Ujumbe Muhimu kwa wana CCM Wote

Ujumbe Muhimu kwa wana CCM Wote

First they came for the Jews
and I did not speak out
because I was not a Jew.
Then they came for the Communists
and I did not speak out
because I was not a Communist.
Then they came for the trade unionists
and I did not speak out
because I was not a trade unionist.
Then they came for me
and there was no one left
to speak out for me.
 
Asante comrade kwa kuiona kaz ya nape nategemea kuskia kauli ya kinana na jk kuhusiana na hili jambo vingnevyo ccm tutakuwa tunajikaanga wenyew maana hyo combination ya wabunge wasio mawazir itakuwa na nguvu ambayo sio tulia tuli wala job atakaeizima hasa kwa wakat tunaelekea kwny bajet, bajet ambayo haijatrkelezwa hata robo
 
Wana JF,
Napenda kujua, Kati ya nape na Magufuli nani aliyeisalimisha ccm July 2015 pale Dodoma?
Ni nani aliye wapa kifua mbele ccm wakati wa kampeni mwaka 2015.

NB: Najua kila mtu alikuwa na wajibu wake kwa wakati wake.
Nape Ndio aliyemuweka kichaa hapo angepigwa risasi tu Sijui kwanini huyo aliemtishia bastora alisita kupiga.....
 
Tena wewe bora unyamaze! kuna kipindi hayo walikuwa wanafanyiwa upinzani mkawa mnaanzisha thread zenu za dhihaka humu ndani!

Mlijua yataishia kwa wapinzani tu?

Zitto na Lissu walionya sana haya mambo mkawaona ni wehu!

Leo yako wapi?
Jifunzeni kutenda mema haijalishi upo upinzani au ccm
 
Ndugu wanajamvi;

Naandika haya kwa masikitiko makubwa sana nikiwa shuhuda kwa mambo yanayotokea katika chama changu na katika taifa langu pendwa.


CCM tujirekibishe kama wafuasi na wanachama wazalendo:

Ni takribani masaa yamepita tokea kwa kuenguliwa kwa waziri wa michezo, sanaa na utamaduni Mhe. Nape lakini cha kushangaza wengine tunajisahau kwa kusifia na kupiga vigelegele, shangwe vifijo na nderemo. Tunajivua akili yetu na kujisahau kabsaa.

NAPE Historia itambeba sikuzote;

Siyo Mara yangu ya kwanza kumwita Nape Shujaa wa mabadilko ndani ya chama na taifa kwa ujumla; Tuanzie na Mzee Nauye mwenyewe Babake Nape, ni mtu aliyetumikia chama kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu bila kuhusishwa na kashfa yoyote ndani na nje ya chama.

Nape alianza mageuzi ndani ya CCM tokea akiwa kijana kwa bahati nzuri alipewa sauti yenye nguvu na high influencing power alikuwa akisikika kukemea maovu hadharani bila kujali usalama wa maisha yake.

Nape aliungana na Kinana katika harakati ya kupambana na CCM maslahi , Nape aliongoza vita ya kuwafukuza wale wote walioitwa wafalme na ma herode kwenye chama bila kujali usalama wa maisha yake.

Mafisadi wote wa CCM ilifika mahali wasikie jina lolote lakini wasisikie jina Nape kwa sababu ya Ideologies zake, Leo hii tunakuwa wepesi tunasahau vita ya 2015 ambapo huyu kijana alinusurika maisha yake kisa tyuuu kufia chama.

Wengine walishinda lakini Leo ukiwauliza walishindaje hawajui leoo, utasikia muuluze J.Makamba, Mwighuru na Nape , leo CCM tunasahau hadi " Goli la mkono" nimefadhaika sana na nimekerwa sanaa.

Wakati hawa vijana wanaweka rehani maisha yao wengine walikuwa wanabadilisha Clubs na makasino na warembo wa bongo, ila wao waliona uhai wao kama ni kitu kidogo ilimradi tuuh CCM ishinde vita.

Leoo hiii Nape anazuiwa kufanya press conference na police CCM tunashangilia naomba mjiulize kwanza Comrade A. KINANA amejisikiaje baada ya haya maswahibu kumpata Nape ndipo angalau turudi kwenye mjadalah huu.

Na lengo la Nape ilikuwa kuja kumshukuru tuuh Rais na kumpongeza waziri mtarajiwa mhe. H.Mwakyembe pamoja na kushukuru vyombo na wadau mbalimbali wa habari. Kama CCM ni mda wa kusimama imara sikuzote na kuwa pamoja kama siku zote hatupo tena kwenye nyakati za kawaida.

Nyie mnaoshangalia jiulizeni kwanza ata Mzee JK amejisikiaje vitu vingine ni kutumia tuuh akili ya kawaida siyo mpaka uweke uwendawazimu kwenye kadamnasi kama hii kama huna la kufanya si uombe utapewa ata ushauri.

Kwako Nape popote ulipo kuna maisha baada ya uwaziri just cool calm watanzania wamekupima ndani ya serikali na nje ya serikali ukiwa mwanachama mtiifu wa CCM just take it easy brother hakuna jambo lisilokuwa na mwisho. Sisi kama CCM tuliopata kulelewa chini ya comrade A. Kinana tupo na wewe daima.

