Boniphace Kichonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 1,605
- 1,958
Dear JF Members
You can read it for yourself!
*NAPE MOSES NNAUYE, UFANYE ULIMI WAKO KUWA KIUNGO CHA KUJENGA MSHIKAMANO KATIKA CHAMA NA SERIKALI*
*Na Mkweru Zakaria Maswale*
*Mtama, lindi*
*02/01/2018*
*Salamu* , ndugu zangu Heri ya mwaka *2018* , naungana na wenzangu Wazalendo katika kumshukuru Mungu kuona mwaka huu wenye Neema kwetu.
*Wahenga* wa kale walisema *"Kikulacho ki nguoni mwako"* na wengine wakasema "Adui wa mtu, ni mtu wa karibu yake"
*Kwa wale* wanaofahamu kuhusu maandiko matakatifu ya *Biblia* , wanajua fika kuhusu semi hizi, kwani hata Yesu katika *kukamatwa* , kusulubiwa hadi kuuawa kwake alisalitiwa na mtu wa karibu yake *Yuda Iskarioti* waliyekuwa wakila, kunywa na kulala pamoja.
*Nape Moses Nnauye* mbunge wa Mtama ni miongoni mwa wanachama vijana katika *Chama cha Mapinduzi* waliolelewa na kukulia katika Chama kuanzia Jumuiya ya Umoja wa Vijana hadi kufikia kuaminiwa kupewa nafasi nyeti ya kuwa msemaji wa chama ngazi ya kitaifa, Katibu wa Itikadi na Uenezi na hatimaye kuteuliwa kushika nafasi ya kuwa Waziri kamili wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika serikali ya awamu ya tano kabla ya uteuzi wake kutenguliwa baadaye.
*Nijuavyo kama mwanachama* wa kawaida, na ninaamini hata *Nape Mosses Nnauye* anajua hivyo kwamba mtaji wa kwanza wa chama chochote cha siasa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni rasilimali watu kwa maana ya wanachama.
*Hukuwezi* kuwa na chama cha siasa kisichokuwa na idadi kubwa ya wanachama, kisha chama hicho kikatarajia siku moja kipate ridhaa ya wananchi ili kiunde serikali.
*Sichelei* kusema kwamba tangu mbunge huyu wa chama cha Mapinduzi uteuzi wake wa nafasi ya Waziri ulipotenguliwa amekuwa na kinyongo pamoja na mtazamo hasi dhidi ya chama na hata serikali.
*Kila alipopata* nafasi ya kutoa mchango wake wa maoni, iwe ni bungeni au nje ya bunge, ameitumia nafasi hiyo kuonyesha kilichomo ndani ya nafsi yake dhidi ya chama au serikali.
*Katika kuufunga mwaka 2017* na kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, *Nape Mosses Nnauye* alikuwa ni miongoni mwa wageni walioalikwa katika mjadala kupitia kituo cha luninga cha Azam, na kupitia fursa hiyo, mbunge huyu akaponda vikali swala la wanasiasa na wanachama kuhama chama kimoja cha siasa kwenda kingine kwamba halina mashiko na hata sababu za kuhama kwao wanazozitoa ikiwemo ya kuridhishwa na utendaji kazi wa *Rais Magufuli* hazina maana yoyote.
*Nape* pia akaenda mbali kwa *kukosoa* utaratibu aliyoutumia Rais akiwa kwenye shughuli za kiserikali Jijini Arusha, kugeuza shughuli hiyo na kuwa ya kichama kwa kukubali kuwapokea wanachama wapya waliovihama vyao na kujiunga na *Ccm* .
*Nape Moses Nnauye* alimaliza kwa kuvitaka vyama vya siasa kuwathamini wanachama waliovipigania. Bila shaka hapa alikuwa akijipigia debe yeye mwenyewe, kutokana na kauli zake za huko nyuma kwamba alivunjika mkono na hata kulala chini kwa ajili ya kukipigania chama ambacho kwa maelezo yake alidai kukitoa shimoni.
*Alichosahau* Nape Moses Nnauye ni kwamba, mchezo wa siasa hauna tofauti na michezo mingine ambapo usajili wa wachezaji wenye tija huwa unafanyika kwa ajili ya kuwa na timu bora itakayo kuhakikishia ushindi. Kwa maana hiyo kwenye siasa kukiwa na mchezaji anayeomba kujiunga nanyi na baada ya kupima viwango vyake vya uchezaji, mkaridhika kuna sababu gani ya kutomsajili mchezaji wa namna hiyo bila kujali iwapo anatoka upinzani. Hivyo ndivyo Nape na wewe ulivyosajiliwa kama mchezaji wa kuiwakilisha Ccm katika jimbo la Mtama.
