna DC anasema kuwa Mnali ni shujaa.Ameenda mbali hadi kufananisha alichokifanya Mnali na lile agizo la PM,kuwa eti hakuna tofauti...
  Check it here;
  Mwananchi Read News
   
Loading...