Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,813
- 59,306
...kuna ule msemo watu wanasema huyu uliyemuoa wala sio type yako,....
hebu mtu mzima ichambue hii, naamini ushawahi isikia...!
Naweza na mie nikajaribu kujibu? Pleaaaaase. . . .!!
Nwy acha nijibu tu.
Wanaweza wakawa sahihi kwa maoni yao kwasababu wanaona zile tofauti. Wapo watu wanaotofautiana sana lakini tofauti zao ndio zikawafanya waelewane sana. Yani tofauti za mmoja zikiwekwa na za mwenzake zinatengeneza kitu kilichokamilika.
https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/164443-mimi-na-wewe.html#post2369774
Niliwahi kuanzisha mada inayosema sisi ni kama vipande vya puzzles, tulivyo, tabia zetu, muonekano, akili, fikra ndio hivyo vipande vya puzzles. Na tunapochagua wenzi tunatakiwa tuangalie ambae vipande vyetu vitaendana na vyao kutengeneza picha kamili.
Wengine, kutokana na walivyo inabidi wapate wanaofanana nao, wengine tofauti ndizo zitakazowaweka pamoja. Ukilazimisha kwa mtu unaefanana nae (kama hao walimwengu wanavyotaka) wakati kiukweli unahitaji wa tofauti ndipo matatizo huanza. Ndio maana mimi nadhani ni muhimu watu wakachagua wenyewe kuendana na mataka/mahitaji yao bila ya kujali walimwengu wanawaonaje pamoja.