*Baada ya kutazama* maoni ya Nape Moses Nnauye kupitia luninga, nilijaribu kupitia vifungu kadhaa ndani ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi. *Katika Ibara ya 14 inayohusu haki za mwanachama, nikasoma ibara ndogo (2) inayosema:-*
*(2) Mwanachama atakuwa na haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya Ccm pale ambapo anahusika kwa mujibu wa katiba.*
*Kupitia ibara hii* , nimebaini kwamba, Chama cha Mapinduzi kinao utaratibu wa kikatiba kwa wanachama wake kutoa maoni ndani ya mikutano ya wanachama iliyotajwa kikatiba kila mmoja na ngazi yake mahali alipo na siyo kienyeji.
Aidha pia nimepitia katika *Ibara ya 15 inayozungumzia Wajibu wa mwanachama. Katika Ibara hii, ibara ndogo ya (1) inasema:-
(1) Mwanachama atakuwa na wajibu wa kujua kwamba, Chama cha Mapinduzi ndicho chenye nguvu, uwezo, na kwamba nguvu hizo zinatokana na umoja wa wanachama, fikra sahihi za Ccm na kukubalika kwake na umma. Kwa hiyo kulinda na kuendeleza mambo hayo ni wajibu wa kwanza wa kila mwanachama.
*Kupitia ibara hii* nimebaini kwamba, wajibu wa kwanza wa mwanachama wa chama cha Mapinduzi ni kuhakikisha muda wote nguvu ya wanachama inakuwepo, kwa maana kwamba uhai wa chama chochote cha siasa unatokana na kuwepo kwa wanachama hai na uhai huo wa wanachama ndiyo nguvu ya chama kinachotaka kuendelea kushika dola.
*Wakati Rais,* Makamu wa Rais na hata Waziri Mkuu, kwa nyakati tofauti wakiangaika kupokea wanachama wapya na wengine wanaorudi waliokihama huko nyuma, *Nape Moses Nnauye* anajaribu kuuaminisha umma na hata wanachama na mashabiki wa Ccm kwamba, swala la wanachama na wanasiasa wanaovihama vyama vyao kwa vingi kujiunga na Ccm kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ni batili na hata sababu wanazozitoa ni batili.
*Sitaki kuamini* kwamba Nape Moses Nnauye huyu, ndiye yule aliyekuwa Katibu wetu wa Itikadi na Uenezi, ambaye kwa nyakati fulani katika kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinashida uchaguzi, aliwahi kusema watashinda hata kwa kufunga bao la mkono.
*Nataka nimshauri mdogo wangu Nape Nnauye* kwamba, si kila mkulima aliyefyeka pori au msitu, kisha akalima shamba na kupanda mazao, alinufaika na mazao hayo kwa kula mwenyewe bali wakati mwingine walikula watu wengine.
*Inawezekana* kweli uliikuta Ccm na kuitoa shimoni, lakini hiyo haina maana kwamba, madhali ulifanya hivyo basi wewe ndiyo utakuwa alpha na omega kwa kutoguswa hata pale utakapokosea. Kwa maoni yangu, kilichomponza Nape ni mambo mawili, ambavyo ni:-
(1) Utovu wa nidhamu kwa mamlaka yake ya uteuzi. Mara baada ya Rais kutangaza pale Ubungo kumuunga mkono Paul Makonda na kumwagiza aendelee kuchapa kazi, kiutawala kauli ile ilikuwa ni ya mwisho na kamwe Nape hukupaswa kuendelea na zoezi lake la kuunda tume kumchunguza Makonda.
Kitendo cha hatua ya Nape kuendelea na zoezi lile, kwa tafsiri ya Itifaki kiutawala ni kama tume ile aliyoiunda ilikuwa ikimchunguza Rais, hatua ambayo ni sawa na kumtunishia msuli kwa kuwa kauli ya Rais ni ya mwisho.
(2) Alichotakiwa Nape kufanya baada ya Rais kutoa kauli yake Ubungo, angewasiliana na Waziri Mkuu ili kupokea ushauri juu ya nini afanye, kinyume chake yeye aliingia kifua mbele pasipo kusoma mazingira na alama za nyakati kwamba ni Rais wa namna gani anayefanya naye kazi kwa sasa tofauti na mazoea ya huko nyuma.
*Ukiwa bado mwanasiasa kijana* , kama hauna agenda ya siri kuhusu kubakia kwako kwenye medani za siasa, tafuta ushauri wa kisaikolojia utakaokusaidia uendelee kudumu kwenye siasa. Kumbuka hata kukaa kimya ni kufanya siasa pia, si lazima kila kitu uongee.
*Mwisho niwaombe wataalam wa Saikolojia* kumpa ushauri nasihi mbunge huyu ili aachane na siasa za mihemuko ambazo hufanywa na wapinzani, na kama anaona hawezi tena kuishi ndani ya Chama cha Mapinduzi basi aondoke kwa amani na siku akitaka kurejea apokelewe kwa nderemo na vifijo.
Wasalamu kutoka Mtama