Ujumbe kwa Zitto: Umekimbia Nini, Unafanya Nini?

Ujumbe kwa Zitto: Umekimbia Nini, Unafanya Nini?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Ndani ya ACT hakujengwi chama; kunajengwa mtu. Ndani ya ACT hakuna demokrasia, kama kungekuwa na demokrasia kusingekuwa na mgogoro kati “wavamizi” wanaoongozwa na Zitto na genge lake; na wenye chama chao, wanaoongozwa na Lucas Kadawi Limbu, mwenyekiti mwanzilishi wa ACT Tanzania.

Limbu na wenzake leo hii, wako mahakamani kupinga kinachofanywa na Zitto, Prof. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.-

Kama Zitto angekuwa mkweli, asingefanya mapinduzi ya chama kwa kubadilisha katiba kinyemela; falsafa ya chama, kadi za chama, nembo ya chama na jina la chama.

Ndani ya ACT kuna jitihada mahususi za kufukuza waasisi ili kumuandalia mtu mmoja makazi ya kisiasa; na mwenye maslahi binafi.

Nakubaliana na wewe kuwa mwenyekiti wa chama - Anna Elias Mughira, kwa jina jingine, Anna Shadrack Maghiya, siyo lolote siyo chochote. Amefanywa kama boya linaloelea baharini baada ya kukata nanga.

Anayeitwa kiongozi mkuu wa chama, ndiye mkuu wa chama kwenye mikutano mikuu ya chama taifa, Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC). Kiongozi mkuu wa chama, ndiye anayekuwa mkuu wa siasa, mshauri na mwelekezaji kwa viongozi wote na maafisa wa ACT-Tanzania.

Hata nafasi yake – Kiongozi Mkuu wa Chama – hakuna utaratibu wa kuigombea. Je, iko wapi demokrasia ambayo yeye na genge lake wamekuwa wakidai kuipigania?

Mbona mwenyekiti hana mamlaka ya kuagiza, kuteuwa; na au kuelekeza katibu mkuu wa chama ama mfanyakazi mtumishi mwingine wa chama? Madaraka yote yametupwa kwa kiongozi mkuu wa chama.
Iko wapi tofauti ya mfumo wa utawala wa kiongozi mkuu na utawala wa kifalme?-

Katiba ambayo Zitto na wenzake wanatumia inasema, pamoja na mengine, kiongozi mkuu ndiye atateua wajumbe watano wa kamati kuu; ndiye mtoa tamko rasmi kuhusu masuala ya sera na mtazamo wa chama; mtoa habari mahususi kwenye mkutano mkuu, NEC na CC na masuala mengine ya kitaifa na kimataifa.

Kitila na wenzake wanaimba kuwa Zitto sasa ndiye atakuwa “nuru na taswira ya ACT-Tanzania ambayo wamegeuza jina na kuita ACT-Wazalendo."

Katika mifumo ya kidemokrasia, “nuru na taswira” ya chama inakuwa mtu mmoja? Ni kitu gani hasa? Ni “zidumu fikra za Zitto?” Fikra zipi” Ni wanachama kumwacha Zitto awapeleka anakotaka? Ni ufalme wa Zitto?

Inawezekana kuwa hilo ndilo alikuwa anatafuta katika Chadema – na alikiri kuandaa – kupindua uongozi na watendaji ili achukue chama na kubaki dikiteta mkuu katika mfumo anaouita wa kidemorasia?

Yako wapi majigambo ya kupigania demokrasia? Kwa hili, hata wale ambao Zitto anatuhumu udikiteta, hawajawahi kujiundia uungu wa aina hii.
 
ACT haina mwenye chama hii sio CDM na ndio maana limbu na uasisi wake wote ashawekwa pemben koz n mzigo kwa chama hanauwezo na speed ya chama.... hapa hakuna cha mtei....
 
mnaweweseka polen angaluen influence alonayo ZZK ktk utambulosho wa chama songea, makambako na iringa jamaa anatisha.... mlimtabilia kifo cha kisiasa mara mmemvua nguo xaxa ngoja afanye yake na hana muda wa kuwajibu
 
Yetu macho...... tusubiri "Akili kubwa" ifanye mambo....

Ha ha ha haaaa! Umenikumbusha mbali sana alooo; yaani hawa jamaa sijui wanafikiria kwa kutuma masaburi, waraka waliouita wa mabadiliko as such ulikuwa wa kuua nia zao taasisi. Shame on them
 
mnampa umaarufu huyu,mnamuanzishia nyuzi kila siku bila sababu!

waambie wenzako hawajielewi kuna mmoja kakurupuka et threads za ZZK na ACT zianzishiwe jukwaa lingine ha ha haaa anadhan apa n CDM ambapo slaa aliamka na kufunga mjadala wa ZZK anadhan na uku JF kuna ujuha mpen pole lazma demokrasia iheshimiwe xaxa ndo huyu mwingine badala ya kuanzisha uzi mbowe yupo wap anakurupuka et ZZK kwan haon kuwa nyuzi za ZZK zko za kutosha. BUT TUNASHUKURU KWA PROMO. team wazalendo
 
Watu wanashindwa kujua kwamba Katiba Rasmi au Chama Rasmi kimekuwepo wiki 3 zilizopita baada ya national congress before that hakikuwo... So walio mahakamani hawajui watendalo.
 
Hii mimba ya Zitto aliyoacha ufipa mbaya sana, kila mmoja analia yeye hata habari hana, Zitto hebu punguza speed ufipa wamekubebea mimba
 
Last edited by a moderator:
ACT haina mwenye chama hii sio CDM na ndio maana limbu na uasisi wake wote ashawekwa pemben koz n mzigo kwa chama hanauwezo na speed ya chama.... hapa hakuna cha mtei....

Zitto ndio mungu wa ACT - Mazalendo
 
Zzk ni hawezi kujenga taasisi kwasababu hawezi kuwa team leader au kukubali criticisms.

Tabia zake mbaya hasa ubinafsi, kiburi na dharau hawezi kujenga taasisi. anakwisha kijana mzee kwa matendo.

hana team leadership ha ha haa kwel ww ndo haun ipo wap PAC ya ZZK?
 
Mbowe amebadili katiba ili atawale milele misukule ya Chadema iko kimya kisa chama cha mkwe wake
 
Back
Top Bottom