Ujumbe kwa rafiki yangu

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Habari zenu WanaJF:

Ujumbe huu ni kwa rafiki yangu na wengine wenye tabia kama zake. Mtaniuliza kwanini nisimfuate nimwambie uso kwa uso, mwanamke yule anaongea akinisema na jinsi sina maneno mengi nitazimia..

Kwanza nikushukuru rafiki kwa huduma yako jana usiku loh nilienjoy kwa kweli.. Japo uliniharibia furaha yangu na nikaondoka kwako nikiwa na mawazo na sikupata usingizi usiku kucha rafiki..

Kumbuka kauli hii niliyokuambia wakati naondoka "JIREKEBISHE MAISHA HAYAENDI HIVI" ukacheka na kuniambia umeanza na mie nikakuaga na kuondoka..

Shoga kilichoninyima usingizi kikubwa ni hich, mwanao anapata haja kubwa wewe unamwita housegirl wako kwa sauti na kwa ugomvi huku umekishika mtoto mkono mmoja na mguuu mmoja umemning'iniza kama mtoto si wako, nilishtuka nikasema umeona nyoka nini ndani ? kumbe mwanao kapooo si vizuri hivyo ...

Mtoto anashikwa na housegirl anafurahi kuliko ulivyokuwa umeshika wewe jamani si vyema.... Najiuliza kama mwanao anapoo unamtreat hivyo hg yeye anaroho gani ya kuchezea kinyesi cha mtoto wa mwingine? Ukifanya mchezo katapata UTI sababu hujui hata kama anasafishwa vizuri mtoto.... Niliumia kama uligundua pamoja na kuwa wine ilianza kuchanga ila nilikuwa down sana ghafla narudia tena si vizuri vile..

Unalalamika ndoa yako ina matatizo lakini kiukweli kwa tabia ile kufoka foka na ya kufuliwa hadi chupi kazi ipo my dear acha punguza hayo makucha yako anza kufua vichupi vyenu au nunua washing machine uwe unafua na si kumpa hg hapo umepitiliza mpenzi..

Fanya siku moja moja angalia usafi wa nyumba yako pika na wewe acha kuwa kama remote controller we unabonyeza tu kinakuja jana umenichosha jinsi unavyoita weeee unafoka foka mpaka sura umeanza kuzeeka wewe....

Kiukweli nyumba yako haina amani kabisa japo we unajiona upo sawa ila unapoteza mpenzi wangu.. Narudia tena JIREKEBISHE MPENZI".

Ukipiga simu yako sipokei, whats app nipo off labda email.. Nakupenda sana rafiki yangu..

Weekend njema!
 
Kati ya wanawake ambao siwapendi ni wa kukaa na kuagiza agiza tu..
Utaskia nipe kijiko
Kaniletee kikombe mara sio hicho rudisha
Kanichukulie simu kitandan

Sio majumbani hadi kazini wapo...utaskia mkwe ebu kanichukulie keki na popcorn pale kwa bwashe.

JIREKEBISHENI TUNAWAVUMILIA SAANA
 
heri umetoa ya moyoni hapa maana kukaa na dukuduku sio vzur ila hata kama atakusema tafuta siku moja pia umwambie ukwel mkiwa wote
 
Ngoja nimuite wifi/shemeji yenu mpya akuje hapa ajifunze machache
 
Back
Top Bottom