Ujumbe kwa wanaume

Hapa swala siyo kujilinganisha ila swali langu ni hili kwahiyo wanaume mnafanya maovu kwa makusudi kwa misingi ya kwamba wanawake hawawezi kuwalipizia si ndiyo?
Wanaume hawafanyi kwa makusudi endapo kama wana akili zao timamu, ila ikitokea amefanya kosa hilo na wewe ukafanya vile vile kwa kulipiza utakuwa ni mpuuzi sana na ndio kujilinganisha kwenyewe.
 
Nenda kalipize uzinzi kwa kufanyiwa uzinzi kama ambavyo nimekwisha elezea hapo juu, ndio utafahamu kama kweli jamii haina impact yoyote kwenye maisha yako.
 
I don't cheat but I teach. I teach them that I am a real man. Hivi, mwanamke akinichukulia mimi mpumbavu napungukiwa na nini! Mke wangu ni mke wangu, akiniona mimi ni mpumbavu kisa nina mwanamke mwingine, yeye tu kuchagua asuke au anyoe.
 
I don't cheat but I teach. I teach them that I am a real man. Hivi, mwanamke akinichukulia mimi mpumbavu napungukiwa na nini! Mke wangu ni mke wangu, akiniona mimi ni mpumbavu kisa nina mwanamke mwingine, yeye tu kuchagua asuke au anyoe.
Unapungukiwa akili maana upumbavu ni kupungukiwa maarifa.
"Asuke au anyoe" Unaona sasa
haya si maneno ya kipumbavu
 
Wanaume hawafanyi kwa makusudi endapo kama wana akili zao timamu, ila ikitokea amefanya kosa hilo na wewe ukafanya vile vile kwa kulipiza utakuwa ni mpuuzi sana na ndio kujilinganisha kwenyewe.
Na vipi ikitokea mwanamke ndo akaanza kulifanya kabla ya mwanaume huyo mwanaume anatakiwa afanyaje?
 
haya sasa wapumbavu....ata baba janet aliwaita watu wapumbavu....kwaiyo wapumbavu endeleeni kucheat wake zenu mnawaona wapumbavu, na wanaocheat na wanaume wa wezao ndo hawa hawa wanaona waume wao wakicheat ni wapumbavu...........pumbavuu sana
 
Samahani kama nitakachosema kitakuwa kimeonwa na wenzangu maana message nimeiona leo? Swali je ukiwa hujaolewa umeshaplan nani atakuoa? Hivi unajua ratio ya idadi ya watu namba ya wanawake iko juu kuliko ya wanaume. Tukishajua kwamba wanaume ni wachache kuliko wanaume na wewe hujaolewa na chukulia kila mwanaume achukue mwanamke mmoja, je ukikosa mwanaume utajisikiaje? Je ni halali ukae bila mwanaume, uzeeke bila mtoto maana wanaume wote wameoa mke mmoja niambie utajisikiaje? Ukishajibu ilo uone kwamba wanaume kuwa na nyumba ndogo ni msaada kubalance wiano ulipo
 
Nmeongelea swala la adabu, kuheshimu wake zenu
Mimi kuzeeka bila mume its okay si ndo Mungu kapanga sasa.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Nmeongelea swala la adabu, kuheshimu wake zenu
Mimi kuzeeka bila mume its okay si ndo Mungu kapanga sasa.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Unataka adabu gani. Hata kwenye vitabu imeandikwa wanawake wapendeni waume zenu, na nyie waume waheshimu wake zenu. Kwa kukuheshimu nachepuka bila kukwambia na nikirudi nyumbani nakuheshimu. Wewe ukianza kuchunguza nimekwenda wapi ndio kukosa adabu. Wewe unayechunguza ndiye unacheat, unacheat kwa kuchungulia visivyokuhusu.
Lakini kama unaona unaweza kuishi bila mwanaume haya unayoandika yanakuhusu nini, kwani wanawake wamekulalamikia kwamba waume zao wanacheat njoo uwasemee. Subiri muda wako ufike. hata hivyo umeshasema huna haja na mwanaume. Basi wewe ni kilema
 
Wanaume nawashangaaga sana mnavyosema kuwa mnataka kuwa na wanawake zaidi ya mmoja eti kwa sababu duniani wanawake ni wengi kuliko wanaume hivi mnadhani kila mtu alikuja hapa duniani kutimiziwa haja zake zote na mahitaji yake yote?

Ingekuwa hivyo basi kusingekuwa na watu masikini Mungu angemfanya kila mtu tajiri ili kila mtu awe na maisha mazuri maana hakuna anayependa kuishi maisha mabaya lakini jiulize mbona kuna watu wanakufa masikini?

Vivyo hivyo hata kwenye mahusiano lazima kuna wanaume wanakufa hawajaoa na lazima kuna wanawake wanakufa hawajaolewa ndivyo dunia ilivyo ili maisha yabalance lazima kuwe na waliopata na waliokosa yaani matajiri na masikini, waliooa/walioolewa na wasiooa/wasioolewa

Cha msingi ninyi fuateni maandiko yaliyosema kuwa kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe hayo mengine ya wanawake ambao hawaolewi sijui watajisikiaje hayawahusu mbona hamuwawazii masikini wasio na mali kuwa wanajisikiaje mkawasaidia? Acheni kutafuta sababu za kuendekeza na kuhalalisha uzinzi wakati ni dhambi
 
Makubwa haya
mzee em relax kwanza uongee taratibu
 
Ona hata ambavyo haujui maandiko hadi unaandika vice versa maandiko yanasema mwanamume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe yaani unatetea hoja zako kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu acheni kuchepuka ni dhambi ukichepuka do it at your own risk

Ila usisingizie sijui Mungu kawaruhusu sijui wanawake ni wengi kuliko wanaume nipe andiko linaloruhusu mwanaume kusaliti ndoa au kuoa mke zaidi ya mmoja na pia usije kunitolea mifano ya watu kama kina Solomon na David kuwa sijui walioa wake wengi wakati nao walipewa adhabu na walitubu dhambi zao
 
Ebu nitafutie hicho kifungu cha kusema mwanamke mmoja kwa mwanaume mmoja
 
1 Wakorintho 7 : 2 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe"
Ebu nitafutie hicho kifungu cha kusema mwanamke mmoja kwa mwanaume mmoja
 
Lameki katika Mwanzo 4:19 "Lameki alioa wanawake wawili" , Ibrahimu, Yakobo, Daudi, Sulemani, na wengine, wote walikuwa na wake wengi.
Katika 2 Samweli 12:8, Mungu, akizungumza kupitia ya nabii Nathani, alisema kwamba kama wake na mahawara wa Daudi hawakuwa wa kutosha, naye angempa Daudi zaidi. Sulemani alikuwa na wake 700 na masuria 300 (kimsingi wake wa hali ya chini). Kwa hiyo, inaonekana kwamba Mungu aliweza kuruhusiwa mitala kulinda na kukimu wanawake ambao hawakuweza kupata mume kwa vyovyote vile. mitala iliwezesha upanuzi wa jamii kwa kasi zaidi, kutimiza amri ya Mungu ya "Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake" (Mwanzo 9:7). Wanaume wana uwezo wa kuwatia mimba wanawake wengi katika kipindi kimoja, na kusababisha ubinadamu kukua kwa kasi zaidi kuliko kama kila mume alikuwa tu anazalisha mtoto mmoja kila mwaka.
 
1 Wakorintho 7 : 2 "Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe"
Kwa hiyo unataka kuniambia vitabu kwenye Agano la Kale tusivisome?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…