Wengi walipita hakuna atakayebaki milele after all kuna maisha nje ya siasa.

Ni wako kijana mtiifu na mzalendo kutoka Lumumba.

0715829833
Mkuu hapa wewe ndie Lumumba uliyechungulia kidogo!
 
Conference za nini wakati hapa kazi tu. Halafu hoja nyengine unakaa unacheka tu eti nape mpambanaji ideology zake tofauti na wana ccm wengi. Ccm hao hao waliomkataa umoja wa vijana wakamfukuza na mzee makamba akatwambia alofungiwa duniani kafungiwa mpaka mbinguni.ideology gani za matusi na kuwa kipaza sauti cha mines. Malipo dunian akhera huenda hesabu. Tulieni
 
Tena wewe bora unyamaze! kuna kipindi hayo walikuwa wanafanyiwa upinzani mkawa mnaanzisha thread zenu za dhihaka humu ndani!

Mlijua yataishia kwa wapinzani tu?

Zitto na Lissu walionya sana haya mambo mkawaona ni wehu!

Leo yako wapi?
Jifunzeni kutenda mema haijalishi upo upinzani au ccm
Tunapokuwa kwwnye mambo yenye maslahi ya Taifa ni boraa ukaepuka kuweka uchama pembeni Mkuu!!
 
Hii imenikumbusha kitabu kimoja kinaitwa "mfadhilli" duniani hutakiwi kuwa mkwel na mjuaji sasa! Otherwise uwe ni mtu wa kuumia!
 
sina mapenzi na ccm lakini roho imeniuma sana kwa anayofanyiwa nauye, mimi nilikata tamaa tangu october 2015 niliyaona yote haya
 
Tunapokuwa kwwnye mambo yenye maslahi ya Taifa ni boraa ukaepuka kuweka uchama pembeni Mkuu!!
Kwahiyo akiwa wa ccm ni ya kitaifa ila mwingine hayawi ya kitaifa!

Mtatia akili tu
 
Imeniuma sanaa leoo hii Nape ndo wa kutishiwa na Bastola kama nchi tumefika WAP??
Isikuume mkuki kwa ngurue mtamu kwa binadamu mchungu. Upande wa pili wamefanyiwa makubwa zaidi ya hayo, leo kisu kimegusa mfupa inkuuma ? Subiri tutashuhudia mengi zaidi ya hayo.
 
Conference za nini wakati hapa kazi tu. Halafu hoja nyengine unakaa unacheka tu eti nape mpambanaji ideology zake tofauti na wana ccm wengi. Ccm hao hao waliomkataa umoja wa vijana wakamfukuza na mzee makamba akatwambia alofungiwa duniani kafungiwa mpaka mbinguni.ideology gani za matusi na kuwa kipaza sauti cha mines. Malipo dunian akhera huenda hesabu. Tulieni
Mzee siyo kila bandiko ni lazima ucomment zingine ukiona uwezo wa akili yako haiwezi kutafakari kilichoandikwa ni bora upite tyuuh kwa sababu hakuna ata senti uliopewa ili ucomment!!!
 
Wana JF,
Napenda kujua, Kati ya nape na Magufuli nani aliyeisalimisha ccm July 2015 pale Dodoma?
Ni nani aliye wapa kifua mbele ccm wakati wa kampeni mwaka 2015.

NB: Najua kila mtu alikuwa na wajibu wake kwa wakati wake.
Nape na kijana wamefanya kazi kubwa sana kurudisha imani ya chama. Magufuli asingeweza kuwa rais kama kazi ya nape na kinana isingefanyika. Ni mpumbavu tu ambaye atabeza kazi ya nape hata hao wazee wanajua
 
Lumumba naelekea kuifananisha na team bora ilochukua kombe (kushinda uchaguzi 2015) hiyo team ikauza wachezaji wake wote muhimu bila kukumbuka kuna mashindano yanakuja mbeleni (uchaguzi 2020)
Sidhani mtakuja kupambana na wapinzani kuutetea ubigwa wenu kwa kuwatumia wachezaji ambao bado hawajaiva kwa mikiki mikubwa kina pole pole,kina ***** daah mtakuwa MNA Kazi kubwa sana huko mbeleni
 
Kwahiyo akiwa wa ccm ni ya kitaifa ila mwingine hayawi ya kitaifa!

Mtatia akili tu
Tofautisha political issues na mambo yenye maslahi ya Taifa. Ata Mwenyekiti wako amelaani wewe upo busy kusifia ujinga ngojeni tuendelezee taifa lenye watu wanafikiii
 
Halafu huu woga wa Serikali ya bashite unatoka wapi, hebu ona wamemaliza press conference ambayo angeongea na wanahabari kwa akili zao ndogo wanajikita Nape anahutubia mkutano wa hadhara.

Kama mnatenda haki woga ni wa nini! Serikali inalazimisha watu kupenda upinzani, anyway lkn Chama si kishabinafsishwa.
 
Back
Top Bottom